{"id":4429,"date":"2023-05-07T19:40:07","date_gmt":"2023-05-07T19:40:07","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/?p=4429"},"modified":"2023-05-07T19:40:10","modified_gmt":"2023-05-07T19:40:10","slug":"watu-130-waliofariki-kwa-mafuriko-rwanda-wazikwa","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=4429","title":{"rendered":"WATU 130 WALIOFARIKI KWA MAFURIKO RWANDA WAZIKWA"},"content":{"rendered":"\n<p class=\"wp-block-paragraph\">MASHIRIKA YA HABARI YA KIMATAIFA<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">WATU 130 waliofariki dunia baada ya kukumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha siku ya Mei 4, usiku katika mikoa ya Magharibi na Kaskazini mwa Rwanda wamezikwa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Rwanda na mashirika ya habari ya kimataifa, watu hao walizikwa katika Mji wa Rubavu ulioko Magharibi ya Rwanda na mazishi yao yaliongozwa na Waziri Mkuu, Dk. Edouard Ngirente.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Akizungumza wakati wa mazishi, Dk. Ngirente alisema idadi ya vifo inaweza kuongezeka kwa sababu bado miili mingine ya watu wanaohofiwa kufariki katika mafuriko hayo inaendelea kutafutwa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cKuna watu ambao tunaendelea kuwatafuta na huenda idadi ya waliokufa ikaongezeka. Kusema ukweli hili ni janga lililoiangukia nchi yetu kwani maji mengi ya mvua yaliyomomonyoa udongo na kusababisha nyumba kuwaangukia watu.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cTunatambua uchungu na matatizo mnayoyapata, Serikali itajitahidi kuwapa msaada kadri inavyowezekana na mimi niko hapa kumwakilisha Rais ambaye kuanzia jana amekuwa akiwapa taarifa kuhusu msimamo wa Serikali,\u201d alisema Dk. Ngirente.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Watu hao hao walifariki dunia baada ya kunyesha mvua kubwa iliyosababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi.<\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"457\" height=\"300\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2023\/05\/mafuriko-rwanda.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-4431\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/05\/mafuriko-rwanda.jpg 457w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/05\/mafuriko-rwanda-300x197.jpg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/05\/mafuriko-rwanda-150x98.jpg 150w\" sizes=\"auto, (max-width: 457px) 100vw, 457px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kwa mujibu wa Sauti ya Amerika (VOA), baadhi ya watu waliopoteza ndugu zao walieleza kuwa waliofariki dunia walifunikwa na vifusi vya nyumba na kingo za mlima.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cKifusi kilianguka na kutufunika mimi na mume wangu na mtoto wetu, nilipozinduka nikaona mimi kichwa changu bado kinaonekana ndipo mume wangu akaanza kunivuta lakini tulipoangalia vizuri alipokuwa amelala mtoto wetu tukakuta yeye kimemfunika kabisa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cTukajaribu kuondoa matofali lakini tulishindwa, mimi nikapanda ukuta kwenda nje kuomba msaada,\u201d alisema mmoja wa watu walionusurika.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Gashonga Jean Marie Vianney ambaye alinusurika katika mkasa huo alisema amepoteza watoto watatu wa kike.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cKifusi cha mlima kilimeguka na kuangukia nyumba yetu upande wa juu karibu na chumba cha watoto wangu wa kike na wa kiume na mara moja kikafunika chumba cha watoto wangu watatu wa kike waliokuwa pamoja ambao walifariki papo hapo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cUpande wa chumba cha wavulana wao waliweza kujivuta wakatoka na ndiyo waliomsaidia mama yao kumuondoa kwenye kifusi kilichokuwa kimemfunika,\u201d alisema Vianney.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Tayari Serikali ya Rwanda imepeleka msaada wa tani 60 za chakula kwa waathirika ambao wengi wao wamehifadhiwa kwenye majengo ya shule na makanisa na baadhi wamepewa hifadhi na jamaa na marafiki.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Sambamba na hilo, Serikali ya Rwanda imeanza kuzihamisha familia 137 kutoka maeneo hatarishi na imewataka raia wake wanaoishi maeneo yaliyo jirani na kingo za milima mirefu kuhama kwenye maeneo hayo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Naye Waziri wa Usimamizi wa Masuala ya Dharura wa Rwanda, Marie Solange Kayisire aliwataka watu wote kuwa katika hali ya tahadhali na wanaoishi karibu na kingo za milima mirefu kuhama ili wasije kuangukiwa na kingo za milima.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Mwaka 2020, zaidi ya watu 80 walifariki dunia nchini Rwanda kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa na tangu wakati huo Serikali ya Rwanda imekuwa ikifanya kazi ya kuwahamisha watu wenye makazi katika maeneo hatarishi na kuwajengea makazi mengine mapya.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Hii ni mara ya kwanza kwa Rwanda kupoteza idadi kubwa ya raia wake kwa usiku mmoja kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>MASHIRIKA YA HABARI YA KIMATAIFA WATU 130 waliofariki dunia baada ya kukumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha siku ya Mei 4, usiku katika mikoa ya Magharibi na Kaskazini mwa Rwanda wamezikwa. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Rwanda na mashirika ya habari ya kimataifa, watu hao walizikwa katika Mji wa Rubavu ulioko [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":4430,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[74],"tags":[],"coauthors":[],"class_list":["post-4429","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-habari-kimataifa"],"amp_enabled":true,"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/05\/nda.png","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/4429","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=4429"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/4429\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":4432,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/4429\/revisions\/4432"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/4430"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=4429"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=4429"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=4429"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=4429"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}