{"id":1999,"date":"2017-08-25T15:14:00","date_gmt":"2017-08-25T15:14:00","guid":{"rendered":"https:\/\/msangirstz8.wordpress.com\/2017\/08\/25\/kikwete-anaogopa-tumtie-moyo\/"},"modified":"2017-08-25T15:14:00","modified_gmt":"2017-08-25T15:14:00","slug":"kikwete-anaogopa-tumtie-moyo","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=1999","title":{"rendered":"KIKWETE ANAOGOPA, TUMTIE MOYO"},"content":{"rendered":"<p><!--[if gte mso 9]&gt;   Normal  0          false  false  false    EN-US  X-NONE  X-NONE                                       MicrosoftInternetExplorer4                                     &lt;![endif]--><br \/><!--[if gte mso 9]&gt;                                                                                                                                                                                                                                                                                    &lt;![endif]--><!--[if gte mso 10]&gt; \/* Style Definitions *\/  table.MsoNormalTable  {mso-style-name:\"Table Normal\";  mso-tstyle-rowband-size:0;  mso-tstyle-colband-size:0;  mso-style-noshow:yes;  mso-style-priority:99;  mso-style-qformat:yes;  mso-style-parent:\"\";  mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;  mso-para-margin-top:0in;  mso-para-margin-right:0in;  mso-para-margin-bottom:10.0pt;  mso-para-margin-left:0in;  line-height:115%;  mso-pagination:widow-orphan;  font-size:11.0pt;  font-family:\"Calibri\",\"sans-serif\";  mso-ascii-font-family:Calibri;  mso-ascii-theme-font:minor-latin;  mso-fareast-font-family:\"Times New Roman\";  mso-fareast-theme-font:minor-fareast;  mso-hansi-font-family:Calibri;  mso-hansi-theme-font:minor-latin;  mso-bidi-font-family:\"Times New Roman\";  mso-bidi-theme-font:minor-bidi;} &lt;![endif]--> <\/p>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<table align=\"center\" cellpadding=\"0\" cellspacing=\"0\" class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;text-align:center;\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/4da3b-jk.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"212\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/4da3b-jk.jpg?resize=320%2C212&#038;ssl=1\" width=\"320\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align:center;\">Jakaya Kikwete <\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<p><\/p>\n<div class=\"separator\" style=\"clear:both;text-align:center;\"><\/div>\n<p><\/p>\n<div class=\"separator\" style=\"clear:both;text-align:center;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>RAFIKI yangu Rais Jakaya Kikwete amekumbwa na woga mkuu kiasi kwamba sasa anajiogopa hata yeye mwenyewe.<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Anaogopa kufanya mambo yaliyo ndani ya uwezo wake. Hali hii si nzuri, tunapaswa kumsaidia kuondoka nayo. Kwa pamoja tunapaswa kumtia moyo.<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Tukimuacha, ataendelea kuogopa kwa kipindi kirefu. Atakuwa anaogopa kukutana na mimi rafiki yake, kisa, kiherehere changu cha kumwandama kili ahudhurie mdahalo wa wagombea urais.\u00a0<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Atakuwa anaogopa kukutana na watu wanaomtaka sana kwenye mdahalo, na hasa atakuwa anaogopa kukutana na watu wenye akili. Sitaki jambo hili litokee. Sitaki tuwe na rais mwoga.<\/span><span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Ili kumsaidia kuondokana na hali hiyo ya woga, sote kwa pamoja tunapaswa kuungana, tuwe na kauli moja ambayo itamshinikiza kutusikiliza.\u00a0<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Na kwa sauti hiyo moja tumkataze kuwasikiliza watu wawili, Yusuph Makamba na Abdurahaman Kinana kwa sababu wanampotosha. Wanamshauri ajiweke katika hali ya kipindi cha ujima.\u00a0<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Wala hakuna haja ya kuwajadili kwa undani Makamba na Kinana kwa sababu tumekwishabaini kuwa hamtakii mema, wanataka aonekane ni wa kisoma cha watu wazima hivyo hata wadhfa wa urais aliupata kiujanja ujanja tu lakini hakustahili na hastahili. Kwamba licha ya kuhudhuria masomo pale mlimani, haieleweki kama alielimika kweli au vipi!<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Makamba na Kinana wanataka Kikwete awaone ndiyo tegemeo la pekee la yeye kuingia Ikulu, eti bila wao Ikulu hawezi kuiona hivyo chochote wanachomshauri hata kama wengine tunakiona cha kipuuzi, ni lazima akikubali kama anataka msaada wao wa kumuwezesha kuendelea kukaa magogoni.\u00a0<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Hili ni lazima tulikatae kwa sababu sisi ndiyo wenye uwezo wa kumbakiza hapo kwa kura zetu. Tukikataa, tutamfukuza Ikulu kwa kutompigia kura.<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Tukimwacha akubaliane nao tutakuwa tunampoteza, tumpigie kelele awafukuze. Akishawafukuza kwa sababu tayari amekwishajawa na woga tumtie moyo kwa kumwelekeze kufanya haya hata kama yatamgharimu kiasi cha kukosa ukubwa anaoutafuta, lakini atabaki na heshima yake tofauti na kuendelea kuwa mtawala asiye heshimiwa na watu wake.\u00a0<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Wakimuona wanamcheka na kumkashfu kuwa rais asiyekuwa na chochote kichwani ! Ikiwa hivyo, itakuwa aibu!<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Ingawa jambo hili limezungumzwa mara nyingi na watu wengi mimi nikiwa mmoja wao. Kwa ni njema kabisa narudia tena kulizungumza ili kuulainisha moyo wa rafiki yangu uliopondeka pondeka kwa woga ambao hapaswi kuwa nao kwa sababu ninaamini kuwa anao ubavu wa kujenga hoja zenye mashiko kwenye mdahalo wa aina yoyote kulingana na historia yake kielimu na hata katika utumishi wa taifa letu na kimataifa.<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Jambo la kwanza na la msingi tunalopaswa kufanya ni kumuombea kwa Mungu amjalie afya njema na kamwe asiwe na mawazo ya kutegemea nguvu za giza kumlinda.\u00a0<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Akatae kwa nguvu zake zote kulindwa na mashetani hata kama anayemfikishia ujumbe huo wa kulindwa na mashetani awe ametumwa kutoka mbinguni. Katika hilo awe tayari kutofautiana na malaika kama ndiye atakayemfikishia ujumbe huo na mimi nitamuunga mkono.<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Katika maombi yetu hayo tusisahau kusali ile sala ya kuomba asiwahofie washindani wake wa kiti cha urais. Awaone ni watu wa kawaida tu kama yeye ambao anaweza kukutana nao mahali popote katika tukio la aina yoyote.<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Ajiamini kuwa anaweza kwani kipindi cha miaka mitano ya urais na kile cha miaka kumi cha uwaziri wa mambo ya nje si haba, kimemjengea uwezo wa kutosha kwa kushiriki midahalo ya kila aina ndani na nje ya nchi.<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Inawezekana anawaza kama mimi kwamba kwenye mdahalo huo anaougopa viherehere wataibua hoja za serikali yake kushindwa vibaya kutekeleza ahadi zake, jambo ambalo ni kweli na yeye hana majibu yake.\u00a0<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Issue za ufisadi na kila aina ya uchafu unaoelekezwa katika serikali iliyoko madarakani. Anaogopa kwenda mbele ya jukwaa la mdahalo kwa sababu hapo hakuna ujanja ujanja kama kwenye majukwaa ya kampeni, hivyo anaweza kujikuta akiumbuka.<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Mimi napenda kumtia moyo kuwa hao jamaa wakiibuka na issue hizo, asiwe na haraka ya kuzijibu. Awaache watoe tuhuma na mashambulizi yote kisha yeye akubali, aseme, ndiyo serikali yake kwa kipindi cha miaka mitano imeshindwa kabisa kutekeleza ahazi zake, imeshindwa kumaliza tatizo la rushwa na hata kupambana na mafisadi.\u00a0<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Aende mbele zaidi kwa kueleza kwamba kwa kutambua kuwa ameshindwa alikuwa na mpango wa kukaa kando baada ya kumaliza muhula wake wa uongozi wa miaka mitano. Lakini pamoja na kushindwa huko, ni yupi wa kumuachia ulaji alionao kwa sababu wote waliopo wanaonekana wana tamaa?<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Maelezo haya hayatakuwa yanajibu maswali ya msingi bali yatakuwa yanahamisha kabisa mada nzima kwa kuwachanganya washiriki wote wa mdahalo.\u00a0<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Rafiki yangu Kikwete, hii ni siri ninakupa na nakuomba uniamini. Watu wote wenye akili waliozoe kufikiri mambo magumu huwa wanachanganywa kwa mambo rahisi na mapesi kabisa. Profesa na Daktari wamezoe kufikiri vitu vigumu sasa ukiwapa vya huku uswahili, walah utawaacha tu!\u00a0<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Na mimi siku zote ninapokutana na watu wa aina hiyo huwa nawachanganya kwa namna hiyo niliyoeleza, huwa nawasikiliza kwa umakini, nikiona wanaanza kuniacha, nawachanganyia mada, wanachanganyikiwa na kubaki wanabishana wenyewe kwa wenyewe bila kupata jibu sahihi. Hii ndiyo siri ya mchokonozi kuwa rafiki kipenzi wa wakubwa, wewe mwenyewe ukiwemo.\u00a0 \u00a0\u00a0\u00a0<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Ili kuhalalisha ulichokisema, unaweza kutoa mfano mwepesi unaoeleweka vizuri kwa wapiga kura wa uswahilini waliochoka sana kimaisha kwa kusema kuwa, ni kweli unatambua serikali yako haikufanya vizuri, ukakiri kushindwa na kwamba unastahili kufukuzwa na wapiga kura. Lakini wakikufukuza, mbadala wako ni nani?<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Ndani ya chama chetu hakuna, wote ni kama kondoo. Hakuna aliyejitokeza kuwania kiti chako ingawa wanajua ni kweli umeshindwa. Na walipopotoshwa na yule mfuga majini unayemsaidia vijisenti kidogo anapoumwa kuwa atakayekupinga atakufa, ndiyo kabisa wakaanza kuimba mapambio ya kukusafishia njia ya kuendelea kutawala kwa miaka mingine mitano. Huko wote hawana sifa.<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Kwa wapinzani, sawa kuna Profesa na Daktari. Profesa anakubalika maeneo fulani na Daktari naye anakubalika katika maeneo fulani ingawa yeye anaonekana kutikisa zaidi. Lakini wote wanagombea utukufu mmoja hivyo lazima watagawana kura.<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Zako ziko pale pale na kama zitapungua basi ni kidogo. Kwanini hawa kama nia ni kukuondosha madarakani wasiungane wakakung\u2019oa kiurahisi badala ya sasa wanapopigana vikumbo wenyewe kwa wenyewe kutaka kupanga kwenye nyumba uliyopanga. \u00a0<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Wote wanahubiri ubaya wa ufisadi, wote wana nia ya kuwaletea watanzania mabadiliko ya maisha, wote wanajua wewe umeshindwa ingawa unang\u2019ang\u2019ania kuendelea nadhani kwa sababu ya mapochopocho ya hapo Ikulu, sasa wameshindwa nini kuungana wakatekeleza nia yao moja kwa pamoja?<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Hawa wana tamaa, hawafai. Mpaka hapo mbadala wako hajapatikana ndiyo maana heri uendelee kuongoza kwa kipindi kingine cha miaka mitano labda baada ya hapo atapatikana mbadala wako.\u00a0<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Baada ya maelezo hayo mapesi kabisa naamini Profesa na Daktari watatoana macho kwa sababu ni hakika kwamba muungano kwa wapinzani ni ndoto na wewe rafiki yangu Rais Kikwete unajua.\u00a0<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Hivyo ukishawamwangia upupu huo wewe utabaki ukipumua taratibu na kuwaacha wao wakishambuliana kwa maneno makali ya kwanini mmoja hataki kumuunga mkono mwingine hata kama amegombea na kushindwa kwa kipindi cha miaka 15 mfululizo. Hilo utakuwa umemaliza. \u00a0<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<table align=\"center\" cellpadding=\"0\" cellspacing=\"0\" class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;text-align:center;\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/5b628-hussein2bbashe.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"320\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/5b628-hussein2bbashe.jpg?resize=239%2C320&#038;ssl=1\" width=\"239\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align:center;\">Hussein Bashe<\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>\u00a0\u00a0\u00a0<\/span><span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Ikitokea likaibuka swala la ubaguzi ambalo naamini litaingizwa kwa mgongo wa kuenguliwa kwa yule kijana wetu Hussien Bashe kwa sababu baadhi ya watu makini hapa nchini wameanzisha tabia nzuri ya kupinga maamuzi ya uonevu yanayotolewa na wakubwa dhidi ya wanyonge ambayo najua wewe haikupendezi ingawa wao wanaonekana hawajali hata kama itawagharimu aidha ajira zao au uraia wao, hapa napo inafaa kueleza ukweli kuwa jina lake lilikatwa kwa sababu hakuwa mwenzetu.<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Kwamba ingawa ili mtu awe huru anapaswa kuwa mkweli, lakini ni muhimu ieleweke kwamba ukweli una mipaka yake ndani ya chama chetu. Tumefundishwa kuishi kikondoo, kukubali kila jambo tunaloambiwa na wakubwa hata kama ni la kipuuzi kupindukia pasipo kuhoji chochote.\u00a0<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Ndani ya\u00a0 chama chetu historia inaonyesha baadhi ya waliosimamia haki na ukweli dhidi ya uonevu na uongo wa wakubwa wamekuwa wakiishia pabaya ingawa watu wa aina hii hawaishi. Jambo linaloshangaza kweli!<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Hivyo suala la Bashe kuvuliwa uraia kibabe na chama chetu kinachotawala kibabe liliamuliwa kibabe ili kumkomesha kutokana na tabia yake ya kusumbua wakubwa.<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Kwamba wewe mwenyekiti ndiye uliyewaambia wakubwa wenzako katika mkutano ule kuwa bwana mdogo Bashe hafai kupitishwa kuwa mgombea ubunge kwa sababu ni msumbufu. Alikusumbua sana, yeye na wenzake kwenye mkutano wa kutatua mgogoro wa umoja wa vijana wa chama tawala huko Iringa.<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Kwa sababu ya usumbufu wake na kwa sababu hakuwa tayari kuimba kale ka wimbo ka zidumu na kuvuma fikra sahihi za mwenyekiti wa chama Tanzania bara na visiwani, ulimchukia kuanzia Iringa hadi Dodoma ulipoongoza kukata jina lake kwa kumsingizia kuwa si raia!\u00a0<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Ni vema watu wakaelewa kuwa mkubwa ni mkubwa, hata akikosea hairuhusiwi kushinda naye bali kukubali hata hayo makosa yake, hivyo Bashe alipaswa kukubali yote ya kipuuzi na yasiyo kuwa ya kipuuzi aliyokuwa akielekezwa na wakubwa.\u00a0<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Sasa alipojifanya kujua kibaya ni kipi na kizuri ni kipi hapo ndipo alipoharibu. Na hiyo ndiyo sababu ya kumnyima nafasi ya kugombea ulaji kwa kisingizio cha uraia.<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Inawezekana pia suala la Salma likaibuka manake waswahili wameshaanza kushapalia matanuzi yake. Kwa mtizamo wangu hapa napo ni rahisi kupangua hoja hii.\u00a0<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<table align=\"center\" cellpadding=\"0\" cellspacing=\"0\" class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;text-align:center;\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/5c6be-salma.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"234\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/5c6be-salma.jpg?resize=320%2C234&#038;ssl=1\" width=\"320\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align:center;\">Salma Kikwete<\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Likiibuka jambo hili ili kuondoa swali lolote la nyongeza, kwanza ni kukanusha maneno yote ya Kinana kuwa Salma analipiwa gharama na chama chetu kwani taarifa zilizopo zinadai kuwepo utata katika hayo malipo yaliyoelezwa na Kinana.<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Halafu ni kuwaelewesha wanaohoji raha za Salma kuwa dunia inabadilika na kila mtawala ana staili yake ya kula nchi. Kama wakubwa wa zamani walikuwa wanawazibia \u2018mawife\u2019 zao kufaidi matunda yao ya ukubwa, kwako haiko hivyo.<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Ni ruksa kwa Salma kujirusha kwa pesa za walalahoi hata kama baadaye atakuja kufikishwa mahakamani kwa kufaidi asivyostahili. Hayo ni matokeo.<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Hapo jambo la kuweka wazi ni kuwa Salma baada ya kuingia Ikulu maisha yake yalibadilika kulingana na hali ya jengo lenyewe. Alibadilika kuanzia mwili, mavazi, usafiri wake na kila kitu.\u00a0<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Hivyo mambo yote ya kuanzisha taasisi hata kama pesa inayopatikana anaibugia yote ni sawa kwani hayo ndiyo matunda ya ukubwa. Majuto yatakuja baadaye na hasa akiingia mpinzani madarakani jambo ambalo si rahisi hata kidogo kwa sababu ambazo ziko wazi kabisa na kila mmoja anazijua. Wakati mwingine ni bora kuweka mambo wazi ili kuondoa vijimaneno maneno.\u00a0<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Na hawa viherehere walio kwenye ofisi za umma wanaomfuata fuata Salma kwenye matembezi yake eti kwenda kumpokea, hao ni kuwakana mapema kwa sababu hawakutumwa na mtu kumfuatafuata bali viherehere vyao na adhabu yao waweza itangaza hapo hapo kuwa katika serikali yako ijayo kama utafanikiwa kushinda uchaguzi, hawatakuwa na kazi kwa sababu kwanza wanamnyima uhuru wa kujitanua.\u00a0<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Jambo lenye utata hapo ni hili la Salma naye kuanza kutoa maagizo kwa wakuu wa mikoa. Hapo sijui utajibuje? Katika hili atakuwa amekuangusha kwa sababu huwezi kusema ulimtuma amuagize yule jamaa hivyo alivyomuagiza, nadhani inabidi kumrekebisha kidogo. Ale tu raha za wavuja jasho la damu lakini asiingilie kazi zako.<\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Mambo ya kipuuzi kwenye mdahalo, eti nyumba ndogo ziko!? Na upuuzi mwingine hayatakuwa na nafasi, hilo naomba ulielewe mapema na lisikunyime usingizi. Atayeibuka nayo huyo hatutamsikiliza na tutamuweka katika kundi la wapuuzi. <\/span><span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height:normal;\"><span>Ikiwa hivi, kwa namna yoyote mdahalo utakuwa mzuri sana kwa upande wako. Ni juu yako kutafakari na kuchukua hatua. <\/span><span><\/span><\/div>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Jakaya Kikwete RAFIKI yangu Rais Jakaya Kikwete amekumbwa na woga mkuu kiasi kwamba sasa anajiogopa hata yeye mwenyewe. Anaogopa kufanya mambo yaliyo ndani ya uwezo wake. Hali hii si nzuri, tunapaswa kumsaidia kuondoka nayo. Kwa pamoja tunapaswa kumtia moyo. Tukimuacha, ataendelea kuogopa kwa kipindi kirefu. Atakuwa anaogopa kukutana na mimi rafiki yake, kisa, kiherehere changu [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":false,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[1],"tags":[33],"coauthors":[],"class_list":{"0":"post-1999","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","6":"category-uncategorized","7":"tag-mchokonozi"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/1999","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=1999"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/1999\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=1999"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=1999"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=1999"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=1999"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}