{"id":221,"date":"2022-06-06T10:06:00","date_gmt":"2022-06-06T10:06:00","guid":{"rendered":"https:\/\/msangirstz8.wordpress.com\/2022\/06\/06\/waziri-mkuu-akemea-utiririshaji-maji-machafu\/"},"modified":"2022-06-06T10:06:00","modified_gmt":"2022-06-06T10:06:00","slug":"waziri-mkuu-akemea-utiririshaji-maji-machafu","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=221","title":{"rendered":"WAZIRI MKUU AKEMEA UTIRIRISHAJI MAJI MACHAFU"},"content":{"rendered":"<p class=\"MsoNormal\" style=\"text-align:left;\"><span style=\"font-size:medium;\"><\/p>\n<table align=\"center\" cellpadding=\"0\" cellspacing=\"0\" class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/blogger.googleusercontent.com\/img\/b\/R29vZ2xl\/AVvXsEgVZn1D7NMYmVzM2AO9FSSKgseF4KT1DlzRY5WXLZCWUjCpv8xHroMB3yeDmFBiCC8Wvc4J03gSQW9-e42FT9V1U_dHgVbFAFYK7THYLfKyvjyNsiY-75VwMhoYC2w_Zog_cGG9mckHVY1uHjspcYT53u6VY-OEeD772CPZLmqcsV1IbhVZ_nc98fzjUg\/s4176\/pm2.JPG?ssl=1\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"306\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/blogger.googleusercontent.com\/img\/b\/R29vZ2xl\/AVvXsEgVZn1D7NMYmVzM2AO9FSSKgseF4KT1DlzRY5WXLZCWUjCpv8xHroMB3yeDmFBiCC8Wvc4J03gSQW9-e42FT9V1U_dHgVbFAFYK7THYLfKyvjyNsiY-75VwMhoYC2w_Zog_cGG9mckHVY1uHjspcYT53u6VY-OEeD772CPZLmqcsV1IbhVZ_nc98fzjUg\/w640-h306\/pm2.JPG?resize=640%2C306&#038;ssl=1\" width=\"640\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align:center;\"><i>Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza jana katika siku ya maadhimisho ya mazingira duniani <br \/><\/i><\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<p><i>\u00a0<\/i>\u00a0<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"text-align:left;\"><span style=\"font-size:medium;\">\u00a0<span style=\"font-family:Georgia;\">*Aagiza uhifadhi wa mazingira nchini,<\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\">*\u00a0Ataka\u00a0mpango kabambe wa mazingira utengewe bajeti<\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\">RIPOTA WA WAZIRI MKUU<\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><\/span><\/span><!--[if gte mso 9]&gt;1111&lt;![endif]--><!--[if gte mso 9]&gt;&lt;![endif]--><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"text-align:left;\"><span style=\"font-size:medium;\"><span style=\"font-family:Georgia;\">WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amekemea tabia ya utiririshaji wa maji machafu na majitaka kutoka viwandani na kwenye migodi kwani inachangia kuhatarisha usalama wa afya ya binadamu na mazingira.<\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\">Akizungumza jana katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambayo ilifanyika kitaifa jijini Dodoma ikiwa na kauli mbiu ya &#8216;Tanzania ni moja tu, Tanzania mazingira, alikemea tabia ya uchomaji miti, uvamizi na uharibifu wa mapori tengefu, ukataji wa miti holela kwa ajili ya uchomaji wa mkaa, uvamizi na uharibifu wa vyanzo vya maji pamoja na uchomaji moto misitu.<\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><span style=\"font-family:Georgia;\">\u201cHivi karibuni tumeshuhudia kutoweka kwa baadhi ya viumbe hai, maeneo mengi ya vyanzo vya maji yameathirika kutokana na ukame wa mara kwa mara, uchafuzi wa mazingira unaotokana na majitaka na kemikali kutokana na shughuli za viwandani.\u00a0 Uchafuzi huu umeendelea kuongezeka kwa kasi nchini na kuathari maji, hewa na ardhi. Hali hii inahatarisha usalama wa afya ya binadamu na mazingira.<\/span><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\">\u00a0<\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><span style=\"font-family:Georgia;\">\u201cKutokana na kuongezeka kwa uharibifu wa mazingira, ninaagiza wizara na taasisi husika, pamoja na wananchi kwa ujumla, kuimarisha ushirikiano katika kukomesha uvamizi na uharibifu wa mapori tengefu kote nchini. Ninawasihi wananchi tutoe ushirikiano wa kutosha kuhakikisha tunarejesha misitu, ikolojia na uoto wa asili katika maeneo yetu, hususan maeneo ambayo miti ya asili iko kwenye tishio la kutoweka. Tuwe walinzi wazuri wa mazingira kwa faida ya kizazi hiki na kijacho,\u201d alisisitiza Waziri Mkuu Majaliwa.<\/span><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\">Wakati huohuo,\u00a0Waziri Mkuu Majaliwa ametoa maagizo 15 kwa wizara, taasisi na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu uhifadhi wa mazingira nchini na kutaka yatekelezwe kikamilifu.<\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\">Akizungumza na washiriki wa maadhimisho hayo kwa niaba ya Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango, Waziri Mkuu Majaliwa amesema Wizara ya Fedha na Mipango ihakikishe\u00a0mpango kabambe wa usimamizi na hifadhi ya mazingira unakuwa sehemu ya vipaumbele\u00a0vya bajeti vya kila mwaka kwa kipindi chote cha utekelezaji wake wa miaka 10.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"text-align:left;\"><span style=\"font-size:medium;\"><span style=\"font-family:Georgia;\"><\/p>\n<table align=\"center\" cellpadding=\"0\" cellspacing=\"0\" class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/blogger.googleusercontent.com\/img\/b\/R29vZ2xl\/AVvXsEhMrzYjMS-LmINn6zha0bahS6sOpryw7ElcatXo9gjt0rnbvLkzG7c83JLcRNjNO_8a5KVI_W4gg2lFTiFpY4IbOa1i5IWiARc6_2WeP8_lkSqFlj7-xXVlfFajS6bgwsXWyXJF8CJiQGcternoW5sqwf2n4A_tiXW5J0TqjR4OwdkcUcS2KMjHUz2EfQ\/s3400\/pm%201.JPG?ssl=1\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"434\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/blogger.googleusercontent.com\/img\/b\/R29vZ2xl\/AVvXsEhMrzYjMS-LmINn6zha0bahS6sOpryw7ElcatXo9gjt0rnbvLkzG7c83JLcRNjNO_8a5KVI_W4gg2lFTiFpY4IbOa1i5IWiARc6_2WeP8_lkSqFlj7-xXVlfFajS6bgwsXWyXJF8CJiQGcternoW5sqwf2n4A_tiXW5J0TqjR4OwdkcUcS2KMjHUz2EfQ\/w640-h434\/pm%201.JPG?resize=640%2C434&#038;ssl=1\" width=\"640\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align:center;\"><i>Waziti Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika siku ya mazingira duniani iliyoadhimishwa Jijini Dodoma jana<\/i><\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<p>\u00a0<\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\">Alisema wizara za kisekta na Mamlaka za Serikali za Mitaa zihakikishe mpango kabambe wa hifadhi na usimamizi wa mazingira unajumuhishwa katika mipango na bajeti zao, sambamba na kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji Ofisi ya Makamu wa Rais.<\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\">Alizitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kusimamia uboreshaji wa maeneo yaliyoharibiwa kwa kupata tena miti. <\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><span style=\"font-family:Georgia;\">\u201cKila Mamlaka ya Serikali za Mitaa ihakikishe maeneo yote yaliyoharibiwa yanarejeshwa kwa kupandwa miti upya na kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa ihakikishe inatekeleza vema programu ya kitaifa ya upandaji miti 1,500,000 ili kuhakikisha nchi yetu inakuwa ya kijani,\u201d alisisitiza.<\/span><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\">Waziri Mkuu Majaliwa alizitaka wizara, taasisi, mashirika ya Serikali na binafsi yanayotumia nishati ya kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia au shughuli nyingine za uzalishaji kuanza kutumia nishati mbadala na kwamba kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa ihakikishe inadhibiti matukio ya uchomaji ovyo misitu.<\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\">Kuhusu tafiti za nishati mbadala na viumbe vamizi, Waziri\u00a0Mkuu Majaliwa alizitaka\u00a0taasisi za utafiti na vyuo vya elimu ya juu kuendelee kufanya tafiti za nishati mbadala ili kuondokana na utegemezi wa nishati ya kuni na mkaa kwa kupikia.<\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\">Aidha, alitaka zifanyike tafiti za namna ya kuzuia na kudhibiti kuenea kwa viumbe vamizi vinavyochangia uharibifu wa mazingira nchini.<\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\">Kuhusu takataka, alizitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa ziweke utaratibu wa kuhakikisha taka zinatenganishwa na zinakusanywa na zile zinazohusika na usimamizi wa mifereji ya maji ya mvua mijini kuhakikisha mifereji hiyo inasafishwa ili kupunguza matukio ya mafuriko.<\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\">Kuhusu misitu na uoto wa asili, Waziri Mkuu Majaliiwa alisema kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa ihakikishe maeneo yaliyotengwa kwa matumizi ya misitu ya mijini katika mamlaka zao hayabadilishwi matumizi wala kuvamiwa. <\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><span style=\"font-family:Georgia;\">\u201cSekta zinazohusika zihakikishe kuwa ardhi na uoto asili katika vyanzo vya maji, vilima na milima iliyo katika maeneo yao inalindwa na kuhifadhiwa ili kuzuia mmomonyoko wa udongo na kukauka kwa vyanzo hivyo vya maji,\u201d aliongeza na kusisitiza kuwa vilima vinavyozunguka mji wa Dodoma vihifadhiwe.<\/span><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\">Kuhusu\u00a0kilimo cha umwagiliaji maji, Waziri Mkuu Majaliwa alizitaka sekta zinazohusika na usimamizi wa shughuli za umwagiliaji mashamba kuhakikisha kunakuwepo matumizi sahihi ya maji yenye kuzingatia uhifadhi na ulinzi wa mazingira.<\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\">Kuhusu hifadhi za wanyamapori, alizitaka mamlaka zinazohusika na usimamizi wa hifadhi za wanyamapori kudhibiti matukio ya ajali za barabarani kwa wanyamapori, na pia zidhibiti shughuli za binadamu pamoja na uvamizi katika maeneo ya mapito ya wanyamapori (shoroba) ili kupunguza uharibifu wa mazao, mali na binadamu kupoteza maisha kutokana na kuwepo mwingiliano wa wanyama na binadamu.<\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\">Kwa upande wake,\u00a0Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamiu wa Rais anayeshughulikia mazingira, Dk. Suleiman Jafo alisema ofisi yake imezindua mpango wa soma na mti ambapo kila mwanafunzi anapaswa kupanda mti mmoja.<\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><span style=\"font-family:Georgia;\">\u201cTumezindua kampeni ya\u00a0Soma na Mti\u00a0ambapo wanafunzi milioni 14.5 kutoka shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu wameshiriki kwa kupanda mti mmoja mmoja.<\/span><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\"><br \/><\/span><span style=\"font-family:Georgia;\">Waziri Mkuu Majaliwa alizindua\u00a0mpango kabambe wa hifadhi ya mazingira\u00a0na kutoa tuzo kwa\u00a0mabalozi wa mazingira na viongozi wakuu watano akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\" style=\"text-align:left;\"><span style=\"font-size:medium;\"><span style=\"font-family:Georgia;\"><\/span><\/span><\/p>\n<div class=\"separator\" style=\"clear:both;text-align:center;\"><span style=\"font-size:medium;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/blogger.googleusercontent.com\/img\/b\/R29vZ2xl\/AVvXsEjR9fMSLS4Jl2FJ5YnPiy239xsr3w4tE_LsK-pHIkOWoXkOQ1NqjpnNM07VuT3-ipdyfWKwBtwJpuJnxSFqt0xCDWyuhRrcUk9kUBkceWgmM6_wKKMivIJ67-vwUu1zPRQWxB2iUy9oOtSUU5jwWNhEAZDQvAXqvHUHqXnGODPoXyAscZb8kezG5D2eEQ\/s2560\/pm3.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:1em;margin-right:1em;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"450\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/blogger.googleusercontent.com\/img\/b\/R29vZ2xl\/AVvXsEjR9fMSLS4Jl2FJ5YnPiy239xsr3w4tE_LsK-pHIkOWoXkOQ1NqjpnNM07VuT3-ipdyfWKwBtwJpuJnxSFqt0xCDWyuhRrcUk9kUBkceWgmM6_wKKMivIJ67-vwUu1zPRQWxB2iUy9oOtSUU5jwWNhEAZDQvAXqvHUHqXnGODPoXyAscZb8kezG5D2eEQ\/w640-h450\/pm3.jpg?resize=640%2C450&#038;ssl=1\" width=\"640\" \/><\/a><\/span><\/div>\n<p><span style=\"font-size:medium;\"><br \/>\u00a0<\/span><span style=\"font-family:Georgia;font-size:16pt;\"><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Georgia;font-size:16pt;\">\u00a0<\/span><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza jana katika siku ya maadhimisho ya mazingira duniani \u00a0\u00a0 \u00a0*Aagiza uhifadhi wa mazingira nchini,*\u00a0Ataka\u00a0mpango kabambe wa mazingira utengewe bajetiRIPOTA WA WAZIRI MKUU WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amekemea tabia ya utiririshaji wa maji machafu na majitaka kutoka viwandani na kwenye migodi kwani inachangia kuhatarisha usalama wa afya ya binadamu na mazingira.Akizungumza [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":false,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[1],"tags":[34],"coauthors":[],"class_list":{"0":"post-221","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","6":"category-uncategorized","7":"tag-habari"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/221","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=221"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/221\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=221"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=221"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=221"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=221"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}