{"id":408,"date":"2022-02-10T04:19:00","date_gmt":"2022-02-10T04:19:00","guid":{"rendered":"https:\/\/msangirstz8.wordpress.com\/2022\/02\/10\/jinsi-fedha-za-benki-ya-dunia-zilivyopigwa\/"},"modified":"2022-02-10T04:19:00","modified_gmt":"2022-02-10T04:19:00","slug":"jinsi-fedha-za-benki-ya-dunia-zilivyopigwa","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=408","title":{"rendered":"JINSI FEDHA ZA BENKI YA DUNIA \u2018ZILIVYOPIGWA\u2019"},"content":{"rendered":"<p>\u00a0<\/p>\n<table align=\"center\" cellpadding=\"0\" cellspacing=\"0\" class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/blogger.googleusercontent.com\/img\/a\/AVvXsEhJ1dNwnMiRK5U5gCFvZ19_tQD-af_m6Ylz5DzqmcAJSqpWIsPZleufR_lNdR1NFmPP77w6mvhOpUgnv9E1v4MRIsUoPGbVRRdhN0PDDfQ6yGaduXgA-lfqk2olgjkBCLxkGIwpT50z5ZPWO9cjlz9qFuJmGyJlfy5mFz2Sbv-8SUH7v_36TD-r2wb2dg=s1280\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"506\" src=\"https:\/\/blogger.googleusercontent.com\/img\/a\/AVvXsEhJ1dNwnMiRK5U5gCFvZ19_tQD-af_m6Ylz5DzqmcAJSqpWIsPZleufR_lNdR1NFmPP77w6mvhOpUgnv9E1v4MRIsUoPGbVRRdhN0PDDfQ6yGaduXgA-lfqk2olgjkBCLxkGIwpT50z5ZPWO9cjlz9qFuJmGyJlfy5mFz2Sbv-8SUH7v_36TD-r2wb2dg=w288-h506\" width=\"288\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align:center;\">Charles Werongo<\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<p><!--[if gte mso 9]&gt;   Normal  0          false  false  false    EN-US  X-NONE  X-NONE                                       MicrosoftInternetExplorer4                                     &lt;![endif]--><!--[if gte mso 9]&gt;                                                                                                                                                                                                                                                                                    &lt;![endif]--><!--[if gte mso 10]&gt; \/* Style Definitions *\/  table.MsoNormalTable \t{mso-style-name:\"Table Normal\"; \tmso-tstyle-rowband-size:0; \tmso-tstyle-colband-size:0; \tmso-style-noshow:yes; \tmso-style-priority:99; \tmso-style-qformat:yes; \tmso-style-parent:\"\"; \tmso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt; \tmso-para-margin-top:0in; \tmso-para-margin-right:0in; \tmso-para-margin-bottom:10.0pt; \tmso-para-margin-left:0in; \tline-height:115%; \tmso-pagination:widow-orphan; \tfont-size:11.0pt; \tfont-family:\"Calibri\",\"sans-serif\"; \tmso-ascii-font-family:Calibri; \tmso-ascii-theme-font:minor-latin; \tmso-fareast-font-family:\"Times New Roman\"; \tmso-fareast-theme-font:minor-fareast; \tmso-hansi-font-family:Calibri; \tmso-hansi-theme-font:minor-latin; \tmso-bidi-font-family:\"Times New Roman\"; \tmso-bidi-theme-font:minor-bidi;} &lt;![endif]--> <\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>RIPOTA PANORAMA<\/span><\/span> <\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>0711 46 49 84<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>MIRADI mingi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na umeme iliyotekelezwa kwa awamu mbili na wakarandasi wa ndani kwa fedha zilizotolewa kwa mkopo na Benki ya Dunia, tayari \u2018imekwishaoza.\u2019<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Miradi hiyo ya mabilioni ya fedha ilitekelezwa mwaka 2006 na 2010 ikihusisha ujenzi wa barabara katika Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na ujenzi wa miundombinu ya umeme ikiwa ni kusikimika nguzo, kutandaza nyaya za umeme na kufunga taa za barabarani.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Hayo yameelezwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Construction Co. Ltd, Charles Werongo katika mahojiano na Tanzania PANORAMA Blog yaliyofanyika ofisini kwake Mabibo, Dar es Salaam.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Werongo alikuwa akijibu na kutoa ufafanuzi wa jinsi kampuni yake ilivyotekeleza miradi mbalimbali iliyopewa na Serikali kwa gharama za fedha za Benki ya Dunia baada ya kudaiwa kuwa ni moja ya wakandarasi waliotafuna bila huruma fedha hizo.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Katika utekelezaji wa miradi hiyo, inadaiwa baadhi ya wakarandasi walijenga barabara na miundombinu ya umeme chini ya kiwango na katika baadhi ya maeneo walitumia vifaa visivyofaa vinavyopatikana kwa bei ya chini ambavyo pia ni hatarishi kiusalama.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Kwamba hayo yalifanywa makusudi na wakarandasi hao ili waweze kuweka kibindoni mabilioni ya fedha za mkopo za miradi hiyo; fedha ambazo sasa zinalipwa na Serikali. <span>\u00a0<\/span><\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Kampuni ya Werongo ya Mabibo Construction Co, Ltd, pamoja na mambo mengine inadaiwa kusimika miti ya mirunda kama nguzo za umeme katika baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Ilala. Maeneo hayo ni Buguruni kwa Binti Madenge hadi Buguruni Malapa.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Maeneo mengine ambayo kampuni hiyo inadaiwa kusimika nguzo za miti ya mirunda kwa ajili ya kushikilia nyaya za umeme yapo Wilaya ya Temeke eneo la Tandika katika vitongoji vya Keko Toroli, Tambuka Reli, Mashine ya Maji, Mtoni Unguja na kwingineko.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Awali Tanzania PANORAMA Blog ilifanya mahojiano na mmoja wa mafundi waliohusika kusimika nguzo za miti ya mirunda ambaye alikiri hilo kwa kueleza kuwa yeye aliitwa kwenda kufanya kazi ya kusimika nguzo na kukuta ni za miti ya mirunda lakini baada ya kusimika, Mhandisi Mshauri aliyekuwa akisimamia ujenzi huo kwa Wilaya ya Temeke alibaini kasoro hiyo na kuiamuru Mabibo Constuction Co, Ltd kuiondoa mara moja kwa sababu ingesababisha maafa makubwa.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span><\/p>\n<table align=\"center\" cellpadding=\"0\" cellspacing=\"0\" class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/blogger.googleusercontent.com\/img\/a\/AVvXsEiCUTiKeBvQ3nT1D3NlArnXnk6lh9yj_Qi5VF8cZffE48eXJUamM6j9In5GfKHwFRYTkZt_BCyW6TwU4mRlu49nS7p4FLDPg1taBoDQ9ffqN8gRUH8e3IQvWhb1gecr6S69erbZZI_5qV-VdCGvht5M30qLcTypdOT3GURzsy42Rp3R2x-R2E_LnvbMzw=s259\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"640\" src=\"https:\/\/blogger.googleusercontent.com\/img\/a\/AVvXsEiCUTiKeBvQ3nT1D3NlArnXnk6lh9yj_Qi5VF8cZffE48eXJUamM6j9In5GfKHwFRYTkZt_BCyW6TwU4mRlu49nS7p4FLDPg1taBoDQ9ffqN8gRUH8e3IQvWhb1gecr6S69erbZZI_5qV-VdCGvht5M30qLcTypdOT3GURzsy42Rp3R2x-R2E_LnvbMzw=w479-h640\" width=\"479\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align:center;\">Mirunda<\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<p>\u00a0<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cYeye kwenye huo mradi alitakiwa kuweka \u2018sub contractor\u2019 lakini badala yake alituita baadhi ya mafundi tunaojua kazi za umeme kwenda kufanya kazi hiyo na mimi nikiwemo. Hiyo mirunda mimi niliikuta na tuliambiwa tusimike hiyo.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cSasa huwezi kumuhoji bosi wako akishatoa amri, tulisimika tukafunga nyaya za umeme na tukaweka taa Buguruni hiyo kuanzia kwa Binti Madenge hadi Buruguni Malapa.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cHiyo ni kwa Wilaya ya Ilala na kwa Wilaya ya Temeke tulifunga Tandika kuanzia Keko Toroli, Tambuka Reli, Mashine ya Maji, Mtoni Unguja na kwingineko.<span>\u00a0 <\/span><\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cSasa yule Mhandisi Mshauri wa Wilaya ya Temeke hakutaka ubabaishaji alipofika tu akafoka na akaamuru mirunda yote iondolewe ziwekwe nguzo za ukweli, ikabidi mimi ndiyo nitumwe sasa kwenda kutafuta nguzo halisi maana Werongo hajui chochote kuhusu umeme na kampuni yake ni ya ujenzi wa barabara siyo umeme.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cNikaenda kununua nguzo za ukweli Mbezi Makonde kuna jamaa namfahamu anauza pale, tukaja tukafunga na hizo ndiyo zipo mpaka leo.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cLakini kwa upande wa Buruguni kote tulikofanya, sijui jamaa alicheza vipi na hao watu wa manispaa na Mhandisi Mshauri hawakuhoji chochote na hazichukua muda kwa sababu mirunda inaliwa sana na mchwa, miezi minne zikawa zimeanguka zote na mpaka leo hakuna umeme kote huko.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cJamaa akakunja mabilioni yake akatia mfukoni, sisi alitulipa hela yetu ya ufundi hayo mengine muulizeni yeye,\u201d alisema fundi huyo ambaye jina lake tumelifadhi.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Akijibu hayo yote, Werongo kwanza alikanusha kata kata kampuni yake kupewa zabuni ya kujenga miundombinu ya umeme mahali popote tangu alipoianzisha.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cHata siku moja siyo kweli, sisi, kampuni yangu hatujawahi kupata tenda yoyote ile ya kujenga miundombinu ya umeme. Tangu kampuni hii ianzishwe inahusiana na ujenzi wa barabara, mitalo na nyumba lakini mambo ya umeme, hilo halipo,\u201d alikanusha Werongo.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Alipoelezwa kuwa Tanzania PANORAMA Blog imefika katika eneo la miradi mbalimbali aliyoitekeleza katika Wilaya za Ilala na Temeke na kukuta yote imeoza na kumbukumbu zilizopo kwenye manispaa hizo zinaonyesha kuwa kampuni yake ndiyo iliyokuwa na kandarasi ya kujenga miundombinu hiyo kwenye baadhi ya vitongoji vya Buguruni ambako sasa hakuna nguzo hata moja; alibadili kauli, alisema.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cJamani, mimi ni mwafrika, ni mweusi. Iko hivi, 2006 na 2010 ndiyo tulitekeleza huo mradi, tulipata zabuni ya kujenga barabara na kuweka taa. Ni kweli kama mmefika hayo maeneo kwa sasa taa hazipo, hatujui zipo wapi, sisi tulimaliza jukumu letu tukakabidhi.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cBarabara pia zilishaharibika ni muda mrefu sana tangu tuzijenge, taa za barabarani tulizofunga zilishatolewa lakini hilo siyo jukumu letu ni jukumu la wale tuliowakabidhi baada ya sisi kumaliza kazi,\u201d alisema Werongo.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span><\/p>\n<table align=\"center\" cellpadding=\"0\" cellspacing=\"0\" class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/blogger.googleusercontent.com\/img\/a\/AVvXsEhhM4EBkpzC1DqV9iyAyUGMa9FpRbkadw1tnxCeKa__nCRD1dsQdLvVnp9vO7TI8i_3Hg_HaJu0cKAdZVqC5sF4Eq-P4pukzZbHO7YIbv9hcyd0pL2XUZHaBrusfNDwKj7yYjIoFPSrCv8wHghmpo7AdAuRK_Q136FWtAjkYXWRm9bvaOM9Uu6olhbLQQ=s595\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"422\" src=\"https:\/\/blogger.googleusercontent.com\/img\/a\/AVvXsEhhM4EBkpzC1DqV9iyAyUGMa9FpRbkadw1tnxCeKa__nCRD1dsQdLvVnp9vO7TI8i_3Hg_HaJu0cKAdZVqC5sF4Eq-P4pukzZbHO7YIbv9hcyd0pL2XUZHaBrusfNDwKj7yYjIoFPSrCv8wHghmpo7AdAuRK_Q136FWtAjkYXWRm9bvaOM9Uu6olhbLQQ=w640-h422\" width=\"640\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align:center;\">Nguzo halisi za umeme<\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<p>\u00a0<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Alipoulizwa barabara alizozijenga zilipaswa kudumu kwa muda gani kwa makadirio ya chini alisema hilo halikuwemo kwenye mkataba wake bali kilichokuwa ndani ya mkataba huo ni \u2018guarantee\u2019 ya muda usiozidi mwaka mmoja.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cHayo mambo mimi hayakuwa kwenye mkataba wangu, mkataba wangu ulikuwa na \u2018guarantee\u2019 ya barabara hizo na ni miezi sita nadhani au mwaka mmoja, basi,\u201d alisema.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Akijibu kuhusu kusimika nguzo za miti ya mirunda kama nguzo za umeme alisema siyo kweli bali alifunga nguzo ambazo hazina viwango zilizokataliwa na Mshauri Elekezi wa Wilaya ya Temeke aliyemtaka kuzibadilisha, jambo ambalo alilitekeleza lakini kwa upande wa maeneo ya Ilala hakukuwa na tatizo.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Kwa maneno yake mwenyewe; alisema, \u201cNguzo za kawaida ndiyo tulisimika na tulifunga taa, siyo mirunda. Hizo zilikuwa nguzo za umeme. Sasa tuliweka hizo nguzo zikakataliwa na mshauri kuwa hazikuwa na ubora na zile ni kabla mradi hatujakabidhi, zikakataliwa kwamba hazina ubora.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cTukabadilisha, aliyekuwa anasimamamia huo mradi ni huyo huyo mmoja kwa Wilaya ya Temeke na Ilala, ndiye aliyekataa kwa upande wa Temeke akataka zibadilishwe.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cLakini huku upande mwingine wa Buguruni hakukuwa na shida, hakukataa na tunachojua sisi tulipata shida kwenye mradi wa kule Tandika kwamba nguzo hazina ubora na tukabadilisha.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cMimi niwaambie sasa, msipende mambo ya kusikia sikia, huo mradi wa umeme kwanini umefeli, naweza kuwaambia mimi lakini suala la kwamba hazina ubora lilikuwa Tandika tukabadilisha nguzo lakini siyo Buguruni. <\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cNa Mshauri Elekezi alikubali kwa upande wa Buguruni kwa sababu ule mradi ulikuwa na Mshauri Elekezi wa umeme ambaye alikuwa anacheki kuanzia waya mpaka nguzo.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cHuo mradi umefeli pote, hata ukiambiwa kulikuwa na \u2018street light,\u2019 hii Manzese utakubali? mahakama ya ndizi mpaka midizini kulikuwa na taa za barabarani lakini sasa hazipo, Mbona sasa hata huku Manzese kuliwa na taa lakini sasa hazipo? we fuatilia. Ule ulikuwa mradi wa Benki ya Dunia ambao ulikuwa mpaka huku Manzese lakini sasa hamna kitu hata huku Manzese, hamna.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cMimi kwenye mkataba wangu kuna \u2018parkage ya street lights,\u2019 mkataba wangu wa ujenzi wa barabara ulikuwa na \u2018parkage ya steet lights\u2019 kwa hiyo mimi kazi yangu ni kumtafuta \u2018sub contractor.\u2019 Lakini simkumbi kwa sababu tunazungumza mambo ya miaka ya 2006.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cNa mnapaswa mjue kuwa kuna sehemu tatu ambazo mnatakiwa muende, hapo kwanza kuna mwenye mradi wake ambao ni manispaa anaweza kuelezea pande zote kwa sababu na wao walikuwa na mshauri wa mradi wa umeme na wa kusimamia hizo barabara, halafu mimi mkandarasi na kulikuwa na Mshauri Elekezi wa Benki ya Dunia.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cMimi nafanya kazi yangu, nikimaliza inakaguliwa lakini mtu asikudanganye kuwa eti ule mradi wa umeme umefeli kwa sababu nguzo zilikuwa mbovu.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cUle mradi umefeli kwa sababu kwanza hawakuwa na hela ya kununua umeme kwa ajili ya mtaani hao Manispaa ya Ilala. Umeme wa kutumia, ule umeme haukuwa wa \u2018solar\u2019 ulikuwa wa Tanesco. Waliweka weka mwanzoni wakashindwa, mtaani wakawa wanachangishana wakashindwa.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cSasa kushindwa kwao, wakati ule ndiyo kulikuwa na shida ya waya za umeme. Kwa hiyo waya zikawa zinaibiwa, waya kuibiwa nguzo nazo zikawa zinaibiwa na msishangae kama kuna vishoka na watu wanaruhusiwa kununua nguzo zao hiyo siyo ajabu.\u201d<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span><\/p>\n<table align=\"center\" cellpadding=\"0\" cellspacing=\"0\" class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/blogger.googleusercontent.com\/img\/a\/AVvXsEg5MdExrY85mG11E4NH6G32QxBajbQoV1SkbYNgDNLeb90QSLjwERvN3porut6QMHR5HG9AfQxQW56qoelxYkzIC6Og9E0mKCa7aB86e9AVIskf2Ydc9TojIgXKtLteFLajCBIEvbf_7QbDQfzgzIcKsyMLUoqRurRAF_naWfuqvRs4C7HBs2-85_dgFQ=s259\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"479\" src=\"https:\/\/blogger.googleusercontent.com\/img\/a\/AVvXsEg5MdExrY85mG11E4NH6G32QxBajbQoV1SkbYNgDNLeb90QSLjwERvN3porut6QMHR5HG9AfQxQW56qoelxYkzIC6Og9E0mKCa7aB86e9AVIskf2Ydc9TojIgXKtLteFLajCBIEvbf_7QbDQfzgzIcKsyMLUoqRurRAF_naWfuqvRs4C7HBs2-85_dgFQ=w640-h479\" width=\"640\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align:center;\">Nyaya za umeme (Picha kwa hisani ya mtandao)<\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<p>\u00a0<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Kuhusu mkandarasi mdogo aliyempa ukandarasi wa kujenga miundombinu ya umeme; alisema \u201csisi tuliwapa mafundi siyo kampuni . Mimi ninachosema ni hivi nilipewa kufanya kazi nikaifanya, ikakaguliwa ikaonekana ina ubora isipokuwa na ubora nikarekebisha, nikafanya kipindi changu kile cha maangalizo nikamaliza, \u2018that my end,\u201d alisema.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Tanzania PANORAMA ilipomuuliza Weronga mahali aliponunua nguzo zilizokataliwa na Mshauri Elekezi wa Wilaya ya Temeke, ghafla alibadilika na kuanza kung\u2019aka, alisema, \u201cNguzo zilizokataliwa niliponunua \u2018is not your issue\u2019 kwa sababu nguzo zilizoharibika ulinunua wapi haikuhusu. <\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cUmeleta nguzo imethibitishwa kuwa hii ndiyo ina ubora, kwa sababu kuna mtu ambaye ni \u2018consultant,\u2019 yule ni \u2018specialist\u2019 wa umeme wa mradi mzima wa \u2018world bank.\u2019 Umeleta kitu ambacho sicho amekukatalia lakini umeleta kitu kingine amesema hiki ndicho sahihi sasa shida ni nini?<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cNi kweli baadhi ya nguzo nilinunua Makonde, yule jamaa ni \u2018supplier\u2019 mkubwa, ni mtu wa dini sana, ana maduka yake pale Mwenge. Ataendaje kununua fundi wakati mwenye jukumu ni mimi?<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cWatu wa \u2018world bank\u2019 walikuwepo kuangalia, ndiyo wanaotoa hela, hii kazi ilikuwa ya \u2018world bank\u2019 watu wa manispaa walikuwepo,<span>\u00a0 <\/span>watu wa jiji walikuwapo, sasa sidhani kama hapo unaweza kufanya kitu cha ajabu. Mimi ndiyo najua kwanini huo mradi ulifeli.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cMimi ninapoweka fundi akija mkaguzi na msimamizi wa mradi akisema \u2018ok, issue\u2019 ni nini? Mimi nilifanya kazi nzuri na kazi yangu ikakamilika, mimi nimemaliza.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cNguzo nilinunua wapi inakuhusu nini, wewe shati lako umenunua wapi?\u201d aliuliza kwa ukali Weronga na Tanzania PANORAMA ilimjibu Kariakoo.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Akiwa bado amekunja ndita aliuliza bei lililonuliwa na kujibiwa sh. 17,000 mashati sita katika maduka ya wachina, kisha alitaka kuonyeshwa risiti na kujibiwa ipo imetunzwa mahali salama nyumbani. Hapo alishusha pumzi kwa nguvu huku akieleza mshangao kwa mtu mzima kutunza risiti ya sh.17,000 aliyonunulia mashati kwa wachina kisha aliendelea kueleza kuwa;<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u201cKama kuna watu, hao mafundi wamewaambia kuwa hizo nguzo hazipo ni kweli zilikaa miezi mitatu au minne hivi nadhani zikaanza kuharibika, zikaanguka lakini siyo eneo hilo tu, miradi yote ya Benki ya Dunia imefeli,\u201d alisema kisha akakataa kuulizwa swali jingine lolote kwa kile alichodai amekwishasigana na Tanzania PANORAMA Blog.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>Jitahada za kupata kauli ya uongozi wa Wilaya ya Ilala na ile ya Mshauri Elekezi wa mradi kuhusu sakata hili zinaendelea.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span><br \/><\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size:large;\"> <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span>\u00a0<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span>\u00a0<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span>\u00a0<\/span><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>\u00a0 Charles Werongo RIPOTA PANORAMA 0711 46 49 84 MIRADI mingi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na umeme iliyotekelezwa kwa awamu mbili na wakarandasi wa ndani kwa fedha zilizotolewa kwa mkopo na Benki ya Dunia, tayari \u2018imekwishaoza.\u2019 Miradi hiyo ya mabilioni ya fedha ilitekelezwa mwaka 2006 na 2010 ikihusisha ujenzi wa barabara katika Wilaya [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":false,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[1],"tags":[34],"coauthors":[],"class_list":{"0":"post-408","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","6":"category-uncategorized","7":"tag-habari"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/408","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=408"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/408\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=408"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=408"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=408"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=408"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}