{"id":4152,"date":"2023-03-16T07:52:11","date_gmt":"2023-03-16T07:52:11","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/?p=4152"},"modified":"2023-03-16T08:07:57","modified_gmt":"2023-03-16T08:07:57","slug":"kikosi-cha-utekaji-utesaji-chadema-chaanikwa","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=4152","title":{"rendered":"KIKOSI CHA UTEKAJI, UTESAJI CHADEMA CHAANIKWA"},"content":{"rendered":"\n<p class=\"wp-block-paragraph\">RIPOTA PANORAMA<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kina genge la kihalifu kinalolitumia kuteka, kutesa, kushambulia watu na kuwamwangia tindikali. Tanzania PANORAMA Blog imeelezwa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Tuhuma hizi zimeanikwa na baadhi ya waliokuwa viongozi waandamizi wa Chadema ikiwa ni siku chache tu baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa kukaririwa na chombo kimoja cha habari akieleza kuwepo kwa vitendo vya kihalifu ndani ya chama hicho alipokuwa akizungumzia shambulio la kupigwa risasi kwa Makamu Mwenyekiti wa chama hivyo, Tundu Lissu.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Akizungumza na Tanzania PANORAMA hivi karibuni kuhusu Chadema kuwa na kundi linalojihusisha na vitendo vya kihalifu, aliyekuwa Msaidizi wa Mkurugenzi wa Taifa wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Ludovick Joseph alisema ni kweli kundi hilo lipo na lilihusika na matukio mengi ya utekaji, utesaji na kushambulia watu. &nbsp;<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cSitakwenda kwenye details za hayo lakini ninachotaka tu kusema ni kwamba daktari yuko sahihi na <em>actually, basically<\/em> daktari mambo mengi alikuwa anafichwa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cHayo anayotamba kwamba anajua,\u2026.anajua machache sana ambayo amepata <em>knowledge<\/em> lakini yeye binafsi alikuwa hahusishwi kwa sababu alikuwa anafahamika yupo <em>against, so operation<\/em> nyingi yeye hakujua.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cKwa hiyo tungesema tunakwenda kwenye <em>details,<\/em> labda tungepata mengi na ya ndani zaidi. Kwa hiyo kujibu swali lako kwa ufupi, alichosema kiko sahihi na kwamba yeye mengi hayajui bado.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cKuhusu matukio hayo kwamba yalikuwepo ni <em>obvious<\/em> yalikuwepo na mwenyekiti alikuwa anajua. Sitaki kwenda kwenye <em>details<\/em> lakini unachoweza kunikunuu ni kwamba nimeongea na Ludovick amesema kwamba ana <em>knowledge<\/em> kwamba hayo matukio yalikuwepo na kwamba yeye mwenyewe alikuwa muhusika, walau alikuwa anajua. Hayo matukio mengi tu nayafahamu kwenye <em>details.<\/em><\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cNa anasema kwamba Dk. Slaa alikuwa hahusishwi kwa sababu walikuwa wanahofia kwamba yeye anapinga, Ludovick anasema kwamba Dk. Slaa anafahamu sehemu ndogo sana ya hayo matukio anayoyazungumzia, kwa leo nafungia hapo,\u201d alisema Ludovick.<\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"320\" height=\"213\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2023\/03\/ludovick.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-4154\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/03\/ludovick.jpg 320w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/03\/ludovick-300x200.jpg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/03\/ludovick-150x100.jpg 150w\" sizes=\"auto, (max-width: 320px) 100vw, 320px\" \/><figcaption class=\"wp-element-caption\">Aliyekuwa Mkurugenzi wa Taifa wa Ulinzi na Usalama Taifa wa Chadwema Wuilfred Lwakatare (aliyevaa nguo za kaki) akiwa na Ludovick Joseph ambaye alikuwa msaidizi wake.<\/figcaption><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Mwingine aliyezungumzia hilo na kukiri kufahamu kuwepo kwa kundi hilo ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha na pia Mhasibu wa Chadema Taifa, Samsoni Mwigamba aliyesema kundi hilo la kihalifu liliundwa mwaka 2010 na 2011.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cTukizungumzia hayo masuala, kwanza kamanda wa anga mwenyewe, mwamba, aliwahi kuniambia wakati fulani kwamba, tukiwa tuko Karatu tunashughulika na mgogoro wa uongozi. Aliwahi kuniambia kwamba hakuna namna unaweza kushinda nchi hii na kuingia madarakani bila kuwa na jeshi lako mwenyewe.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cKwa hiyo lazima tuimarishe <em>red brigade<\/em> ili tuhakikishe kwamba tuna mfumo wetu wa ulinzi na usalama nchi nzima. Na mimi nakumbuka miaka hiyo ya 2010, 2011 sisi tulipata ushauri wa kijana mmoja pale Arusha anaitwa (anamta jina). Huyu ni hawa watu wenye mafunzo ya ngumi na karate.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cYeye alitufuata mimi nikiwa Mwenyekiti wa Mkoa, akamfuata katibu wangu anaitwa Amani Bulugwa, akamwambia mnajua ni kwanini polisi walipowavamia pale kwenye uwanja. Unakumbuka kule kulikuwa na tukio la watu kuandamana na kulala uwanjani wakishinikiza Lema (Godbles) apewe dhamana atoke ndani.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cLema alikamatwa, akapelekwa mahakamani halafu mahakama ikasema dhamana iko wazi na watu wa kumdhamini wakajitokeza lakini yeye akakataa. Akasema mimi sitaki dhamana, nipelekeni huko ndani, wakampeleka ndani,\u201d alisema Mwagamba.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Akizungumzia zaidi tukio hilo, Mwigamba alisema Lema alipopelekwa gerezani na kuanza kupata suluba za huko aliomba adhaminiwe lakini hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi yake alikataa kwa sababu yeye mwenyewe alikataa kudhaminiwa awali.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cAlipofika kule, amekaa siku kadhaa akaanza kusota, akaomba dhamana, wakaja kuomba <em>remove order<\/em> kwa hakimu aliyekuwa na kesi yake ili jamaa apewe dhamana atoke. Hakimu akawaambia dhamana ilikuwa wazi siku hiyo na wadhamini walikuwepo tayari lakini mtuhumiwa alikataa akasema yeye anataka akae ndani, msinisumbue mwacheni akae ndani. Hakimu akakataa kutoa <em>remove order.<\/em><\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cBaada ya kukataa, sasa ndiyo ikabidi wa-<em>organize <\/em>maandamano mimi nikiwa Dar es Salaam makao makuu kama mhasibu wakati huo. Kwa hiyo, siku hiyo sikuwepo Arusha lakini mwenyekiti alikuwepo pamoja na Katibu Mkuu na baadhi ya viongozi wa mkoa na wilaya, wakaandaa maandamano wakaenda wakaishia pale uwanja wa NIC na wakaamua kulala uwanjani.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cSasa usiku ule polisi wakawa wamewazingira, nafikiri ilikuwa kama alfajiri saa 10 hivi kuelekea saa 11 wakati mwamba amechoropoka amemuacha Katibu Mkuu, alimwambia nakuja sasa hivi. Majira ya saa tisa hivi alimwambia kamanda natoka nakuja sasa hivi lakini hakurudi. Saa 10 kuelekea saa 11 alfajiri polisi wakawa wamewazingira, wakawatandika vibaya sana.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cYule kijana akamfuata katibu wangu akamwambia bwana hawa vijana wenu hawana mafunzo, hawa <em>red brigade<\/em> kwa sababu wangekuwa na mafunzo msingepigwa kama kuku namna ile. Ndiyo sisi tukamchukua tukawa tunampa hela akatufundishie sasa vijana wetu wa <em>red brigade,\u201d<\/em> alisema Mwigamba.<\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"591\" height=\"310\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2023\/03\/mwigamba.jpeg\" alt=\"\" class=\"wp-image-4155\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/03\/mwigamba.jpeg 591w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/03\/mwigamba-300x157.jpeg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/03\/mwigamba-150x79.jpeg 150w\" sizes=\"auto, (max-width: 591px) 100vw, 591px\" \/><figcaption class=\"wp-element-caption\">Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samsoni Mwigamba.<\/figcaption><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Alieleza zaidi kuwa kijana huyo alikuwa akitoa mafunzo kwa <em>red brigade<\/em> nyuma ya Ofisi ya Mkoa ya Chadema na kwamba mara ya kwanza kundi hilo likiwa na mafunzo lilitumika kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cAliwapa mafunzo sana, mazoezi sana pale kwenye ofisi ya mkoa kwa nyuma kulikuwa kuna banda, wakawa wanafanyia mazoezi hapo. Basi tukaenda kwa mara ya kwanza tumewatumia kwenye uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, wakati ule Nassari (Joshua) akiwa anagombea uchaguzi mdogo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cKwa hiyo tukawa tume &#8211; <em>organize<\/em> vijana tunawalipa hela, wana mafunzo, wakawa wanazunguka jimbo zima. Wakiona tu mahali CCM wamejikusanya katika mazingira ambayo wao wanahisi kuwa wanatoa rushwa wanawavamia, wanawatandika.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cBasi baada ya kushinda ule uchaguzi, ndiyo mwenyekiti akapenda sana ule mkakati na ndiyo akaniambia hayo maneno kuwa hutuwezi kuingia madarakani bila kuwa na jeshi letu la ulinzi na usalama. Kwa hiyo lazima tuwe na watu wetu na ndiyo wakamchukua yule kijana kutoka Arusha. Akawa ndiye mratibu wa Red Brigade Taifa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cNa alikuwa anazunguka mkoa na wilaya kwa hiyo ikawa inatengenezwa <em>network<\/em> ya red brigade Taifa, mkoa, wilaya mpaka kwenye kata. Wakachukuliwa watu wengi sana ndiyo kilichoendelea,\u201d alisema Mwigamba.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Dk. Slaa amekaririwa hivi karibuni akieleza kuwa Chadema ilikuwa na kundi la watu waliokuwa wakijihusisha na vitendo vya kuteka na kushambulia watu na alimtaja aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Temeke kuwa mmoja wa watu waliotekwa na kushambuliwa vibaya na kundi hilo la kihalifu la Chadema kabla ya kwenda kutupwa eneo la Ununio.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Dk. Slaa ambaye alikuwa akieleza sababu za yeye kutotaka kuzungumzia shambulio la kupigwa risasi kwa Lissu kwa vile hana data kamili za tukio hilo, alisema; \u201cMimi sipendi kuzungumzia haya masuala ya Lissu kupigwa risasi kwa sababu sina data za kutosha. Lakini vile vile ndani ya Chadema sina uhakika kwa sababu, nikatoa <em>cases<\/em> labda ndiyo kitu ulichokitaka cha aina hiyo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cNikasema mimi nimeletewa taarifa ya mtu wangu aliyekamatwa, kwa maana kwamba ametekwa nyara na kwa maelezo kwamba ametekwa nyara na watu wa Usalama wa Taifa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cNa mimi asubuhi, kesho yake, bwana huyo anaitwa Joseph, alikuwa mwenyekiti wetu wa Wilaya ya Temeke, na hiyo kesi baadaye nafikiri ilifika polisi sijui baadaye iliishia wapi.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cHuyu bwana ametekwa nyumbani kwake saa sita usiku, mimi najua ametekwa na usalama wa Taifa na nilikuwa na kesi nyingi za Usalama wa Taifa kweli kutekwa watu wangu.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cSaa sita asubuhi nikaitisha press conference, nikaisema sana Usalama wa Taifa na Serikali. Saa nane mchana huyu mtu amepatikana ametupwa maeneo ya Ununio, ameumia sana usoni.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cLakini mwezi mmoja baadaye, kijana wangu, ofisa wa red brigade anakuja kwangu ananiambia Dk. Slaa mimi ndiye niliongoza kikosi kilichoenda kumteka nyara na tumempiga tukamtupa Ununio.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cNikauliza kwanini mnakuja kwangu kwa sababu mimi Katibu Mkuu nilikuwa sikupewa taarifa, nikaambiwa wako viongozi wanaojua. Ukiambiwa hivyo unaendelea?<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cSasa vitu vya namna hiyo ni kweli vilikuwepo na mimi nilikuwa nimevichukia na nimesema hii siku nyingi siyo kitu kipya. Ndiyo maana lilipokuja suala la Lissu nikasema ndani ya Chadema tujitazame, tuko salama, tusinyooshe vidole kwa watu kabla sisi wenyewe hatujatizama.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cHuyo kijana ni wa kwetu, mwenyekiti wa chama wa wilaya, ametupwa na bahati nzuri nafikiri sijui upepo umepiga maana waliomtupa walisema walifikiri amekufa na wakamuacha <em>beach<\/em> na leo tunasema kuna watu wanaokotwa <em>beach<\/em> kumbe na sisi tupo. Sijui unanielewa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cUkiwa kiongozi, lazima uwe kiongozi wa kweli, unayesema ukweli na usimamie ukweli hata kama watu wako wamefanya vitu hivyo,\u201d alisema Dk Slaa.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>RIPOTA PANORAMA CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kina genge la kihalifu kinalolitumia kuteka, kutesa, kushambulia watu na kuwamwangia tindikali. Tanzania PANORAMA Blog imeelezwa. Tuhuma hizi zimeanikwa na baadhi ya waliokuwa viongozi waandamizi wa Chadema ikiwa ni siku chache tu baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa kukaririwa na chombo kimoja cha [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":4153,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[],"class_list":["post-4152","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-habari-kitaifa"],"amp_enabled":true,"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/03\/lissu.jpg","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/4152","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=4152"}],"version-history":[{"count":2,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/4152\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":4158,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/4152\/revisions\/4158"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/4153"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=4152"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=4152"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=4152"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=4152"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}