{"id":4225,"date":"2023-03-31T20:28:22","date_gmt":"2023-03-31T20:28:22","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/?p=4225"},"modified":"2023-03-31T20:28:25","modified_gmt":"2023-03-31T20:28:25","slug":"waziri-mkuu-akagua-uwanja-wa-ndege-terminal-i","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=4225","title":{"rendered":"WAZIRI MKUU AKAGUA UWANJA WA NDEGE TERMINAL I\u00a0\u00a0"},"content":{"rendered":"\n<p class=\"wp-block-paragraph\">RIPOTA WA WAZIRI MKUU<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua uwanja wa ndege wa&nbsp;<em>Terminal I<\/em>&nbsp;ili kujiridhisha na kazi ya ukarabati unaoendelea kwenye eneo la kuegesha na kufanyia matengenezo ya ndege za Serikali.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Akiwa uwanjani hapo, aliwataka viongozi na wafanyakazi wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) kuhakikishe wanashirikiana na mamlaka husika kuufanya uwanja huo wakati wote kuwa nadhifu ili kukidhi hadhi ya viongozi wa kitaifa na kimataifa wanaoingia ama kuondoka nchini.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Akizungumza na viongozi na watumishi wa TGFA mara baada ya kufanya ukaguzi huo Machi 28, mwaka huu,&nbsp;jijini Dar es Salaam,&nbsp;Majaliwa alimuagiza Mkurugenzi Mkuu wa&nbsp;<a><\/a>TGFA, Mhandisi John Nzulule kuhakikishe ujenzi huo unakamilika haraka.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cSerikali ilishatoa kibali kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa karakana hiyo ambayo nimeelezwa itakapokamilika itawezesha kuegesha ndege kubwa mbili kwa wakati mmoja pale zinapohitaji matengenezo,\u201d alisema.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Majaliwa aliwaagiza Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwan Kikwete na Katibu Mkuu wa Utumishi, Juma Mkomi wafuatilie maslahi na motisha za watumishi wa taasisi hiyo ili kuinua ari yao ya utendaji kazi.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Mapema,\u00a0akimkaribisha Waziri Mkuu Majaliwa kuzungumza na watumishi hao, Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwan Kikwete alisema Serikali ilitoa Shilingi bilioni 2.5 za ujenzi wa awamu ya kwanza ya ofisi za TGFA ambao umekamilika na ofisi zimeanza kutumika.<\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"285\" height=\"177\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2023\/03\/PM-AIRFPORT-2.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-4227\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/03\/PM-AIRFPORT-2.jpg 285w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/03\/PM-AIRFPORT-2-150x93.jpg 150w\" sizes=\"auto, (max-width: 285px) 100vw, 285px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kwa upande wake&nbsp;Afisa Mtendaji Mkuu wa TGFA, alisema kukamilika kwa jengo hilo kumesaidia kuboresha utekelezaji wa majukumu ya wakala kwa idara zilizopo uwanja wa ndege kwa kuwa lina nafasi za kutosha na mifumo ya kisasa kwa ajili ya marubani, wahandisi, wahudumu wa ndege na watumishi wengine.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Alisema awamu ya pili ya ujenzi inahusisha ujenzi wa eneo la kuegesha na kufanyia matengenezo ya ndege na inatarajiwa kuanza hivi karibuni kwa sababu kibali cha ujenzi kimeshapatikana.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cTaratibu za kumpata mkandarasi zimeshakamilika na taratibu zote za kimkataba zimekamilika. Tunaahidi kusimamia kazi hii ili kupata thamani halisi ya fedha (value for money) katika mradi huu,\u201d alisema.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>RIPOTA WA WAZIRI MKUU WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua uwanja wa ndege wa&nbsp;Terminal I&nbsp;ili kujiridhisha na kazi ya ukarabati unaoendelea kwenye eneo la kuegesha na kufanyia matengenezo ya ndege za Serikali. Akiwa uwanjani hapo, aliwataka viongozi na wafanyakazi wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) kuhakikishe wanashirikiana na mamlaka husika kuufanya uwanja huo wakati wote [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":4226,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[],"class_list":["post-4225","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-habari-kitaifa"],"amp_enabled":true,"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/03\/PM-AIRPOTT.jpg","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/4225","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=4225"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/4225\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":4228,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/4225\/revisions\/4228"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/4226"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=4225"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=4225"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=4225"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=4225"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}