{"id":257,"date":"2022-05-29T13:12:00","date_gmt":"2022-05-29T13:12:00","guid":{"rendered":"https:\/\/msangirstz8.wordpress.com\/2022\/05\/29\/mastaa-wa-muziki-afrika-waachia-african-lullabies-part-2-kwa-kishindo\/"},"modified":"2022-11-10T08:51:31","modified_gmt":"2022-11-10T08:51:31","slug":"mastaa-wa-muziki-afrika-waachia-african-lullabies-part-2-kwa-kishindo","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=257","title":{"rendered":"MASTAA WA MUZIKI AFRIKA WAACHIA AFRICAN LULLABIES PART 2 KWA KISHINDO"},"content":{"rendered":"<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size: large;\">JOSEPH SHALUWA<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size: large;\">KIKOSI kazi cha kusherehekea mwezi wa Afrika kwenye mkusanyiko wa nyimbo zenye mahadhi ya Kiafrika zilizopewa jina la African Lullabies Part 2, kimeachia toleo la pili kutoka kwa kizazi cha muziki wa Kiafrika.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size: large;\">Mastaa kadhaa kutoka pande mbalimbali za Afrika wameshiriki katika ujio huo, wakiwemo\u00a0 Asa, Ayra Starr, Karun, Teni, Simi, WurlD, Olayinka Ehi, Tresor, Manana, Aymos na Ntsika. <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size: large;\">Wakati katika sehemu ya kwanza, &#8211; African Lullabies Part 1 iliangazia utunzi asilia wa waimbaji na watunzi wa nyimbo wa Afrika Kusini huku ikiimbwa katika lugha mbalimbali, safari hii inapanuka zaidi ya mipaka ya Afrika Kusini na kutoa toleo tofauti la muziki wa watoto katika lugha mbalimbali za Kiafrika.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size: large;\">Nyimbo zote ni tungo asili za wasanii, zikichorwa kutokana na uzoefu wao katika ngano za Kiafrika, huku zingine zikiwa ni tafsiri za nyenzo zilizotolewa hapo awali zilizopangwa na kurekodiwa tena.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size: large;\">Ikiwa ni mara ya kwanza kwa msanii Karun kutunga wimbo wa kwanza kwa ajili ya watoto, alisema: &#8220;Ilinifurahisha sana pale nilipotakiwa kutengeneza wimbo kwa ajili ya watoto, Huu ni wimbo wangu wa kwanza wa watoto, sikuwahi kufikiria ningefanya. <\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size: large;\">\u201cNimefurahia sana kufanya muziki huu wa utulivu. Sijawahi kuona muziki wa watoto kama kitu ambacho ningefanya lakini nilipopewa nafasi nimeonyesha uwezo wangu wote. Binafsi nina mtoto wa kiume na ninapenda sana watoto, imekuwa kitu kizuri sana kwangu.\u201d<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size: large;\">Karun ameongeza kusema, amejifunza mengi kutoka kwake mwenyewe wakati alipokuwa akiandika wimbo huo.<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size: large;\">\u201cNimetayarisha wimbo wote mwenyewe, napenda sana mikito mizuri, kwa hiyo nilichofanya ni kucheza na mikito ya aina mbalimbali wakati wa utayarishaji. Kuna mengi ya kujifunza katika kibao hiki. Pia nilijifunza kuna mengi zaidi ninayohitaji kuunganisha katika lugha yangu ya mama ya Kikikuyu.\u00a0<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\">\n<table class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left: auto; margin-right: auto;\" cellspacing=\"0\" cellpadding=\"0\" align=\"center\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align: center;\"><a style=\"margin-left: auto; margin-right: auto;\" href=\"https:\/\/blogger.googleusercontent.com\/img\/b\/R29vZ2xl\/AVvXsEi-aRmD8TWJFEEkTJWZFtJqhiubhoE3ylVmCvp0HBxO6a1RRRKWfkXOF8Q9T3KvkqWELBWp63r35I2KGVE0uL0--hMvmcxTc0aOYJDkJmUSc_26ibdtT4C9Mpa5qznr0wvbeVrOJsIjrr01L66GNItZjc6yeot-KpBZ3kJNGif05rseWsvro3YOwH88tg\/s1080\/shaluwa%202.jpg\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" src=\"https:\/\/blogger.googleusercontent.com\/img\/b\/R29vZ2xl\/AVvXsEi-aRmD8TWJFEEkTJWZFtJqhiubhoE3ylVmCvp0HBxO6a1RRRKWfkXOF8Q9T3KvkqWELBWp63r35I2KGVE0uL0--hMvmcxTc0aOYJDkJmUSc_26ibdtT4C9Mpa5qznr0wvbeVrOJsIjrr01L66GNItZjc6yeot-KpBZ3kJNGif05rseWsvro3YOwH88tg\/w512-h640\/shaluwa%202.jpg\" width=\"512\" height=\"640\" border=\"0\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align: center;\"><i>Karun<\/i><\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size: large;\">\u201cKuna wakati ilibidi bibi yangu kunikumbusha baadhi ya maneno. Kikuyu ni lugha yangu ya kwanza lakini niliisahau muda mrefu uliopita, hivyo nilijifunza kuwa bado ninaunganishwa nayo.&#8221;<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size: large;\">Kwa upande wa msanii Ayra Starr anasema, \u201cShangazi yangu ni kila kitu kwangu na alijifungua miezi mitatu iliyopita. Kwa hiyo ikawa ni kama nimemtengenezea mpwa wangu wimbo. Nakumbuka wakati tunakua, tulitunga nyimbo sisi wenyewe, shuleni pia tulikuwa tukitengeneza nyimbo zetu wenyewe kwa sababu hatukutaka kuimba &#8220;Twinkle, twinkle, little star.&#8221;<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size: large;\">Majina ya wasanii walioshiriki kwenye albamu hiyo na nyimbo zao kwenye mabano ni pamoja na Psalms of Suli (Hello Little One), Teni (One Day), Simi (Iya Ni Wura), Karun (Dream Lullaby (Wakarir\u00fc) na Tresor (La Vie Est Belle).<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size: large;\">Wengine ni Olayinka Ehi (Sweet One), Asa (Little Darling), Ayra Starr (Stars), Aymos (Lullaby Song), Ntsika (Busuku Benzolo), WurlD (Never Alone) na Manana (In The Morning).<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size: large;\">Kusikiliza ingia hapa: https:\/\/platoon.lnk.to\/African-Lullabies-Part2<\/span><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>JOSEPH SHALUWA KIKOSI kazi cha kusherehekea mwezi wa Afrika kwenye mkusanyiko wa nyimbo zenye mahadhi ya Kiafrika zilizopewa jina la African Lullabies Part 2, kimeachia toleo la pili kutoka kwa kizazi cha muziki wa Kiafrika. Mastaa kadhaa kutoka pande mbalimbali za Afrika wameshiriki katika ujio huo, wakiwemo\u00a0 Asa, Ayra Starr, Karun, Teni, Simi, WurlD, Olayinka [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":3473,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","footnotes":""},"categories":[79],"tags":[],"coauthors":[],"class_list":{"0":"post-257","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-michezo"},"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/257","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=257"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/257\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":3474,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/257\/revisions\/3474"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/3473"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=257"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=257"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=257"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=257"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}