{"id":1990,"date":"2017-09-02T13:33:00","date_gmt":"2017-09-02T13:33:00","guid":{"rendered":"https:\/\/msangirstz8.wordpress.com\/2017\/09\/02\/kwa-sababu-ya-uchaguzi-2010-mungu-atujalie-mateso-na-kilio\/"},"modified":"2017-09-02T13:33:00","modified_gmt":"2017-09-02T13:33:00","slug":"kwa-sababu-ya-uchaguzi-2010-mungu-atujalie-mateso-na-kilio","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=1990","title":{"rendered":"KWA SABABU YA UCHAGUZI 2010 MUNGU ATUJALIE MATESO NA KILIO"},"content":{"rendered":"<p><!--[if gte mso 9]&gt;   Normal  0          false  false  false    EN-US  X-NONE  X-NONE                                       MicrosoftInternetExplorer4                                     &lt;![endif]--><br \/><!--[if gte mso 9]&gt;                                                                                                                                                                                                                                                                                    &lt;![endif]--><!--[if gte mso 10]&gt; \/* Style Definitions *\/  table.MsoNormalTable  {mso-style-name:\"Table Normal\";  mso-tstyle-rowband-size:0;  mso-tstyle-colband-size:0;  mso-style-noshow:yes;  mso-style-priority:99;  mso-style-qformat:yes;  mso-style-parent:\"\";  mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;  mso-para-margin-top:0in;  mso-para-margin-right:0in;  mso-para-margin-bottom:10.0pt;  mso-para-margin-left:0in;  line-height:115%;  mso-pagination:widow-orphan;  font-size:11.0pt;  font-family:\"Calibri\",\"sans-serif\";  mso-ascii-font-family:Calibri;  mso-ascii-theme-font:minor-latin;  mso-fareast-font-family:\"Times New Roman\";  mso-fareast-theme-font:minor-fareast;  mso-hansi-font-family:Calibri;  mso-hansi-theme-font:minor-latin;  mso-bidi-font-family:\"Times New Roman\";  mso-bidi-theme-font:minor-bidi;} &lt;![endif]--> <\/p>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"separator\" style=\"clear:both;text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/65606-masikini.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:1em;margin-right:1em;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"180\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/65606-masikini.jpg?resize=320%2C180&#038;ssl=1\" width=\"320\" \/><\/a><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>YAPATA miezi nane sasa tangu nilipowaonya wapiga kura wa Tanzania waliokuwa wakifurahia kupewa ubwabwa na maharage, khanga, tisheti na kofia wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu ili wawachague waliokuwa wakiwahonga kuwa si muda mrefu watakuwa wakinung\u2019unika, wakilia na hata <span class=\"yshortcuts\"><span>kufa<\/span><\/span> kwa makosa yao wenyewe ya kutumia kura zao vibaya kwa kuchagua bora viongozi badala ya viongozi bora.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><br \/>Katika makala ile niliandika kufafanua <span class=\"yshortcuts\"><span>yale<\/span><\/span> ambayo nilikuwa nikiyaandika katika mfululizo wa makala zangu za maswali elfu lela na moja kwa rafiki yangu Rais Jakaya Kikwete.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Ingawa niliandika kwa lugha nyepesi mno kueleweka ajabu alifeli yote kwa ujumla wake kwa sababu hakujibu hata moja.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><br \/>Kama nilivyoandika miezi hiyo nane iliyopita, leo, ambapo watanzana wengi wapo katika mateso makali yanayosababishwa na ugumu wa maisha ninaandika tena maneno mapesi kabisa huku nikiepuka kugusia mambo mazito yanayoumiza mioyo kuwakumbusha wapiga kura wa <span class=\"yshortcuts\"><span>Tanzania<\/span><\/span> kuwa mateso watakayokutana nayo sasa wanayastahili kwa sababu ya uzuzu wao.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><br \/>Tukubali au tukatae, w<span class=\"yshortcuts\"><span>atanzania wana <\/span><\/span>kila sababu ya kuishi maisha magumu kwa sababu walikubali kuyauza maisha bora waliyokuwa wakiyachungulia kwa thamani ya ubwabwa na mahagare, khanga, tisheti, kofia na wakati mwingine kwa sh 5,000 au 10,000 baada ya kufanya kazi kubwa ya kuimba kwa sauti kubwa nyimbo za masifu kwa chama kinachowatesa sasa.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"separator\" style=\"clear:both;text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/a6d16-khanga2bccm.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:1em;margin-right:1em;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" decoding=\"async\" border=\"0\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/a6d16-khanga2bccm.jpg?w=696&#038;ssl=1\" \/><\/a><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><br \/>Ni wapiga kura hawa wanaolia kutokana na ugumu wa maisha ndiyo waliokuwa wakichukua shoka na mapanga kwenda kuwashambulia wenzao waliokuwa wakitaka kuking\u2019oa mamdarakani chama kinachowatesa sasa kutokana na kukosa sifa zinazostahili za kuendelea kuiongoza nchi yetu. Wapuuzi wao na machozi yao.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><br \/>Wamesahau kuwa kwa makusudi licha ya makala nyingi za upendo na zilizojaa maonyo nilizokuwa nikiwaandikia kuhusu kutokufanya kosa la kuchagua bora viongozi walinipuuza. Wakawachagua. Walifanya kosa la kukataa kuyakimbilia maisha yenye matumaini, sasa wanajuta. <\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Nami kwa nafsi nyeupe kabisa namsihi mwenyezi azidi kuwapa maisha magumu yenye kulia na kusaga meno.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><br \/>Namuomba mwenyezi mungu anisamehe kwa kuwaombea maisha magumu na yenye kila aina ya suluba ndugu zangu ninaokula na kunywa nao kwa jasho la damu. Ninafanya hivi kwa sababu ninaamini ndiyo njia pekee ya kuwafundisha kufikiri sawasawa.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><span>\u00a0<\/span><br \/>Ninaamini kuwa watakapokuwa wanakufa kwa kukosa huduma ya vidonge vya kutibu maralia katika hospitali zetu za umma huku hao waliowapa kura kwa kughilibiwa na vipande vya khanga na wali na maharage wakienda kutumbuliwa vipele Ujerumani na <span class=\"yshortcuts\"><span>Amerika<\/span><\/span>, ndipo watapojifunza maana ya kutumia kura zao vizuri kwa kukataa kurubuniwa kijinga.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><br \/>Ni jambo la ajabu kwa watu walioishi chini ya mfumo wa uongozi wa chama kinachowatesa kwa takribani miaka 50 sasa, wanaojua jinsi chama hicho kilivyochoka na kinavyobaka demokrasia kuendelea kukikumbatia kwa kudanganywa kipuuzi kuwa, eti! Bila chama hicho Tanzania haitakalika.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><br \/>Kwa watu wanaofikiri sawasawa ni jambo lisiloingia akili kukiingiza madarakani chama ambacho <span class=\"yshortcuts\"><span>kina<\/span><\/span>lundo la watu wasiokuwa na sifa za uongozi lakini wanaong\u2019ang\u2019ania madarakani kwa gharama kubwa ya fedha za umma. <\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Watu hawa, hata walipojifanya wamesahau walikumbushwa kwa lugha nyepesi kuwa ili kuifikia Tanzania yenye neema tunahitaji mabadiliko ya uongozi lakini ajabu waliziba pamba masikioni.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><br \/>Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi wenye akili ambao walikuwa wakifuatilia mwenendo wa kampeni na hata uchaguzi wetu, wapiga kura wa Tanzania waliyakataa maisha bora wakachagua maisha magumu. <\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Leo hata kabla maisha hayajawakamata sawa sawa wameanza kupiga kelele za maisha magumu. Naiomba serikali isiwasikilize, izidi kuwahimiza wafunge mikanda kabla ya baa la njaa la kujitakia halijafika. Waanze sasa kuzoea maisha yenye ukakasi usiovumilika.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><br \/>Ni watanzania wenzangu ambao wengi ninaishi nao huku uswahilini waliowabeza watumishi waliokuwa wakiomba kututumikia ili kwamba kutokana na utumishi wao kwa taifa letu, siku moja watoto wetu waweze kusoma bure.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><span>\u00a0<\/span><br \/>Leo ninapowatizama, wakiwa wanahimizwa na serikali iwakopeshe hela za kuchapishia mitihani na ripoti za mitihani ya watoto wao, nawaona wana sura za majuto. <\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Wanasononeshwa na serikali waliyoichagua wenyewe miezi michche iliyopita kuishiwa hela za kusomeshea watoto wao na kubakiza hela za posho za semina, kuketi bungeni na chai na vitafunwa kwa wakubwa wanapotembelewa na wakubwa wenzao wenye maisha bora.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Kwa yeyote asiyesadiki maandishi haya, aje huku uswahili kwa wachokonozi asikilize wanavyolia kwa uchungu kutokana na kupanda kwa bei ya umeme ambao haupatikani.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"separator\" style=\"clear:both;text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/64d7c-kandili.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:1em;margin-right:1em;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" decoding=\"async\" border=\"0\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/64d7c-kandili.jpg?w=696&#038;ssl=1\" \/><\/a><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Wapo ambao wameshaanza kununua vibatari kwa sababu kulingana na kipato chao hawataweza kumudu gharama za umeme. Wameamua kurudi kuishi maisha ya enzi za ujima katika karne hii ya 21 ya sayansi na teknolojia, tena wakiwa wanakaribia kabisa kuazimisha miaka 50 ya uhuru wao.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Katika hali halisi ya maisha ya mtanzania kwa sasa, pambio la maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekana ni upuuzi na linatia hasira. Lakini acha kibwagizo chake kiendelee kujirudia masikioni mwa watanzania ili kiwaongoze katika majuto ya kweli.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><span>\u00a0<\/span><br \/>Kilio kiko kila mahali kwani hata kwa wale wenye uwezo wa kujikamua na kulipa gharama za umeme, umekuwa lulu, unapatikana kwa mgawo na\u00a0katika sehemu nyingi za uswahili unapatikana usiku.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><br \/>Mchana shughuli zote zinalala, watu wanashinda wanapiga soga nje ya ofisi zao. Matumaini ya kutekelezwa kwa ahadi lukuki za kusambaza umeme sehemu mbalimbali nchini yameyeyuka, yamebaki majuto ya kukosekana kwa umeme na ukali wa mgawo wa umeme. <\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><br \/>Majuto haya yanastahili kutokea kwa watu wanaojuta kwa makosa yao ya kuendekeza uroho wa ubwabwa na maharage na kutelekeza haki yao ya msingi ya kutochagua majuto.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><br \/>\u00a0<\/span><\/span><\/div>\n<table align=\"center\" cellpadding=\"0\" cellspacing=\"0\" class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;text-align:center;\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/2efc1-william-ngeleja.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"320\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/2efc1-william-ngeleja.jpg?resize=213%2C320&#038;ssl=1\" width=\"213\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align:center;\">Ngelleja<\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Ninapotafakari sana nikiwa <span class=\"yshortcuts\"><span>katikati<\/span><\/span> ya lundo la watanzania maskini wanaolizwa na kauli ya William Ngeleja, waziri kijana wa Wizara ya Nishati na Madini, ambaye siku chache baada ya kuteuliwa aliwaambia watanzania kuwa tatizo la umeme limefikia kikomo, ninaziona mbongo dhaifu za wazee na watu kadhaa wa umri wa makamo zisizokuwa na uwezo wa kifikiri kama walionao vijana wa sasa.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><br \/>Katikati ya lundo hili la maskini wa kitanzania walio katika majuto baada ya kuyatelekeza matumaini, wanaolia wengi ni wazee na watu wa rika linalokimbilia uzeeni. Wanalalamika kuwa walidanganywa kuwa mambo yatakuwa mazuri baada ya uchaguzi na wakapewa mifano ya jinsi vigogo kadhaa walivyofikishwa mahakamani kwa tuhuma mbalimbali za ulafi.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><br \/>Kutoka huko kwa vigogo wanaokabiliwa na tuhuma za ulafi wakageuzwa upande wa pili na kuonyeshwa sinema kadhaa za bunge zilivyokuwa zikichezwa.\u00a0<\/span><\/span><\/div>\n<table align=\"center\" cellpadding=\"0\" cellspacing=\"0\" class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;text-align:center;\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/e0617-rambo.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" decoding=\"async\" border=\"0\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/e0617-rambo.jpg?w=696&#038;ssl=1\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align:center;\">Rambo<\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Wakaonyeshwa tamthilia \u2018feki\u2019 ya Dowans ambayo waigizaji wake wakuu sasa wanafahamika dunia kote kwa umaarufu walionao kama wanavyofahamika akina na Rambo na Van Damme na wakati wakiangalia tamthilia hizo hawakukosa viburudisho vya khanga, fulana, kofia na ubwabwa na maharage vilivyoiharibu kabisa akili yao.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><\/span><\/span><\/div>\n<table align=\"center\" cellpadding=\"0\" cellspacing=\"0\" class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;text-align:center;\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/546e3-damme.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" decoding=\"async\" border=\"0\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/546e3-damme.jpg?w=696&#038;ssl=1\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align:center;\">Van Damme<\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><br \/>Siku chache baada ya wapigakura kulipa fadhila kwa waliokuwa wakiwahonga khanga hizo kwa kuwapigia kura ya ndiyo, tamthilia ya kweli ya Dowans imeingia Tanzania, hii inaonyesha jinsi watanzania watakavyokamuliwa jasho <span class=\"yshortcuts\"><span>lao<\/span><\/span>kulilipa dude tulilosadikishwa na serikali kuwa ni \u2018zimwi.\u2019<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><br \/>Na ukitaka kujua mbivu na mbichi za chama cha maulaji angali tamthilia hizi mbili za Dowans, hii iliyochezwa bungeni na iliyochezwa kwenye mahakama ya kimataifa huko kwa wenzetu walioendelea. <\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Ukitazama vizuri picha hizo ndiyo utajua kuwa bila kukiondoa chama cha maulaji madarakani, chama ambacho watu walioanza kuchoka kiumri wanaking\u2019ang\u2019ania sana, Tanzania italiwa na itakwisha.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><br \/>Zinajieleza vizuri tu, ukiangalia waigizaji wetu wa hapa nyumbani waliokwenda kuisaka Dowans ughaibuni wanaeleza kuwa ni zimwi lisiloonekana hivyo hakuna haja ya kuendelea na mkataka nalo ikizingatiwa kwamba liliingia nchini na kuanza kufanya shughuli zake kinyemela. <\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><br \/>Tena katika kunogesha igizo lao wakaenda mbali kiasi cha kumtisha mkuu wa kaya kuwa yakiyafumua yote waliyoyabaini kuhusu zimwi <span class=\"yshortcuts\"><span>hilo<\/span><\/span> <span class=\"yshortcuts\"><span>basi<\/span><\/span>serikali yake yote yaani na yeye akiwemo itaanguka, lakini kwa sababu wanampenda sana mengine yanayaficha. <\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Huko kwa wenzetu Dowans imethibitika kuwa ipo, sio zimwi, imekwenda mahakamani imeshinda kesi na sasa tunalazimika kuilipa. Matumaini tuliyopewa yameyeyuka, tunajuta kwa kuiamini tamthilia ya waigizaji wetu wa hapa bongo.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><br \/>Ni lazima tulipe bila kujali kama tutashinda na njaa, tutakufa kwa kukosa fedha za kununulia dawa kutokana na makali ya kulipa deni hilo au tutashindwa hata kununua chaki za kufundishia watoto wetu huku uswahilini. Serikali na chama kinachotutawala ndiyo msimamo wao.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Jambo la msingi ambalo wapiga kura wa Tanzania wanapaswa kulifahamu ni kwamba hivi sasa wanalazimika kuishi maishi magumu kwa sababu chama chetu kiko katika mchakato wa kufidia kama sio kurejesha mabilioni ya fedha kiliyoyatumia kuwahonga wao ili wakichague. <\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Ni lazima wengi wetu tule mlo mmoja kwa siku au tulale na njaa kwa sababu tuna deni la kulipia gharama za mabango ya picha za mgombea urais wetu yaliyokuwa yamesambazwa nchi nzima wakati wa kampeni zake za kurejea madarakani.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Sote tunajua kuwa gharama hizi zilikuwa za lazima ili kumuwezesha kushinda na tunaopaswa kuzilipa ni sisi, hivyo asitokee wa kulalamika kwa sababu kinachotekea sasa binafsi niliwahi kuwadokeza Watanzania.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><br \/>Kama <span class=\"yshortcuts\"><span>kuna<\/span><\/span>mtu asiyejua hilo nikumbushe kuwa niliwahi kuhoji hivi; \u2018rais aliyechaguliwa kwa kura nyingi na kukaa madarakani kwa miaka mitano, inakuwaje anahangaika kutumia mabilioni ya fedha ili kuwashawishi wapiga kura wamchague?<\/p>\n<p><\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>\u2018Fedha hizi wangepewa akina Nicholaus Mgaya si wangepunguza kupiga miayo ya njaa na kutishia kugoma kufanya kazi? Matumizi haya ya CCM kumnadi mgombea wao\u00a0 kwa nchi maskini kama hii ambayo ina watu wanaoishi chini ya dola moja kwa siku sio ufisadi?\u2019<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><br \/>Sasa ili haya yaweze kuthibitika, mwenendo wa maisha yetu ya kila siku utatuongoza kufika huko kwa kuyafuta matumaini ya maisha bora na kubaki tukijuta kwa kujikosesha kwa makusudi maisha bora katika kipindi cha miaka mitano ijayo.<\/p>\n<p><\/span><\/span><\/div>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>YAPATA miezi nane sasa tangu nilipowaonya wapiga kura wa Tanzania waliokuwa wakifurahia kupewa ubwabwa na maharage, khanga, tisheti na kofia wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu ili wawachague waliokuwa wakiwahonga kuwa si muda mrefu watakuwa wakinung\u2019unika, wakilia na hata kufa kwa makosa yao wenyewe ya kutumia kura zao vibaya kwa kuchagua bora viongozi badala ya [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":false,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[1],"tags":[33],"coauthors":[],"class_list":{"0":"post-1990","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","6":"category-uncategorized","7":"tag-mchokonozi"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/1990","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=1990"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/1990\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=1990"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=1990"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=1990"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=1990"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}