{"id":3649,"date":"2022-11-25T14:45:28","date_gmt":"2022-11-25T14:45:28","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/?p=3649"},"modified":"2022-11-25T17:12:58","modified_gmt":"2022-11-25T17:12:58","slug":"dereva-anko-wabaka-mtoto-miaka-6-kwenye-school-bus","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=3649","title":{"rendered":"DEREVA, \u2018ANKO\u2019 WABAKA MTOTO MIAKA 6 KWENYE \u2018SCHOOL BUS\u2019"},"content":{"rendered":"\n<p class=\"wp-block-paragraph\">RIPOTA PANORAMA<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">MTOTO mwenye umri wa miaka sita anayesoma darasa la kwanza katika Shule ya Starlight Pre and Primary iliyopo Tegeta Wazo mkoani Dar es Salaam (jina kapuni) amebakwa na wanaume wawili watu wazima kwenye gari la shule, \u2018school bus.\u2019<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Wanaume hao ni dereva wa basi la Shule ya Starlight Pre and Primary na kondakta wake ambaye anafahamika zaidi na watoto kwa jina la \u2018anko\u2019 na kwamba mtoto huyo amekuwa akifanyiwa ukatili huo kwa muda mrefu bila kuwaambia wazazi wake kwa sababu wabakaji hao walikuwa wakimtisha kuwa akisema watamuua.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Akizungumza na Tanzania PANORAMA Blog, mzazi wa mtoto huyo (jina limehifadhiwa) amesema alibaini mtoto wake kufanyiwa kitendo hicho cha kikatili baada ya kulalamika mfululizo kuumwa na tumbo ndipo alipoanza kumdadisi jinsi anavyoumwa huku akimfanyia uchunguzi wa mwili.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cSiamini kwa sababu sikuwahi kufikiria wale watu wazima tena wa shule tunayoiamini kuwafuata watoto wetu nyumbani kuwapeleka shule na kuwarudisha wanaweza kufanya kitendo cha kikatili hivyo. Mtoto alikuwa haishi kulalamika kuumwa tumbo, nimempeleka Kitengule Hospitali zaidi ya mara tano, tunapewa dawa lakini malalamiko ya kuumwa tumbo hayaishi.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cMajuzi akaanza kulia tena tumbo linamuuma, nikachanganyikiwa kabisa maana kila nikienda hospitali hawaoni tatizo, nikaamua kukaa naye chini kumbembeleza huku nikimuuliza tumbo linaumaje, akawa anasita kusema, hapo akili ikashtuka.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cNikazidisha utulivu huku nikimbembeleza asilie bali aseme linaumaje akasema anaogopa kwa sababu watamuua, nikamuuliza akina nani, hakusema. Nikamwambia hakuna wa kumuua mimi nipo na baada ya kumbembeleza sana ndiyo akaanza kusema dereva na \u2018anko\u2019 wa gari lao la shule yaani \u2018school bus\u2019 huwa wanambaka, wanambaka kwa zamu.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cAlieleza kila kitu, alisema wanavyomshika mpaka wanavyomvua nguo na wao wanavyovua. Alisema wakati wanarudishwa nyumbani kutoka shuleni watoto wote huwa wanapelekwa kwanza anabaki yeye peke yake kwenye gari, kisha gari linapelekwa eneo la ukimya, wanafunga vioo na mapazia ya kwenye vioo vya gari ndiyo wanamtendea huo unyama, wakimaliza ndiyo wanamrudisha nyumbani huku wakimtisha kuwa akisema watamuua,\u201d alisema mzazi wa mtoto huyo na kuongeza.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cUsiku ule ule tulimpeleka hospitali akapata matibabu ya awali na wakatuambia ni kweli kaishaharibiwa kabisa. Tuliwasiliana na polisi usiku huo huo wakawahi nyumbani asubuhi asubuhi ile gari ya shule ilipofika tu yule dereva akatiwa nguvuni ila huyo mwenzake alikamatwa baadaye wakapelekwa kituo cha polisi cha Madale, kesi namba iliyofunguliwa ni MDL\/RB\/3889\/2022, KUBAKA. Hivi sasa tunaendelea na matibabu ya mtoto katika Hospitali ya Mwananyamala.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Tanzania PANORAMA Blog jana ilifika Shule ya Starlight Pre &amp; Primary na kukutana na mwalimu mkuu wa shule hiyo ambaye hakuwa tayari kujitambulisha jina na baada ya kuulizwa kuhusu tukio la kukamatwa kwa wafanyakazi wa shule yake, alisema hawezi kuliongea kwa sababu anajiandaa kwenda kuswali hivyo aulizwe meneja wa shule na kumuongoza mwandishi ofisi kwa meneja.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Alipoulizwa meneja wa shule ambaye naye hakujitambulisha jina lake alisema hana taarifa kuhusu tukio hilo na kuomba muda wa kuwasiliana na mkurugenzi wa shule ambaye aliomba kuongea na Tanzania PANORAMA Blog na kukanusha katakata wafanyakazi wa shule yake kubaka mtoto mwenye umri wa miaka sita huku akisisitiza wafanyakazi wake wote wapo kazini kama kawaida.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Baadhi ya wafanyakazi wa shule hiyo waliozungumza na Tanzania PANORAMA Blog wamethibitisha kukamatwa kwa wenzao wawili wanaotuhumiwa kumbaka mtoto huyo na kueleza kuwa uongozi wa shule unafanya kila jitihada kuficha ukweli.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Wakati uongozi wa Shule ya Starlight Pre and Primary ukikanusha kwa nguvu kubwa wafanyakazi wake kukamatwa kwa tuhuma za kumbaka mtoto mdogo wa miaka sita, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Mtatiro Kitinkwi amethibitisha kutokea tukio hilo na kueleza kuwa upelelezi umeishakamilika na jalada la kesi hiyo litapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><strong>Tanzania PANORAMA Blog INAENDELEA KUFUATILIA KWA KARIBU TUKIO HILI LA KIKATILI.<\/strong><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>RIPOTA PANORAMA MTOTO mwenye umri wa miaka sita anayesoma darasa la kwanza katika Shule ya Starlight Pre and Primary iliyopo Tegeta Wazo mkoani Dar es Salaam (jina kapuni) amebakwa na wanaume wawili watu wazima kwenye gari la shule, \u2018school bus.\u2019 Wanaume hao ni dereva wa basi la Shule ya Starlight Pre and Primary na kondakta [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":3650,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[],"class_list":["post-3649","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-habari-kitaifa"],"amp_enabled":true,"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/75634b7d-5884-4628-bdde-6ed87386f217.jpg","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3649","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=3649"}],"version-history":[{"count":3,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3649\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":3655,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3649\/revisions\/3655"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/3650"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=3649"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=3649"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=3649"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=3649"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}