{"id":1530,"date":"2017-08-24T17:57:00","date_gmt":"2017-08-24T17:57:00","guid":{"rendered":"https:\/\/msangirstz8.wordpress.com\/2017\/08\/24\/serikali-ilivyoibiwa-tanzanite-mkononi\/"},"modified":"2017-08-24T17:57:00","modified_gmt":"2017-08-24T17:57:00","slug":"serikali-ilivyoibiwa-tanzanite-mkononi","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=1530","title":{"rendered":"SERIKALI ILIVYOIBIWA TANZANITE MKONONI"},"content":{"rendered":"<p><!--[if gte mso 9]&gt;   Normal  0          false  false  false    EN-US  X-NONE  X-NONE                                       MicrosoftInternetExplorer4                                     &lt;![endif]--><br \/><!--[if gte mso 9]&gt;                                                                                                                                                                                                                                                                                    &lt;![endif]--><!--[if gte mso 10]&gt; \/* Style Definitions *\/  table.MsoNormalTable  {mso-style-name:\"Table Normal\";  mso-tstyle-rowband-size:0;  mso-tstyle-colband-size:0;  mso-style-noshow:yes;  mso-style-priority:99;  mso-style-qformat:yes;  mso-style-parent:\"\";  mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;  mso-para-margin-top:0in;  mso-para-margin-right:0in;  mso-para-margin-bottom:10.0pt;  mso-para-margin-left:0in;  line-height:115%;  mso-pagination:widow-orphan;  font-size:11.0pt;  font-family:\"Calibri\",\"sans-serif\";  mso-ascii-font-family:Calibri;  mso-ascii-theme-font:minor-latin;  mso-fareast-font-family:\"Times New Roman\";  mso-fareast-theme-font:minor-fareast;  mso-hansi-font-family:Calibri;  mso-hansi-theme-font:minor-latin;  mso-bidi-font-family:\"Times New Roman\";  mso-bidi-theme-font:minor-bidi;} &lt;![endif]--> <\/p>\n<div class=\"separator\" style=\"clear:both;text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/4d687-fazal2b3.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:1em;margin-right:1em;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"240\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/4d687-fazal2b3.jpg?resize=320%2C240&#038;ssl=1\" width=\"320\" \/><\/a><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Na Mwandishi Wetu<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>MAOFISA wa Serikali waliokuwa katika chumba cha kuchenjulia madini cha mgodi wa <\/span><span>TanzaniteOne, uliopo Mererani mkoani Manyara<\/span><span> Juni 20, 2017, wanadaiwa kuhadaiwa na mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya <\/span><span>Sky Associates Limited na kuibiwa ndoo iliyokuwa imejaa madini ya tanzanite.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Mkurugenzi wa kampuni hiyo anayetajwa kuwahadaa maofisa hao ambao majina na nyadhifa zao tunayahifadhi kwa sasa, ni Faisal Juma Shahbhai.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Kwamba Shahbhai akiwa na wakurugenzi wenzake na maofisa wa Serikali kabla ya kuanza ukaguzi wa ndoo sita za madini katika chumba cha ukaguzi wa madini cha mgodi wa TanzaniteOne, alitoa jiwe kubwa linalodhaniwa kuwa madini na kulionyesha.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Imeelezwa kuwa jiwe hilo liliwaduwaza maofisa wa Serikali ambao walibaki kulikodolea macho na wakiwa katika hali hiyo, ndoo inayodaiwa kujaa tanzanite ilivutwa na mmoja wa washirika wa Shahbhai na kufichwa.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"separator\" style=\"clear:both;text-align:center;\"><span style=\"font-size:small;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/449cf-tanzaniteone2bpix2b2.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:1em;margin-right:1em;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"161\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/449cf-tanzaniteone2bpix2b2.jpg?resize=320%2C161&#038;ssl=1\" width=\"320\" \/><\/a><\/span><\/div>\n<p><\/p>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Taarifa za Shahbhai kuwaduwaza maofisa hao ili kuwawezesha washirika wake kukwapua kiasi kikubwa cha madini hayo, zimepatikana ndani ya mgodi wa TanzaniteOne ambao ni mmoja wa wakurugenzi wake.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Kwa mujibu wa taarifa hizo, mkakati wa kuibwa kwa ndoo hiyo ya madini uliratibiwa Juni 20, mwaka huu kabla ya kutekelezwa Juni 21. Mbali na Shahbhai, wakugerenzi wengine wa kampuni hiyo ya Sky waliokuwa ndani ya chumba cha ukaguzi ni Hussein Gonga na Rizwan Ullah.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Mmoja wa watoa taarifa kutoka ndani ya mgodi huo, ambaye amefanya mahojiano na Mikito Blog kwa sharti la jina lake kuhifadhiwa, alisema: <\/span><span>\u201cHiyo story ni ya kweli. Kinachozungumzwa ni kweli.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>\u201cLakini kuna mambo ambayo yanaendelea sasa hivi ya kiserikali na sisi ambao tunalifahamu hilo suala vizuri, tungependa tuiachie Serikali kwanza imalize uchunguzi wake kwa sababu kuna kasoro nyingi zimekwishatokea kuhusu hiyo kampuni kipindi cha nyuma, lakini nyingi zimekuwa zikiishia njiani.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>\u201cKama unavyoona, hii ilivyotokea wakaitwa waandishi wa habari, hatujui walipewa nini wakaenda wakakanusha wao hao hao ambao walisema hiyo kitu ni kweli.\u00a0<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>\u201cSasa tumeona ili hizi longo longo zisiendelee, tuiachie Serikali ikamilishe uchunguzi wake, baada ya hapo sisi tutaendelea kuongea kilichotokea kwa usalama wetu na kuhahakisha kuwa hili jambo linafika mwisho.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>\u201cKwa sababu hawa jamaa wanafuatilia sana magazeti, kila kinachotoka kwenye magazeti wanakuwa hatua moja mbele, wanajua wafanye nini, wanajua waende wakazuie wapi.\u201d<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Alipoulizwa jinsi tukio hilo lilivyotokea, huku akikataa kueleza kinaga ubaga, alisema: \u201cNinaweza nikakupa \u2018hint\u2019, lakini siwezi kukueleza mambo mengi kwenye simu kwa sababu za kiusalama na hii simu inafuatiliwa kwa sababu mimi ninahusika kwa kiasi fulani na hilo tukio.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>\u201cHao jamaa ni kweli walifanya hilo tukio. Ilikuwa ni tarehe 20 na tarehe 21 ndiyo waliweza kutoa huo mzigo. Sasa kuna vipande vya \u2018footage\u2019 vimesambaa hapa mjini vikionyesha namna mpango huo ulivyotekelezwa, lakini pia wapo ambao wana \u2018footage\u2019 zinazoonyesha tukio zima kuanzia tarehe 20 wakijiandaa kufanya hilo tukio, tarehe 21 mzigo ule ukitolewa \u2018ghalani\u2019 na kuingizwa kwenye gari pamoja na yule mhusika aliyebeba lile dumu, mhindi aliyehusika mpaka gari linatoka nje ya kampuni.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>\u201cKwenye \u2018footage\u2019 wahusika wote wanaonekana, anaonekana Faisal, anaonekana Gonga na <\/span><span>Rizwan,<\/span><span> wote walikuwa wamekaa kwenye meza, wanaonekana.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>\u201cWakurugenzi wa kampuni wanaruhusiwa kuingia kwenye chumba cha kuchenjulia madini. Wanaingia wakati mzigo unapokatwa utepe ukitoka mgodini kuangalia kilichopo ndani kabla ya kutoa ruhusa uanze kufanyiwa usafi na taratibu zote ikiwa ni pamoja na kuupanga.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>\u201cKatika tukio hili wafanyakazi pia wanahusika, wakiwemo walinzi kwa sababu wapo ambao wamekuwa wakieleza jinsi mchezo mzima ulivyofanyika.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>\u201cJinsi madini hayo yalivyoibwa ni kwamba wale wakurugenzi walikuwa wamekaa kwenye meza pamoja na wale watu wa Serikali. Sasa kabla ya kuanza kukagua zile ndoo, <\/span><span>Shahbhai<\/span><span> alitoa jiwe fulani akawaonyesha wale watu wa Serikali ambao walianza kuliangalia kwa mshangao.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>\u201cHuku nyuma maofisa wale walipokuwa wakishangaa jiwe lile, mhindi mmoja aliyekuwa mle ndani, alilivuta lile dumu kwa chini chini akampatia mwenzake kwa nyuma akalipeleka chumba kingine wakati wale maofisa wa Serikali wakiendelea kushangaa jiwe walilokuwa wakionyeshwa na <\/span><span>Shahbhai<\/span><span>.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>\u201cHivyo watu wa Serikali hawakuona jinsi lile dumu lilivyotoroshwa na lilivyotolewa likapelekwa hadi kwenye chumba cha pili na yule mhindi akaenda kulifungia huko, ndiyo wakarudi wakaendelea na shughuli nyingine kama kawaida.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>\u201cHaya yote kwenye \u2018footage\u2019 yanaonekana na mtu yeyote akiiona hata kama hajui masuala ya wizi, atajua ni namna gani mchezo ulivyochezwa.\u201d <\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><b><span>Arafat<\/span><\/b><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Mdogo wake <\/span><span>Shahbhai<\/span><span> ambaye katika mahojiano na Mikito Blog alijitambulisha kwa jina la Arafat, alipoulizwa kuhusu tukio hilo baada ya jina lake kutajwa, alikana kuhusika kwa kueleza kuwa siku inayodaiwa wizi huo kufanyika yeye alikuwa mgonjwa.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span><span>\u00a0<\/span>\u201cMimi siku ya tukio inayosemwa nilikuwa naumwa, ni kweli nilitoka mgodini, lakini sikuwa eneo la tukio. Hapa kuna maneno mengi sana na fitina nyingi sana.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>\u201cSiku ambayo tukio linadaiwa kutokea ilikuwa mwezi wa Ramadhani, mimi nilikuwa nimefunga. Nina matatizo ya kifua na nilikuwa nimefunga. Nilitoka asubuhi nikaenda nikachukua dawa nikarudi nyumbani, lakini usiku tena nikabanwa nikaenda tena kuchukua dawa.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>\u201cNilitoka kwenye saa tatu asubuhi nikaenda nikachukua dawa yangu nikarudi, usiku tena baada ya kufuturu tu nikashindwa tena kupumua nikaenda zangu mjini kuchukua dawa.\u00a0<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>\u201cSikuwa kwenye chumba cha kuchenjulia kabisa na huyo Yusuf (Mhagama) wanayesema nilikuwa naye mimi sikuwa naye.\u201d<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Akiendelea kujitetea, alisema kuwa huenda taarifa hizo zimezushwa kutokana na ukali wake katika kusimamia ulinzi.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>\u201cNiko upande wa ulinzi na tunabana watu na ukweli watu hapa hawanipendi kwa sababu tuko wakali.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>\u201cTaratibu zinaturuhusu kuingia mgodini, lakini kwenye chumba cha kuchenjulia madini mimi huwa siingii. Kazi yangu ni kuhakikisha usalama kuanzia mgodini hadi kwenye chumba cha kuchenjulia madini.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>\u201cMimi mwenyewe sipendi kuingia kwenye chumba cha kuchenjulia lakini ninaruhusiwa ila sijaenda kwa muda wa miezi kama minne hivi,\u201d alisema Arafat.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Wakati Arafat akieleza hayo, mtoa taarifa mwingine kutoka ndani ya mgodi wa TanzaniteOne ameieleza Mikito Blog kuwa siku ya tukio Arafat alikuwa mgodini akisimamia mitambo ya ulinzi na baada ya gari lililokuwa na ndoo ya tanzanite iliyoibwa kutolewa ndani ya eneo la mgodi, ndipo akaondoka kwenye eneo alilolitaja kuwa ni \u2018control room.\u2019<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><span>Arafat alipoulizwa kama baada ya tukio hilo alisafiri kwenda Nairobi, Kenya kama tetesi zilivyosambaa katika Jiji la Arusha, Arafat aliruka kimanga kwa kueleza kuwa hajasafiri kwenda nchini huko.<\/span><\/span><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:small;\"><b><span>Shahbhai<\/span><\/b><b><span><\/span><\/b><\/span><\/div>\n<p><span style=\"font-size:small;\"><span>Tayari Shahbhai anayedaiwa kuwahadaa maofisa wa Serikali amekwishaeleza kuwa ni kweli yeye pamoja na wakurugenzi wanzake, Gonga na <\/span><span>Rizwan walikuwa katika chumba cha kuchenjulia madini siku inayodaiwa kutokea kwa wizi huo.<\/span><\/span><\/p>\n<div class=\"separator\" style=\"clear:both;text-align:center;\"><span style=\"font-size:small;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/cf79d-husein2bgonga.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:1em;margin-right:1em;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"320\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/cf79d-husein2bgonga.jpg?resize=280%2C320&#038;ssl=1\" width=\"280\" \/><\/a><\/span><\/div>\n<p>  <span style=\"font-size:small;\"><span>Shahbhai ambaye alikuwa wa kwanza kuzungumzia suala hilo, pamoja na mambo mengine alisema: \u201c<\/span><span>Hiyo ndiyo kazi yetu sisi, mimi kuwa maeneo hayo au kuwa na madini ni sawa kabisa, kati ya tarehe 19 au 20 ni kweli nilikuwa kwenye shughuli ya uchenjuaji wa madini. Kuwa katika maeneo yangu ya kazi ya kuchenjua madini si jambo la ajabu kwangu kwa sababu ndiyo shughuli zangu.<\/span><\/span><\/p>\n<p>  <span style=\"font-size:small;\"><span>\u201cNi kweli Arafat ni mdogo wangu wa damu, kuna mambo mengi ya msingi yanayoweza kujenga taifa ya kuandika huku Mirerani badala ya haya ya uongo uongo.<\/span><\/span><\/p>\n<p>  <span style=\"font-size:small;\"><span>\u201cYaani gari iende ibadilishwe huko iweje sasa, kwa nini mtu hata kama anataka kitu asiende na gari hiyo hiyo? Watanzania hawajui kitu, hawajui kabisa biashara ya tanzanite, wako \u2018very blind\u2019 kwenye biashara hiyo.<\/span><\/span><\/p>\n<p>  <span style=\"font-size:small;\"><span>\u201cTunapowaambia vitu, tuwaambie ambavyo kesho hata mwenyezi Mungu akisimama tuweze kusimama kujibu kwamba Mola nilichokisema kiko sawa. Yupo mwandishi alikuja Mirerani kufuatilia suala hili na alikaa hapa kwa muda wa siku tatu, lakini nilimshauri aandike vitu ambavyo vitasaidia jamii ya Watanzania.<\/span><\/span><\/p>\n<p>  <span style=\"font-size:small;\"><span>\u201cNi jambo jema kama waandishi wa habari watakuwa wanawajuza watu vitu ambavyo vitajenga uchumi wa taifa kwa sababu hizo taarifa hazijakaa vizuri sana. Katika biashara hii tuna tofauti kubwa na wafanyabiashara wenzetu.\u00a0<\/span><\/span><\/p>\n<p>  <span style=\"font-size:small;\"><span>\u201cBaada ya kuingia kwenye uwekezaji wa biashara ya tanzanite, tumekuwa na ugomvi mkubwa na wachimbaji wadogo kwa sababu maeneo mengi wanayochimba walikuwa wanachimba upande wetu. Nakuhakikishia jambo hilo si la kweli, ni fitina tu.\u201d<\/span><\/span><\/p>\n<p>  <span style=\"font-size:small;\"><span>Vigogo wa Kampuni ya Sky Associates Limited wanadaiwa kuhusika na utoroshaji wa madini ya tanzanite yenye thamani ya mabilioni ya shilingi kutoka katika mgodi wa TanzaniteOne uliopo Mererani mkoani Manyara.<\/span><\/span><\/p>\n<p>  <span style=\"font-size:small;\"><span>Kwamba Shahbhai na wenzake walitekeleza mpango huo Juni 21 kwa kuyasafirisha madini hayo kwa kutumia gari aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili T 710 BWT ambalo ni mali ya Kampuni ya TanzaniteOne, lililokuwa likiendeshwa na Yusuf Mhagama ambaye ni mfanyakazi wa kampuni hiyo.<\/span><\/span><\/p>\n<p>  <span style=\"font-size:small;\"><span>Taarifa zilinai kuwa Mhagama ambaye alikuwa ameambatana na Arafat katika safari hiyo, waliyashusha madini hayo kabla ya kufika Arusha mjini na kuyapakia kwenye gari jingine aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili T 492 BSS.<\/span><\/span><\/p>\n<p>  <span style=\"font-size:small;\"><b><span>Mikito Blog inaendelea na uchunguzi wa sakata hili.<\/span><\/b><\/span><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Na Mwandishi Wetu MAOFISA wa Serikali waliokuwa katika chumba cha kuchenjulia madini cha mgodi wa TanzaniteOne, uliopo Mererani mkoani Manyara Juni 20, 2017, wanadaiwa kuhadaiwa na mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Sky Associates Limited na kuibiwa ndoo iliyokuwa imejaa madini ya tanzanite. Mkurugenzi wa kampuni hiyo anayetajwa kuwahadaa maofisa hao ambao majina na nyadhifa [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":false,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[1],"tags":[34],"coauthors":[],"class_list":{"0":"post-1530","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","6":"category-uncategorized","7":"tag-habari"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/1530","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=1530"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/1530\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=1530"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=1530"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=1530"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=1530"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}