{"id":4144,"date":"2023-03-15T19:28:24","date_gmt":"2023-03-15T19:28:24","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/?p=4144"},"modified":"2023-03-15T19:28:32","modified_gmt":"2023-03-15T19:28:32","slug":"majaliwa-azindua-mifumo-ya-kibiashara-ya-jiba","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=4144","title":{"rendered":"<strong>MAJALIWA AZINDUA MIFUMO YA KIBIASHARA YA JIBA<\/strong>"},"content":{"rendered":"\n<p class=\"wp-block-paragraph\">RIPOTA WA WAZIRI MKUU<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amezindua programu ya kompyuta, maarufu kama JIBA App iliyotengenezwa na taasisi ya kibiashara ya Jaffery International Business Association&nbsp;(JIBA) Tawi la Tanzania.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">&nbsp;Programu hiyo ambayo&nbsp;lengo lake kuu ni kutengeneza fursa za biashara&nbsp;itawezesha upatikanaji wa taarifa juu ya fursa za uwekezaji za ndani na nje ya nchi na hivyo kurahisisha mawasiliano miongoni mwa wanachama wa JIBA ambao ni wafanyabiashara wakubwa na wadogo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">&nbsp;Akizungumza na washiriki kwenye hafla ya uzinduzi iliyofanyika Machi 12 mwaka huu, kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam, Majaliwa alisema programu hiyo inatarajiwa kupunguza usumbufu na kuongeza ufanisi wa kufanya biashara.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">&nbsp;\u201cProgramu hii inatarajiwa kupunguza usumbufu, kuongeza uwajibikaji na uaminifu kwenye sekta na mifumo ya biashara. Pia, itasaidia kupanua wigo wa soko la dunia kwa kuruhusu na kurahisisha biashara kufanyika mkononi kutoka mahali popote ulipo,\u201d alisema.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">&nbsp;Majaliwa pia alizindua mfumo wa&nbsp;<em>JIBA Sandbox&nbsp;<\/em>ambao unalenga kuwawezesha wadau kupata mafunzo na elimu ya jinsi ya kufanya biashara kwa ufasaha na kujikuza kwenye biashara na soko ulimwenguni.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Piaalizinduamaktaba mtandao (JIBA Investment Desk) ambayo itashughulika na utoaji wa taarifa za mifano ya biashara kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ufugaji wa samaki, kilimo kwa kutumia mfumo wa kisasa wa akili bandia (artificial intelligence).<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">&nbsp;Ili kuhakikisha&nbsp;programu hizo zinakuwa endelevu na zinatoa matunda yaliyokusudiwa, Majaliwa aliitaka timu ya uongozi wa JIBA na wanachama wake waiunge mkono Serikali kuongeza wigo wa utoaji elimu ya fedha kwa vijana na kuwawezesha kutumia vizuri mitaji wanayoipata kwa ajili ya biashara.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">&nbsp;\u201cVile vile wawezesheni kutumia vema fursa mbalimbali za kiuchumi zinazojitokeza kwenye maeneo yao. Tengenezeni nafasi kwa vijana kupata fursa ya mafunzo ya uzoefu wa kazi kwenye kwenye taasisi na biashara zenu na hivyo kuwasaidia kujiajiri au kuwapatia ajira,\u201d alisema.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">&nbsp;Aliwataka washirikiane na Serikali kuibua vipaji kwenye eneo la sayansi na teknolojia, kuwaendeleza na kuwatumia wabunifu wa Kitanzania kama wanavyofanya kwa JIBA App.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cTungejisikia fahari kuona programu kama hizi ambazo tumezindua leo zinabuniwa na kujengwa na vijana wetu,\u201d alisema.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">&nbsp;Akielezea hatua zinazochukuliwa na Serikali kuimarisha mazingira ya uwekezaji na biashara, Majaliwa alisema Serikali kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), imefanya maboresho makubwa ikiwemo kupunguza baadhi ya vigezo ambavyo vilikuwa ni kikwazo kwa Watanzania wenye nia ya kuwekeza nchini hususan kupata Cheti cha Vivutio vya Biashara (Certificate of Incentives).<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">&nbsp;\u201cKabla ya maboresho hayo, iliwalazimu Watanzania wawe na miradi yenye thamani isiyopungua dola za Marekani 100,000, yaani shilingi milioni 235 ili wafuzu kupata Cheti cha Vivutio. Hata hivyo, kuanzia mwaka jana, Serikali imefanya mapitio na kiwango hicho kimepunguzwa kwa asilimia 50. Hivi sasa, mradi wa Dola za Marekani 50,000 sawa na Shilingi milioni 117,500 unafuzu kupata Cheti cha Vivutio cha TIC.\u201d<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u00a0Alisema Serikali itaendelea kufanya maboresho ya kitaasisi, kisera na kisheria kwa lengo la kuimarisha shughuli za uwekezaji na biashara nchini. \u201cTumieni fursa hiyo kuibua changamoto za kisheria, kikodi na nyinginezo na kuwasilisha kwa Serikali kwa ajili ya hatua za maboresho na utatuzi,\u201d alisisitiza.<\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"700\" height=\"400\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2023\/03\/BIN-ZUBEIRY.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-4146\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/03\/BIN-ZUBEIRY.jpg 700w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/03\/BIN-ZUBEIRY-300x171.jpg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/03\/BIN-ZUBEIRY-150x86.jpg 150w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/03\/BIN-ZUBEIRY-600x343.jpg 600w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/03\/BIN-ZUBEIRY-696x398.jpg 696w\" sizes=\"auto, (max-width: 700px) 100vw, 700px\" \/><figcaption class=\"wp-element-caption\">Mufti na Sheikh Mkuu, Abubakar bin Zubeir<\/figcaption><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">&nbsp;Mapema,&nbsp;Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dk. Abubakar&nbsp;bin Zubeir Mbwana alisema suala la biashara kuwa uti wa mgongo wa maisha ya mwanadamu linasisitizwa sana kwenye Quran tukufu.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cSehemu tisa katika mafungu 10 ya riziki yako katika biashara na ukulima na moja ya kumi iliyobaki iko katika ufugaji. Sura nyingine inasema Mwenyezi Mungu anapenda kumuona mja wake anasumbuka kutafuta riziki ya halali,\u201d alisema.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">&nbsp;Alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wafanyabiashara wakubwa wajihadhari na suala la ushoga ambalo hivi sasa limeenea duniani ili kuepuka ghadhabu ya Mwenyezi Mungu.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cNinyi ni wafanyabiashara wakubwa, mliangalie suala hili sababu Mwenyezi Mungu anachukizwa, mkiacha liendelee tunaweza kupata balaa huko mbeleni. Kama zamani waliangamizwa kwa kosa hilo hilo, haiwezekani na sisi tusiangamizwe na Mwenyezi Mungu kama tutaliruhusu,\u201d alisisitiza.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">&nbsp;NayeMwenyekiti wa JIBA Tanzania, Al Junaid Hasham alisema taasisi hiyo iliyosajiliwa Uingereza ina matawi 32 duniani kote na lengo lake kuu ni kukuza fursa za kibiashara kwa wanajamii wa Khoja na wanachama washiriki (associate members).<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">&nbsp;Alisema wanatarajia kuanzisha jukwaa la kibiashara kupitia programu za JIBA App na&nbsp;<em>JIBA Investment Desk&nbsp;<\/em>na kwamba wanataka kuifanya Tanzania iwe kitovu cha wafanyabiashara ulimwenguni kote.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>RIPOTA WA WAZIRI MKUU WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amezindua programu ya kompyuta, maarufu kama JIBA App iliyotengenezwa na taasisi ya kibiashara ya Jaffery International Business Association&nbsp;(JIBA) Tawi la Tanzania. &nbsp;Programu hiyo ambayo&nbsp;lengo lake kuu ni kutengeneza fursa za biashara&nbsp;itawezesha upatikanaji wa taarifa juu ya fursa za uwekezaji za ndani na nje ya nchi na hivyo [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":4145,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[],"class_list":["post-4144","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-habari-kitaifa"],"amp_enabled":true,"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/03\/PM-JIBA.jpg","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/4144","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=4144"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/4144\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":4147,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/4144\/revisions\/4147"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/4145"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=4144"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=4144"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=4144"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=4144"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}