{"id":3697,"date":"2022-12-01T18:12:36","date_gmt":"2022-12-01T18:12:36","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/?p=3697"},"modified":"2022-12-01T18:15:56","modified_gmt":"2022-12-01T18:15:56","slug":"wema-sepetu-alivyojikabidhi-kwa-diamond","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=3697","title":{"rendered":"WEMA SEPETU ALIVYOJIKABIDHI KWA DIAMOND"},"content":{"rendered":"\n<p class=\"wp-block-paragraph\">HIVI NDIVYO NINAVYOMFAHAMU DIAMOND PLATINUMZ &#8211; 6<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">HAMEES SUBA<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><strong>ILIPOISHIA<\/strong><\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><em>Diamond na Vespa<\/em><\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">BAADA ya Diamond kuanza kuzishika noti, siku moja nikiwa naendesha gari katika barabara ya Tandale kuelekea Sinza, nikiwa maeneo ya Tanesco ghafla pikipiki aina ya Vespa<em> &#8216;iliniovateki&#8217;<\/em> kwa mwendo wa kasi sana hali iliyosababisha niitazame kwa jicho la hasira.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Haikwenda mbali sana ikapunguza mwendo na kukata upande wa kushoto kuelekea njia za uswahilini. Kwenye gari nilikuwa na marehemu Boni ndugu yake na Papaa Misifa, yule anayeonekana kwenye video ya <strong><em>nenda kamwambie<\/em><\/strong>. Alinisikia nikisonya kutokana na kutofurahishwa na kitendo cha mwendo kasi ya ile Vespa. Akanitazama na kucheka kisha akasema; &#8220;Unakasirika nini? haya yote umeyasbabisha mwenyewe.&#8221;<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Sikumuelewa alichomaanisha lakini kabla sijamuuliza chochote akaniongeza neno hili; \u201cmwanao huyo ndio anakufanyia vurugu barabarani.\u201d Alimaanisha kuwa aliyepita na ile Vespa kwa mwendo wa kasi alikuwa Diamond.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Sikuamini alichosema, nikamuuliza; \u201ckaanza lini kuendesha Vespa na mbona mwendo anaokwenda nao ni wa hatari Sana?&#8221; Akajibu, \u201cmambo ya ujana hayo, Vespa ni ya kwake kainunua.\u201d<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><strong>SASA TIRIRIKA NAYO&#8230;<\/strong><\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Ghadhabu iliyokuwa imenishika kutokana na ile<em> &#8216;ovateki&#8217;<\/em> ya Vespa ya Diamond niliyoishuhudia ilianza kupoa baada ya kusikia kwamba amenunua pikipiki. Nilicheka kidogo kisha nikamwambia Boni; \u201cMkionana mwambie dogo awe makini barabarani, vyombo vya moto havina uswahiba.\u201d Boni akasema; \u201csawa mkuu ujumbe utafika.\u201d<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Pale kwenye ile kona aliyoingia Diamond na Vespa ndipo nilipomuacha Boni kisha mimi nikaendelea na safari yangu kuelekea Sinza.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Baada ya miezi kadhaa mambo yaliendelea kuwa mazuri, nikiwa kwenye kambi ya Aljazeerah Entertainment, Sinza Palestina nikapata taarifa kuwa Diamond ameachana na usafiri wa Vespa na kununua gari aina ya Toyota Celica iliyokuwa ikimilikiwa na mtangazaji wa Televisheni, Ben Kinyaiya.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Ilikuwa gari kuu kuu lakini kimjini mjini ilitosha kusafishia nyota hasa kwa msanii aliyekuwa anachipukia. Gari hiyo ndiyo ile inayoonekana kwenye video ya Mbagala ambapo kuna sehemu ndugu yake na Diamond, Rommy Jones anaonekana akishusha mguu toka ndani ya gari hiyo akiwa amevaa viatu vyekundu.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Wakati maendeleo ya Diamondyakizidikusonga mbele, nikasikia amepata <em>show<\/em> ya kutoka nje ya Dar es Salaam. Nadhani ilikuwa ndiyo <em>show<\/em> yake ya kwanza kufanyika mkoani, ilikuwa <em>show<\/em> ya Morogoro ambapo kwa mujibu wa Aljazeera walilipwa shilingi laki tano.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Baada ya <em>show<\/em> hiyo Diamond akapata <em>show<\/em> nyingine ndani ya Jiji la Dar es Salaam katika kitongoji cha Mbagala. Inasemekana kuwa <em>show<\/em> hiyo Aljazeerah waliipata kupitia mgongo wa Dj Nelly aliyekuwa mfanyakazi wa Clouds FM.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Nimeitaja<em> show<\/em> hiyo kwa sababu haiwezi kufutika kwenye kumbukumbu za Aljazeereh Entertainment na Diamond mwenyewe kutokanaa na kilichojiri. Ilikuwa ni <em>show<\/em> ya maumivu makubwa sana kwani licha ya kwamba jina la Diamond lilishaanza kuingia masikioni mwa mashabiki wa muziki, lakini <em>show<\/em> hiyo haikupata watu kabisa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Yaani ukichukua idadi ya watu walioingia kwa kiingilio, walioingia kishkaji, Diamond na madensa wake<em>, \u2018kruu&#8217;<\/em> ya Aljazeerah, Dj Nelly na watu wake, wahusika wa ukumbi nk, hawakufika watu hamsini. Ilikuwa ni <em>show<\/em> ya hasara kweli kweli, lakini baada ya <em>show<\/em> Diamond alibaki akicheka na kusema: \u201c<em>dah imetupiga kweli<\/em>.\u201d<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Labda nizungumze kidogo kuhusu tabia nilizozisoma kwa Diamond tangu awali mpaka kufikia kipindi ninachosimulia hapa. Katika kipindi hicho nilishagundua tofauti kubwa kati ya Diamond na wasanii wengine wengi niliokuwa nawafahamu au niliowahi kufanya nao kazi. Na hiyo tabia naamini ndiyo iliyomfikisha Diamond hapo alipo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Jambo la kwanza, Diamond alikuwa jasiri na mtu asiyekata tamaa kwa matokeo yoyote aliyokutana nayo katika kazi. Hebu chukulia mfano mdogo huo, anapata <em>show<\/em> inaandaliwa kwa gharama kubwa na matangazo lakini unafika ukumbini watu hakuna.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kuna wasanii wengi nimewahi kuwashuhudia wakishindwa <em>&#8216;kupafomu stejini&#8217;<\/em> mara baada ya kuona idadi ya mashabiki walioingia ukumbini hairidhishi. Hii imewahi kutokea hata kwa wanamuziki wakongwe kama Muumini Mwinjuma ambaye wakati fulani alipokuwa akizindua albam zake mbili pale Diamond Jubilee Hall na kukosa mashabiki alishuka <em>stejini<\/em> akaenda kwenye chumba cha kukatia tiketi kuangalia hali ya kapu la hela ikoje na alipoona noti ni chache sana alishindwa kurejea stejini, akalala kwenye benchi na kupitiwa na usingizi mzito mpaka watu walipoanza kupiga kelele wakimuhitaji <em>stejini.<\/em><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1000\" height=\"672\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/WEMA-SEPETU.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-3699\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/WEMA-SEPETU.jpg 1000w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/WEMA-SEPETU-300x202.jpg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/WEMA-SEPETU-768x516.jpg 768w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/WEMA-SEPETU-150x101.jpg 150w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/WEMA-SEPETU-600x403.jpg 600w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/WEMA-SEPETU-696x468.jpg 696w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/WEMA-SEPETU-625x420.jpg 625w\" sizes=\"auto, (max-width: 1000px) 100vw, 1000px\" \/><figcaption class=\"wp-element-caption\">Wema Sepetu<\/figcaption><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Hata hivyo, licha ya kulazimishwa kurejea <em>stejini, show<\/em> hiyo ya uzinduzi ulimalizika kabla ya muda na Muumini Mwinjuma alitoweka ghafla <em>stejini<\/em> bila kufanya <em>&#8216;arenjimenti&#8217; <\/em>zozote za kuwarudisha wanamuziki majumbani kwao wala kurudisha vifaa vya bendi, baadhi vikiwa vya kuazima.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Baada ya tukio hilo mmmoja wa wanamuziki wakongwe nchini, Mafumu Bilali &#8216;Bombenga&#8217; alilalamika kwenye vyombo vya habari kuhusu Muumini Mwinjuma kutelekeza vifaa vyake vya muziki alivyomuazima kuvutumia kwenye shoo yake iliyofanyikia Ukumbi wa Diamond Jubilee Hall, akidai Muumini alimpigia simu na kimtaarifu avifuate vifaa hivyo mwenyewe.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Nimetoa mfano huo ili kuona ni jinsi gani Diamond alivyokuwa jasiri na asiyekata tamaa tangu kitambo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Lakini pia Diamond alikuwa mtu wa kujituma sana (hili nilishalizungumza sana huko nyuma,) na pia aliyependa kuthubutu. Jambo la mwisho na ambalo lilikuwa gumu sana kwa wasanii wengine wengi hasa kipindi cha nyuma ni kuhusu <em>skendo<\/em>. Diamond alikuwa hogopa <em>skendo<\/em> hata kidogo, habari mbaya na nzuri kwake ilikuwa sawa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kipindi cha nyuma wasanii hawakupenda kabisa<em> skendo<\/em>, nadhani walikuwa wakitekeleza ule msemo wa \u2018msanii kioo cha jamii.\u2019 Wanamuziki kama Ambwene Yesaya \u2018AY,\u2019 na Judith Wambura \u2018Lady Jay Dee&#8217; ni miongoni mwa wanamuziki ambao ilikuwa ukikosea kidogo kuwaandika au ukawabumbia <em>skendo<\/em> basi mwandishi na na wahariri wake wajiandae kufikishna mahakamani.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kuna wakati AY hata ukosee jambo dogo tu atapiga simu kulalamika na hapo ujue amekuheshimu sana. Hakupenda kabisa <em>skendo<\/em> lakini tangu ujio wa Diamond kukazaliwa kizazi kingine ambacho bila <em>skendo<\/em> mambo hayasongi.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Ingelikuwa <em>show<\/em> ile imefanywa na msanii legelege labda angeweza hata kupoteza fahamu lakini mwamba aliangusha tabasamu akatingisha kichwa na kusema; \u201cimetupiga kweli kweli.&#8217;<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><strong>UHUSIANO NA WEMA SEPETU<\/strong><\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Siku moja nikiwa kwenye kikao na viongozi wa Aljazeerah Entertainment nikasikia taarifa mpya. Mmoja wa wakurugenzi wa Aljazeera akatoa siri kwamba Wema Sepetu <em>\u2018amem-request\u2019<\/em> Diamond kwenye facebook. Alisema kwamba Diamond alimuonyesha facebook yake na kuona <em>request<\/em> ya Wema ambapo naye <em>ali-confirm<\/em> kisha wakaanza kuchati.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Chati za mwanzo toka kwa Wema zilikuwa zikimsifu Diamond kwa muziki wake. Diamond hakuamini jambo hilo ndipo akaamua kumuonyesha bosi huyo huku akimtambia kuwa lazima \u2018amnyooshe\u2019 Wema. Kipindi hicho Wema alikuwa nchini Marekani na ikumbukwe kuwa aliondoka nchini akiwa ni mpenzi wa mwanamuziki wa African Stars \u2018Twanga Pepeta,\u2019 Chalz Baba.<\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-full\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1000\" height=\"667\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/DIAMOND-NA-WEMA-2.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-3700\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/DIAMOND-NA-WEMA-2.jpg 1000w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/DIAMOND-NA-WEMA-2-300x200.jpg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/DIAMOND-NA-WEMA-2-768x512.jpg 768w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/DIAMOND-NA-WEMA-2-150x100.jpg 150w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/DIAMOND-NA-WEMA-2-600x400.jpg 600w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/DIAMOND-NA-WEMA-2-696x464.jpg 696w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/DIAMOND-NA-WEMA-2-630x420.jpg 630w\" sizes=\"auto, (max-width: 1000px) 100vw, 1000px\" \/><figcaption class=\"wp-element-caption\">Diamond na Wema Sepetu<\/figcaption><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kwa upande wangu suala hili halikunistua kwani nikijua muda si mrefu nitakuwa na <em>&#8216;breking news&#8221;<\/em> zitakazonisaidia kuuza gazeti. Nilimsikiliza bosi huyo kwa umakini ili siku <em>&#8216;dili&#8217; litakapotiki\u2019<\/em> niwe na <em>&#8216;full details&#8217;<\/em> za kuwapa wasomaji wa magazeti yetu.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Nilikumbuka jinsi Chalz Baba alivyokuwa amezama kwenye penzi la Wema Sepetu na kuvuta picha atakaposikia yuko kwa Diamond itakuwaje. Nikakumbuka pia jinsi watu walivyokuwa wakitabiri mwisho mbaya wa penzi la Wema na Chalz Baba kutokana na Wema kuwa tayari alishakuwa na rekodi ya kutodumu kwa wanaume.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Nikavuta picha zaidi nikakumbuka jinsi Chalz Baba alivyojitoa Muhanga kumsindikiza Wema Sepetu uwanja wa ndege na wakaagana kwa mabusu mazito huku kamera za mapaparazi zikishuhudia, akisikia yuko na Diamond sura yake ataificha wapi?<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Nikamuuliza mtoa taarifa wangu: \u201cUnaamini anayechati na Diamond ni Wema kweli au kuna mtu amejifanya ni yeye ili kumpima imani dogo?\u201d Akanijibu, \u201cni Wema kweli kwa sababu akaunti ya facebook ya Wema naifahamu vizuri.\u201d Nikayahifadhi maneno hayo akilini mwangu.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Siku zikaendelea kukatika huku ukaribu wa facebook kati ya Diamond na Wema ukiongezeka. Kama wanenavyo wahenga ya kuwa lisemwalo lipo, kama halipo laja. Siku Wema Sepetu alipotua jijini Dar es Salaam, akatua mikononi kwa Diamond.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Mapokezi makubwa yakafanyika Airport, picha zikapigwa na mapaparazi walioalikwa. Baada ya kutoka Airport safari ya Wema na Diamond ikaishia Sinza Madukani mitaa ya Namnani Hoteli alipokuwa akiishi Diamond.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Tetesi zikaanza kuzagaa mjini kuwa Chalz Baba kapigwa chini na Wema Sepetu. Kesho yake habari zikachapishwa kwenye magazeti ili zimfikie vizuri Chalz Baba. Mji ukachafuka, stori ya mjini ikawa ni Wema na Diamond, Chalz Baba akawa haelewi amekosea wapi<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Alichokumbuka ni kwamba waliachana vizuri na Wema na yeye ndiye aliyemsindikiza Airport wakati anakwenda Marekani. Hawakuwahi kugombana, sasa imekuwaje mpaka apokewe na Diamond? Kila alilowaza hakupata majibu.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><strong>NINI KILIENDELEA?<\/strong><\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><strong>USIKOSE KUFUATILIA SEHEMU YA SABA YA SIMULIZI HII YA KWELI NA YENYE MAFUNZO MENGI<\/strong><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>HIVI NDIVYO NINAVYOMFAHAMU DIAMOND PLATINUMZ &#8211; 6 HAMEES SUBA ILIPOISHIA Diamond na Vespa BAADA ya Diamond kuanza kuzishika noti, siku moja nikiwa naendesha gari katika barabara ya Tandale kuelekea Sinza, nikiwa maeneo ya Tanesco ghafla pikipiki aina ya Vespa &#8216;iliniovateki&#8217; kwa mwendo wa kasi sana hali iliyosababisha niitazame kwa jicho la hasira. Haikwenda mbali sana [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":3698,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[88],"tags":[],"coauthors":[],"class_list":["post-3697","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-burudani"],"amp_enabled":true,"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/WEMA-NA-DIAMOND.jpg","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3697","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=3697"}],"version-history":[{"count":2,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3697\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":3702,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3697\/revisions\/3702"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/3698"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=3697"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=3697"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=3697"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=3697"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}