{"id":4037,"date":"2023-02-16T12:16:54","date_gmt":"2023-02-16T12:16:54","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/?p=4037"},"modified":"2023-02-16T12:28:38","modified_gmt":"2023-02-16T12:28:38","slug":"padre-ampiga-risasi-mtoto-wa-miaka-tisa-polisi-wafunika-kombe","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=4037","title":{"rendered":"PADRE AMPIGA RISASI MTOTO WA MIAKA TISA, &#8216;POLISI WAFUNIKA KOMBE&#8217;"},"content":{"rendered":"\n<p class=\"wp-block-paragraph\">RIPOTA PANORAMA<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">PADRE Evodius Msigwa wa Jimbo Katoliki la Bunda lililopo Mkoa wa Mara anadaiwa kumpiga risasi mbili kwenye paja mtoto mwenye umri wa miaka tisa aliyemtuhumu kumwimbia Sungura.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Taarifa zilizopatikana kutoka kwa ndugu wa karibu wa kijana huyo aliyetajwa kwa jina moja la Adam zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea mwaka 2021 katika Kijiji cha Manyamanyama, Wilaya ya Bunda mkoani Mara lakini limekuwa likifichwa na kwamba ingawa liliripotiwa polisi; Polisi walifunika kombe.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Inadaiwa, siku ya tukio Padre Msigwa alikuwa akikata miti katika eneo lililo karibu na Banda lake la Sungura ndipo alipomuona mtoto Adam aliyekuwa amebeba mkaa akielekea nyumbani kwao akipita mbele ya banda lake la sungura akamwita na kuanza kumtuhumu kwa kumwimbia sungura wake.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cLile banda la sungura wa Padre lipo karibu na njia ya kwenda kanisani, ni njiani, watu wote huwa tunapita pale. Tulipomuhoji mtoto alisema kuwa baada ya kufika usawa wa lile banda, yule Padre alikuwa anakata miti, alikuwa na panga mkononi, akaanza kumwita we kijana njoo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cAlipoenda akaanza kumuhoji ni kwanini huwa anamuibia sungura wake, kijana akasema yeye siyo mwizi bali mpita njia na anatoka kununua mkaa aliotumwa na wazazi wake anaupeleka nyumbani. Akamkamata mkono akamuongoza kwenye banda la sungura.<\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"472\" height=\"1024\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2023\/02\/bb85c58e-ebfa-47f2-9821-3cdb2aa672ec-472x1024.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-4040\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/02\/bb85c58e-ebfa-47f2-9821-3cdb2aa672ec-472x1024.jpg 472w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/02\/bb85c58e-ebfa-47f2-9821-3cdb2aa672ec-138x300.jpg 138w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/02\/bb85c58e-ebfa-47f2-9821-3cdb2aa672ec-150x325.jpg 150w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/02\/bb85c58e-ebfa-47f2-9821-3cdb2aa672ec-300x651.jpg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/02\/bb85c58e-ebfa-47f2-9821-3cdb2aa672ec-194x420.jpg 194w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/02\/bb85c58e-ebfa-47f2-9821-3cdb2aa672ec-387x840.jpg 387w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/02\/bb85c58e-ebfa-47f2-9821-3cdb2aa672ec.jpg 498w\" sizes=\"auto, (max-width: 472px) 100vw, 472px\" \/><figcaption class=\"wp-element-caption\">Makovu yaliyosababishwa na risasi yaliyo kwenye mguu wa Adam <\/figcaption><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cAdam baada ya kuona kuna hatari mbele yake akaanza purukushani za kujinasua kwenye mikono ya Padre ili akimbie lakini hakuweza, Padre akamwamuru alale chini kifudifundi, mtoto akalala, akiwa amelala pale chini akachomoa bastola akampiga risasi mbili mguuni kwenye paja,\u201d amedai mmoja wa ndugu wa mtoto huyo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Taarifa nyingine kutoka kwa watu wa karibu na familia ya mtoto Adamu zimedai kuwa Padre Msigwa baada ya kumpiga risasi Adam alieleza kuwa alimkuta akiiba sungura wake, akamtaka ajisalimishe au akimbie kutoka kwenye banda lake kwa kufyatua risasi juu lakini Adamu hakukimbia bali alisimama hapo hapo bandani.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cPadre anasema alimkamata mtoto akiwa anaiba, alimkamata na sungura wake, akawa amefyatua risasi ya kwanza juu ili mtoto ajisalimishe au akimbie. Mtoto hakukimbia wala nini, Padre Msigwa akaona inaweza kuleta shida zaidi labda mtoto ana silaha ndipo akaamua kumpiga risasi ya mguu ili amkamate, akafanikiwa kumkamata.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cPadre Msigwa aliamua kulimaliza jambo hilo kwa kuelewana na wazazi wake Adam kwa kugharamia matibabu baada ya Askari Polisi waliofika eneo la tukio kuwabembeleza wazazi hao wakubali kupokea fedha za matibabu jambo ambalo waliliafiki kwa kupokea fedha za matibabu na fidia nyingine.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cLakini kauli hiyo ya Padre Msigwa ilikanushwa vikali na wazazi wa Adamu, wao walieleza kuwa baada ya kufikishwa Kituo cha Polisi, alipelekwa hospitali akiwa chini ya ulinzi wa Polisi kwa ajili ya matatibu na alilazwa akiwa chini ya ulinzi wa Polisi.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cPolisi walimlinda Adamu kwa zamu, usiku na mchana kwa muda wa siku mbili akiwa anapatiwa matibabu kabla hawajatoweka na kumuacha akiendelea na matibabu kwa gharama na uangalizi wa wazazi wake, hivyo hata alipotoka polisi hawakujui ingawa wao ndiyo walimpeleka pale hospitali na wakawa wanamlinda kwa zile siku mbili.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cAdamu alipotoka hospitali nadhani hakuwa amepona vizuri kwa sababu mguu uliendelea kumsumbua akashindwa kuendelea na masoma, alikuwa anasoma darasa la pili huo mwaka 2021. Wazazi wake walishindwa kuchukua hatua dhidi ya Padre Msigwa kwa sababu ya kutishiwa maisha, hivi sasa Adamu yupo anatibiwa kwa mganga wa kienyeji,\u201d ameeleza mtoa taarifa huyo.<\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"300\" height=\"168\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2023\/02\/RPC-Mara.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-4041\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/02\/RPC-Mara.jpg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/02\/RPC-Mara-150x84.jpg 150w\" sizes=\"auto, (max-width: 300px) 100vw, 300px\" \/><figcaption class=\"wp-element-caption\">Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Longinus Tibashubwamu<\/figcaption><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Tanzania PANORAMA Blog imemtafuta Padre Msigwa kwa simu yake ya kiganjani na kumuuliza kuhusu kuhusika na tukio la kumpiga risasi Adamu lakini amekataa kutoa ushirikiano;<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Mahojiano ya Padre Msigwa na Tanzania PANORAMA Blog yalikuwa hivi;<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">PANORAMA, Padre habari za leo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">PADRE MSIGWA- Nzuri.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">PANORAMA \u2013 Naongea na Padre Msigwa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">PADRE MSIGWA \u2013 Ndiyo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">PANORAMA \u2013 Nafurahi kukupa Padre, mimi naitwa (mwandishi wa Tanzania PANORAMA anajitambulisha jina), ni mwandishi wa habari, naomba nisaidie jambo moja, naomba kusukia kutoka kwako, hivi tukio la wewe kumpiga risasi kijana mwenye umri wa miaka tisa lilitokeatokeaje Padre.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">PADRE MSIGWA \u2013 Wewe ni mwandishi wa wapi?<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">PANORAMA \u2013 Mwandishi wa Tanzania PANORAMA Blog.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">PADRE MSIGWA \u2013 Sasa kwenye simu siwezi kuongea.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">PANORAMA \u2013 Kwanini?<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">PADRE MSIGWA \u2013 Njoo hapa ofisini kwangu.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">PANORAMA \u2013 Ofisi zako zipo wapi.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">PADRE MSIGWA &#8211; Jimbo Katoliki la Bunda.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">PANORAMA \u2013 Mimi niko Dar es Salaam ndiyo maana. nimekupigia simu na kujitambulisha kwako.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">PADRE MSIGWA \u2013 Wewe, nimesema hatuwezi kuongea kwenye simu, tuma mtu basi.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><em>Akakata simu.<\/em><\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) wa Mara, Longinus Tibashubwamu alipoulizwa alisema ndiyo kwanza analisikia tukio hilo na kuahidi kufuatilia kabla ya kutoa taarifa.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>RIPOTA PANORAMA PADRE Evodius Msigwa wa Jimbo Katoliki la Bunda lililopo Mkoa wa Mara anadaiwa kumpiga risasi mbili kwenye paja mtoto mwenye umri wa miaka tisa aliyemtuhumu kumwimbia Sungura. Taarifa zilizopatikana kutoka kwa ndugu wa karibu wa kijana huyo aliyetajwa kwa jina moja la Adam zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea mwaka 2021 katika Kijiji cha [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":4038,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[],"class_list":["post-4037","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-habari-kitaifa"],"amp_enabled":true,"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2023\/02\/bastola.jpg","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/4037","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=4037"}],"version-history":[{"count":2,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/4037\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":4044,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/4037\/revisions\/4044"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/4038"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=4037"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=4037"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=4037"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=4037"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}