{"id":3605,"date":"2022-11-16T06:08:45","date_gmt":"2022-11-16T06:08:45","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/?p=3605"},"modified":"2022-11-16T06:08:51","modified_gmt":"2022-11-16T06:08:51","slug":"mtihani-mzito-tra","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=3605","title":{"rendered":"MTIHANI MZITO TRA"},"content":{"rendered":"\n<p>RIPOTA PANORAMA<\/p>\n\n\n\n<p>MAMLAKA ya Mapato (TRA) jana ilijikuta katika mtihani mzito wa kutoa ufafanuzi wa majibu ya maswali sita iliyoulizwa na Tanzania PANORAMA Blog kuhusu masuala ya kikodi yenye utata.<\/p>\n\n\n\n<p>Hayo yalitokea baada ya Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo kushindwa kutoa ufafanuzi wa majibu ya maswali aliyokuwa ameulizwa awali na Tanzania PANORAMA Blog huku akilalamika kuandamwa na maswali kwa muda wa wiki mbili mfululizo.<\/p>\n\n\n\n<p>Tanzania PANORAMA Blog ilitaka ufafanuzi wa majibu yaliyotolewa na TRA ambayo yaliacha maswali yasiyokuwa na majibu ambapo msingi wa kuibuka kwa maswali hayo ni madai kuwa kampuni ya usafirishaji nafaka nje ya nchi ya Nine Five Group imekuwa ikicheza mchezo mchafu.<\/p>\n\n\n\n<p>Taarifa zilizoifikia Tanzania PANORAMA Blog awali zilidai kuwa Kampuni ya Nine Five Group imekuwa ikitumia nyaraka zenye dosari kusafirishia makontena ya nafaka kutoka hapa nchini kwenda nje ya nchi na kwamba imekuwa ikifanya hivyo kwa msaada wa baadhi ya watumishi wa kampuni moja ya uwakala wa usafirishaji na upokeaji mizigo.<\/p>\n\n\n\n<p>Ilidaiwa kuwa dosari zilizo kwenye nyaraka za Kampuni ni Nine Five Group ni pamoja na baadhi ya \u2018release order\u2019 zinazotolewa na TRA kwa kampuni hiyo kutoonyesha idadi na namba ya kontena wanazosafirisha kwenda nje ya nchi.<\/p>\n\n\n\n<p>Pia ilidaiwa zaidi kuwa Kampuni ya Nine Five imekuwa akikaa na \u2018release order\u2019 zinazotolewa na TRA kwa zaidi ya wiki tatu hali inayoibua shaka ya kutumiwa kwa matumizi mengine tofauti na yaliyokusudiwa.<\/p>\n\n\n\n<p>Vyanzo vya habari kutoka kampuni ya uwakala wa usafirishaji na upokeaji mizigo iliyohusika na usafirishaji wa kontena hizo vimedai kuwa \u2018release order\u2019 ni moja ya hatua za mwisho baada ya kampuni husika kukamilisha nyaraka zote za usafirishaji hivyo haipaswi kukaa muda mrefu kwa mteja bila kutoa mzigo ulipohifadhiwa na kupelekwa bandarini.<\/p>\n\n\n\n<p>\u201cInapotokea kampuni ikakaa na \u2018release order\u2019 kwa muda mrefu wa zaidi ya wiki tatu hamuoni kama kuna ujanja unaotumiwa na kampuni husika kusafirisha mizigo yake mingine kwa kutumia \u2018release order\u2019 hiyo kwa lengo la kudanganya idadi ya mizigo inayosafirisha?<\/p>\n\n\n\n<p>\u201cSiku waliposafirisha mizigo yao, \u2018Loading permission\u2019 ilionyesha kuwa kwa siku moja walisafirisha kontena 10 kwenda Qingdao, China lakini kontena hizi zote hazikuonekana kwenye \u2018release order\u2019 utaratibu huu sijui umeanza lini.<\/p>\n\n\n\n<p>\u201cWaliwezaje kusafirisha kontena kumi kwa siku moja kama inavyoonekana kwenye \u2018loading permission\u2019 lakini kwenye \u2018release order\u2019 hazionekani? Na kwenye \u2018release order\u2019 hiyo kuna malipo ya \u2018gross weight\u2019 zaidi ya milioni 80 kwa kilo zaidi ya 300,000, ni za nini?\u201d<\/p>\n\n\n\n<p>Ili kupata ukweli wa madai hayo, PANORAMA iliiuliza TRA iwapo ni ruksa kwa wafanyabiashara kutumia \u2018release order\u2019 moja kusafirisha mizigo zaidi ya iliyo kwenye \u2018release order\u2019 hiyo iliyopewa kwa mzigo iliyoombea? na TRA kupitia kwa Kayombo ilijibu kuwa siyo sahihi na haiwezekani lakini swali la pili liliuliza kuwa baadhi ya \u2018release order\u2019 zinazotolewa na mamlaka hiyo hazionyeshi idadi ya kontena zinazosafirishwa kwenda nje ya nchi wala namba ya kontena hizo ambapo TRA ilijibu jibu fupi kuwa; hilo ni sahihi.<\/p>\n\n\n\n<p>PANORAMA ilimuuliza Kayombo kuwa baadhi ya nyaraka zinazodaiwa kuibua mashaka ni zile zinazoonyesha kampuni hiyo ililipa \u2018gross weight\u2019 ya mamilioni ya shilingi. Je, kama biashara inayofanywa na kampuni hiyo haitozwi kodi, \u2018gross weight\u2019 iliyolipia ilikuwa ya nini na hapo Kayombo alitoa jibu jingine fupi kuwa; Hakuna kodi ya forodha kwenye nafaka labda walitapeliwa.<\/p>\n\n\n\n<p>Pia Kayombo aliulizwa \u2018Custom Clearence\u2019 inalipwa TRA au kwenye taasisi nyingine ya Serikali naye alijibu kuwa \u2018Customs\u2019 hakuna kodi ya aina hiyo na swali lililofuata liliuliza; kama \u2018release order\u2019 hutolewa na TRA naye alijibu kuwa inatolewa na taasisi yake hiyo na haina malipo.<\/p>\n\n\n\n<p>Swali jingine lilihoji; \u2018kama mizigo ya \u2018transit\u2019 huwa hailipiwi kodi hapa nchini bali hupewa \u2018release order\u2019 baada ya gharama za bandari na taasisi nyingine zinazoshughulikia mzigo husika kulipwa, hii maana yake ni kwamba kuna mizigo inayostahili kulipiwa kodi na isiyostahili, naomba kujua mizigo ya \u2018transit\u2019 hulipiwa kodi wapi?\u2019<\/p>\n\n\n\n<p>Akijibu, Kayombo alisema hakuna kodi ya forodha kwenye mizigo ya \u2018transit,\u2019 kama kuna malipo watu wanalipa waseme wamelipa wapi? au waonyeshe \u2018control numbers.\u2019<\/p>\n\n\n\n<p>Mlolongo wa maswali ulikuwa mrefu, lililofuata lilisomeka hivi; \u2018kama \u2018release order\u2019 inayotolewa na TRA haitaji idadi ya mizigo wala namba za kontena zinazosafirishwa, je huko wanakolipia kodi huwa wanajuaje kodi ya mzigo ambao haujatajwa kwenye \u2018release order\u2019 na Kayombo alijibu; \u2018hakuna kodi inayolipwa, idadi ya kontena inaonekana kwenye \u2018loading declarations.\u2019<\/p>\n\n\n\n<p>Swali la mwisho liliuliza hivi; \u2018naomba kuijua sheria inayoruhusu mizigo kusafirishwa kwenda nje ya nchi bila kuainishwa kwenye \u2018release order\u2019 na Kayombo alijibu \u2018ni utaratibu tu, sio sheria.<\/p>\n\n\n\n<p>Baada ya Tanzania PANORAMA Blog kuandika habari iliyokuwa na kichwa cha maneno \u2018TRA &#8211; hakuna kodi kusafirisha mazao ya chakula nje ya nje\u2019 ikinukuu maelezo yaliyotolewa na Kayombo kuhusu kutokuwepo kodi katika usafirishaji mazao ya nafaka nje ya nchi, baadhi ya wasomaji wetu waliwasiliana nasi na kuomba ufafanuzi zaidi wa maelezo yaliyotolewa na Kayombo kwa kile walichodai kuwa yalikuwa majibu ya jumla, yasiyoeleweka vizuri na yanayoacha maswali mengi.<\/p>\n\n\n\n<p>Tanzania PANORAMA Blog kwa kuzingatia majukumu yake ya kuelimisha na kuupasha umma habari sahihi, ilirejea tena kwa Kayombo ambaye ni Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA akiwa pia na dhamana ya usemaji kumuomba ufafanuzi wa majibu ya maswali iliyomuuliza awali na iliweka bayana kuwa ufafanuzi huo una lengo la kutoa elimu kwa umma, ilimuuliza;<\/p>\n\n\n\n<p>Mosi, Mamlaka ya Mapato (TRA) imeeleza kuwa hakuna kodi ya forodha inayotozwa kwenye mizigo ya \u2018transit,\u2019 kwa faida ya wasomaji wetu, tunaomba kujua \u2018custom value\u2019 inayotajwa kwenye \u2018release order\u2019 ya TRA kwa mizigo ya \u2018transit\u2019 ina maana gani? Naye alijibu hivi; \u2018Hakuna kodi kwenye transit, hiyo value ni kwa ajili ya statistics tu.\u2019<\/p>\n\n\n\n<p>Pili; Mamlaka ya Mapato (TRA) imeeleza kuwa kwenye \u2018release order\u2019 hakuna sheria iliyowekwa ya kuainisha namba ya kontena zinazosafirishwa wala idadi yake. Kwa faida ya wasomaji wetu, tunaomba kujua, je TRA inapotoa \u2018release order\u2019 bila kujua namba ya kontena wala idadi ya wanacho ki\u2018release\u2019 tafasili yake ni nini? Naye Kayombo alijibu; \u2018Cargo Ref Number ndio ina taarifa zote za mzigo, ipo pale kwenye release order.\u2019<\/p>\n\n\n\n<p>Swali la tatu ambalo Tanzania PANIORAMA Blog iliomba kupata ufafanuzi kutoka kwa Kayombo lilisomeka hivi; \u2018Ikiwa kuainisha namba na idadi ya kontena kwenye \u2018release order\u2019 ni utaratibu tu na sio sheria kama ilivyoelezwa na TRA, Tanzania PANORAMA Blog inaomba kujua, je, ni sahihi kuvunja utaratibu kwa sababu sio sheria? Naye Kayombo alijibu, \u2018Utaratibu upi unaovunjwa? Hakuna utaratibu uliovunjwa, idadi ya containers zote inaonekana kwenye \u2018loading permission\u2019 na ndio utaratibu wa mizigo ya \u2018export,\u2019 jibu ambalo haliendani na lile alilotoa awali kuwa kuainisha mzigo kwenye \u2018release order\u2019 si sheria bali ni utaratibu uliowekwa na TRA.<\/p>\n\n\n\n<p>Nne lilisomeka; \u2018Mbali na Kampuni ya Nine Five Group kudaiwa kuvunja utaratibu wa kuainisha idadi na namba za kontena kwenye \u2018release order,\u2019 Tanzania PANORAMA Blog inaomba kujua ni kampuni ngapi mlizoziruhusu au zilizojiamulia kuvunja utaratibu huo? Na jibu lake ni hili; \u2018Hatujaruhusu utaratibu kuvunjwa.\u2019<\/p>\n\n\n\n<p>La tano. \u2018Tanzania PANORAMA Blog inaomba kujua kuna haja gani kwa TRA kuunda utaratibu ambao hauna ulazima wa kuufuata? Naye alijibu; \u2018Hatujawahi kufanya hivyo.\u2019 Kayombo alitoa jibu hili ikiwa na siku chache tu baada ya kueleza kuwa kuanisha mizigo kwenye \u2018release order\u2019 ni utaratibu uliowekwa na TRA lakini siyo sheria lakini jana alikana kauli yake mwenyewe.<\/p>\n\n\n\n<p>Aidha, aliulizwa hivi; \u2018TRA imeeleza kuwa mizigo ya \u2018transit\u2019 hailipiwi kodi ya forodha, tunaomba kujua ni kodi zipi tofauti na forodha zinazolipwa kwa mizigo hiyo? Na yeye alijibu hivi; \u2018Hakuna kodi yoyote.\u2019<\/p>\n\n\n\n<p>Mwisho aliulizwa, \u2018TRA imeeleza kuwa \u2018release order\u2019 moja haiwezi kamwe kutumika kusafirisha mzigo zaidi ya uliokusudiwa, je, ikiwa \u2018release order\u2019 haitaji aina ya mzigo uliokusudiwa kusafirishwa, TRA inawezaje kufahamu kama mzigo unaosafirishwa ndio uliokusudiwa? Naye alijibu kuwa, \u2018TRA system inatambua vizuri aina ya mzigo uliokusudiwa kwa kila \u2018loading permission ref No.\u2019<\/p>\n\n\n\n<p>Jitihada za kumpata Waziri wa Fedha na Mipango ili atoe ufafanuzi wa kina wa maswali haya ambayo yameibua mkanganyiko mkubwa bado zinaendelea.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>RIPOTA PANORAMA MAMLAKA ya Mapato (TRA) jana ilijikuta katika mtihani mzito wa kutoa ufafanuzi wa majibu ya maswali sita iliyoulizwa na Tanzania PANORAMA Blog kuhusu masuala ya kikodi yenye utata. Hayo yalitokea baada ya Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo kushindwa kutoa ufafanuzi wa majibu ya maswali aliyokuwa ameulizwa awali na Tanzania [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":3387,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":false,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[],"class_list":{"0":"post-3605","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-habari-kitaifa"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/kayombo.jpg?fit=640%2C502&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3605","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=3605"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3605\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":3606,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3605\/revisions\/3606"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/3387"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=3605"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=3605"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=3605"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=3605"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}