{"id":429,"date":"2021-12-02T13:39:00","date_gmt":"2021-12-02T13:39:00","guid":{"rendered":"https:\/\/msangirstz8.wordpress.com\/2021\/12\/02\/mikopo-ya-trekta-yawaliza-wakulima\/"},"modified":"2021-12-02T13:39:00","modified_gmt":"2021-12-02T13:39:00","slug":"mikopo-ya-trekta-yawaliza-wakulima","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=429","title":{"rendered":"MIKOPO YA TREKTA YAWALIZA WAKULIMA"},"content":{"rendered":"<table align=\"center\" cellpadding=\"0\" cellspacing=\"0\" class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/829a3-tractor.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"480\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/829a3-tractor.jpg?resize=640%2C480&#038;ssl=1\" width=\"640\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align:center;\">Trekta aina ya New Holland<\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<p>\u00a0<!--[if gte mso 9]&gt;   Normal  0          false  false  false    EN-US  X-NONE  X-NONE                                       MicrosoftInternetExplorer4                                     &lt;![endif]--><!--[if gte mso 9]&gt;                                                                                                                                                                                                                                                                                    &lt;![endif]--><!--[if gte mso 10]&gt; \/* Style Definitions *\/  table.MsoNormalTable \t{mso-style-name:\"Table Normal\"; \tmso-tstyle-rowband-size:0; \tmso-tstyle-colband-size:0; \tmso-style-noshow:yes; \tmso-style-priority:99; \tmso-style-qformat:yes; \tmso-style-parent:\"\"; \tmso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt; \tmso-para-margin-top:0in; \tmso-para-margin-right:0in; \tmso-para-margin-bottom:10.0pt; \tmso-para-margin-left:0in; \tline-height:115%; \tmso-pagination:widow-orphan; \tfont-size:11.0pt; \tfont-family:\"Calibri\",\"sans-serif\"; \tmso-ascii-font-family:Calibri; \tmso-ascii-theme-font:minor-latin; \tmso-fareast-font-family:\"Times New Roman\"; \tmso-fareast-theme-font:minor-fareast; \tmso-hansi-font-family:Calibri; \tmso-hansi-theme-font:minor-latin; \tmso-bidi-font-family:\"Times New Roman\"; \tmso-bidi-theme-font:minor-bidi;} &lt;![endif]--> <\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>RIPOTA PANORAMA<\/span><\/span> <\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>0711 46 49 84<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>WAKULIMA mkoani Morogoro wameilalamikia kampuni inayojihusisha na ukopeshaji wa magari, trekta na mashine za aina mbalimbali ya Equity for Tanzania Limited (EFTA) kuwa inawakandamiza na kuwanyonya katika mikopo inayotoa.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Wamedai kuwa EFTA ambayo katika Mkoa wa Marogoro imejikita zaidi kukopesha wakulima trekta, inawatoza riba kubwa na kwa kutumia \u2018upofu\u2019 wa sheria wa wakulima wengi wanaoingia mikataba ya kukopeshwa trekta na kampuni hiyo, inawanyonya na kuwakandamiza.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Akizungumza na Tanzania PANORAMA Blog jijini Dar es Salaam hivi karibuni, mmoja wa wakulima hao, Miraji Salehe Hassan aliyekopeshwa trekta na EFTA, alidai kampuni hiyo imemkoposhe trekta hilo mara mbili huku ikimtoza riba kubwa na pesa ya malimbikizo ya mkopo.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Hassan alisema kwa mara ya kwanza alikopa trekta kwa EFTA, Septemba 27, 2017 kwa ghamara ya shilingi milioni 48 na kulipa malipo ya awali shilingi milioni 10, lakini baadaye alianza kuandamwa na maofisa wa kampuni hiyo akidaiwa riba ambayo haipo kwenye mkataba wake ulioandikwa kwa Lugha ya Kiingereza pamoja fedha ya kuchelewesha marejesho.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cMimi nilikopa trekta kwa Kampuni ya EFTA Septemba 27, 2017. Thamani ya mkopo wa trekta hiyo ambayo siyo mpya bali imekwishatumika ilikuwa shilingi milioni 48 na nilitakiwa kulipa malipo ya awali shilingi milioni 10. Nilisaini mkataba ambao ulikuwa umeandikwa kwa Lugha ya Kiingereza na nililipa shilingi milioni 10 ambazo ni malipo ya awali, wakanipa nikaendelea na shughuli zangu.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cKuna kipindi kweli nilikuwa nachelewa kulipa kwa sababu hizi shughuli zetu za kilimo nadhani unafahamu wakati mwingine mazao yanagoma kutokana na msimu kuwa mbaya lakini nililipa deni la msingi lote. <\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cWao EFTA wakasema ingawa nimelipa deni la msingi lakini bado ninadaiwa riba na pesa ya malimbikizo hivyo nilipe madeni hayo kwa pamoja vinginevyo nanyang\u2019anywa trekta langu. Nikaenda na ule mkataba kwa wenzangu wanaojua kizungu ili waone masharti hayo wakasema hawaoni kipengele cha riba ila cha kuchelewesha malipo kipo. Nikachanganyikiwa kabisa kwa sababu mimi sijui kiingereza lakini mkataba wao nilisaini.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cNikawarudia nikawaambia sawa nitalipa hizo pesa lakini wanipe muda kidogo, wakagoma wakasema muda wa kufanya marejesho umeishaisha hivyo kama bado nataka hilo trekta inabidi nianze upya mchakato wa kukopa. Basi nikaanza upya taratibu za kukopa trekta lile lile ambalo nilikuwa nimekopa awali na kulipa mkopo wote kasoro riba kidogo na hicho wanachoita wao tozo ya ucheleweshaji marejesho.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cWakanipa mkataba mpya wa kukopa tena hilo trekta ambao thamani yake ilikuwa shilingi milioni 26. Mkataba mpya nilisaini Disembe 22, 2020, nikaanza kulipa upya huo mkopo na riba wakati ule wa mwanzo nao nilikuwa nadaiwa tena kulipa riba ya tozo ya malimbikizo. Hapo sijui sasa taratibu au sheria ya mikopo inasemaje maana hela yote ya kilimo inaishia kwa hawa EFTA,\u201d alisema Hassan.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Taarifa za ziada ambazo Tanzania PANORAMA Blog imezikusanya kuhusu utata wa mkopo wa trekta hilo, zinadai kuwa Hassan alikopa trekta lililotumika, aina ya New Holland \u2013 TT 75- 4 WD, \u2018model\u2019<span>\u00a0 <\/span>8000 &#8211; series 75 HP,<span>\u00a0 <\/span>lenye thamani ya shilingi milioni 48 kwa Kampuni ya EFTA.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Kwa mujibu wa taarifa hizo, Hassan alilipa mkopo wote na kiasi kikubwa cha riba na tozo ya malimbikizo lakini EFTA walimnyang\u2019anya trekta hilo kwa kile walichodai amekiuka mkataba kwa kuchelewa kukamilisha malipo ya tozo ya malimbikizo na kumpa masharti aingie mkataba mwingine mpya wa kukopa trekta hilo.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Nyaraka kadhaa ambazo Tanzania PANORAMA Blog imeziona zinaonyesha kuwa Hassan alisaini mkataba mwingine wa kukopeshwa trekta aina ya New Holland TT75 \u2013 4 WD lenye thamani ya shilingi milioni 26. Hata hivyo mkataba huo wa pili ulioandikwa kwa Lugha ya Kiswahili hauonyeshi baadhi ya maelezo ya trekta kama ule wa mwanzo ulioandikwa kwa Lugha ya Kiingereza.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Taarifa zinadai zaidi kuwa Hassan alilipa shilingi milioni 10 kwa mujibu wa mkataba huo mpya na baadaye alilipa shilingi milioni tatu lakini aliamua kusitisha kulipa baada ya EFTA kumtaka alipe pia gharama za mahakama za kesi ya mgogoro wa trekta ambayo Hassan mwenyewe amekana kuifahamu na kwamba hajawahi kufika mahakamani kwa ajili ya kesi ya trekta baina yake na EFTA.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Tanzania PANORAMA Blog ilifika katika ofisi za EFTA zilizopo jengo la Sky, ghorofa ya tano, makumbusho Dar es Salaam na kukutana na Afisa Uwekezaji aliyejitambulisha kwa jina la Ismail Matete <span>\u00a0<\/span>ambaye alipoulizwa kuhusu madai hayo, alisema kinachoangalia katika hilo ni mkataba baina ya mkopaji na mkopeshaji unaelekeza nini na ndicho kinachofuatwa.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Kwa maneno yake mwenyewe alisema, \u201cHivi ni vitu vya kimkataba, mikataba ipo na ina masharti yake na sisi ndiyo tunayoyasimamia. Mteja kabla hajasaini mkataba anausoma kwanza ndiyo tunaingia kwenye biashara. Tuna taratibu zetu.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cHilo wanalodai kuuziwa trekta mara mbili hizo ni taratibu za kifedha, popote pale kama mteja anakiuka masharti ya mkataba hatua zinachukuliwa kulingana na mkataba wake. Taasisi zote za kifedha zinafanya hivyo kama mtu anakiuka masharti ya mkataba. Lakini vinginevyo kikawaida tu kama mtu hajakiuka mkataba wake sitaki kuamini kama anaweza kukopeshwa bidhaa moja, mara mbili. Na sisi mikataba yetu inaeleza wazi kuwa riba yetu ni asilimia 2.63.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cNa iko hivi kwa mkopaji. Kwenye kulipa deni, kama kutakuwa na malimbikizo, anapolipa kinachokatwa kwanza ni riba, kisha tozo ya malimbikizo na baadaye fedha inayosalia ndiyo inaingizwa kwenye deni la msingi,\u201d alisema Matete.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span><\/p>\n<table align=\"center\" cellpadding=\"0\" cellspacing=\"0\" class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/16d28-bot.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"325\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/16d28-bot.jpg?resize=640%2C325&#038;ssl=1\" width=\"640\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align:center;\">Benki Kuu ya Tanzania (BoT)<\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<p>\u00a0<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Tanzania PANORAMA Blog imezungumza na afisa mmoja wa Benki ya Tanzania (BoT) (jina lake tunalihifadhi) kuhusu sakata hilo ambaye alieleza kuwa jambo kubwa linaloangaliwa katika biashara ya kukopesha ni mkataba na kwamba mkopaji kutojua sheria hakumpa nafasi ya kutotekeleza masharti ya mkataba iwapo ameusaini.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cEFTA inasimamiwa na BoT, hilo nalifahamua na sina shaka nalo. Katika hilo unalouliza, kinachoangalia kwanza hapo ni mkataba unasema nini. Kama mkopaji alisaini mkataba hata kama hajui Kiingereza muhimu ni kwamba alisaini basi analazimika kutekeleza masharti ya mkataba husika.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cLakini hayo unayoyasema ni mambo mazito sana ambayo nasita kuamini kuwa ni kweli yamefanywa na EFTA, siamini hata kidogo kuwa wamemkopesha mkopaji wao kwa mikataba miwili. Naweza kuongea vizuri na rasmi nikiiona mikataba hiyo, yote miwili.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cNinachotaka uelewe, usilichukulie kirahisi hili jambo, hiyo ni taasisi ya kifedha sasa kama kuna jambo wanakiuka au kuna ujanja ujanja wa aina yoyote ile kwenye mikataba yao na wateja wakati wanasimamiwa na BoT, ikibainika, matokeo yake siwezi kuyasema hapa. <\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cUmeanza wewe, baadaye likisambaa hili watadaka wengine kwa sababu ya uzito wa sekta ya fedha na wakulima. Kwahiyo kama nilivyosema niletee kwanza hiyo mikataba niione na nipate maelezo ya kutosha ya wanaolia hao, baada ya hapo ndiyo nitasema au BoT itasema,\u201d alisema.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span><span>\u00a0<\/span><\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span>\u00a0<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span>\u00a0<\/span><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Trekta aina ya New Holland \u00a0 RIPOTA PANORAMA 0711 46 49 84 WAKULIMA mkoani Morogoro wameilalamikia kampuni inayojihusisha na ukopeshaji wa magari, trekta na mashine za aina mbalimbali ya Equity for Tanzania Limited (EFTA) kuwa inawakandamiza na kuwanyonya katika mikopo inayotoa. Wamedai kuwa EFTA ambayo katika Mkoa wa Marogoro imejikita zaidi kukopesha wakulima trekta, inawatoza [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":false,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[1],"tags":[34],"coauthors":[],"class_list":{"0":"post-429","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","6":"category-uncategorized","7":"tag-habari"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/429","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=429"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/429\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=429"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=429"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=429"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=429"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}