{"id":1500,"date":"2017-08-26T15:16:00","date_gmt":"2017-08-26T15:16:00","guid":{"rendered":"https:\/\/msangirstz8.wordpress.com\/2017\/08\/26\/ndani-giza-nje-mimba\/"},"modified":"2017-08-26T15:16:00","modified_gmt":"2017-08-26T15:16:00","slug":"ndani-giza-nje-mimba-2","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=1500","title":{"rendered":"NDANI GIZA NJE MIMBA"},"content":{"rendered":"<p><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><span><span style=\"font-size:x-small;\"><\/span><\/span><\/p>\n<div class=\"separator\" style=\"clear:both;text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/13790-mimba.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:1em;margin-right:1em;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"213\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/13790-mimba.jpg?resize=320%2C213&#038;ssl=1\" width=\"320\" \/><\/a><\/div>\n<p><span><span style=\"font-size:x-small;\"><\/span><\/span><br \/><span><span style=\"font-size:x-small;\"><\/span><\/span><br \/><span><span style=\"font-size:x-small;\">Na Simba Gembagu Ng\u2019wana Njamiti <\/span><\/span><br \/><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><\/p>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"margin:0 0 10pt;\"><span><span style=\"font-size:x-small;\">Kila nikikita ninakitwa. Popote ninapokita napokewa na mikito. Napokewa na mikito halisi ya kitanzania inayonikita.<\/span><\/span><\/div>\n<p><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><span><span style=\"font-size:x-small;\">Ninakita ili nijikite lakini sijikiti badala yake ninakitwa. Ninatafuta pa kukita ili nipate pa kujikita na kuutangazia ulimwengu kuwa ingawa nimekuwa nikiweweseka kwa muda mrefu kutokana na kukosa mahali pa kukita, sasa nimepapata. Nimejikita.<\/span><\/span><br \/><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><\/p>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"margin:0 0 10pt;\"><span><span style=\"font-size:x-small;\">Baada ya kukita huku na kule pasipo kujikita, majuzi nilikita kwenye takwimu za matokeo ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana ili nione kama kuna uwezekano wa matokeo ya sense hiyo kutoa mwanga wa kuboresha maisha ya watu na hivyo kunipa fursa ya kujikita kutumia matokeo hayo kuhubiri matarajio ya kupatikana neema kwa watanzania.<\/span><\/span><\/div>\n<p><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><span><span style=\"font-size:x-small;\">Lakini matokeo ya takwimu ya sensa yalinimaliza nguvu. Nikiwa nimejikita kuyaperuzi, nilijikuta ninakitwa na ongezeko kubwa la mimba za utotoni na ukubwani. <\/span><\/span><br \/><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><\/p>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"margin:0 0 10pt;\"><span><span style=\"font-size:x-small;\">Kwangu mimi jambo la maana nililoliona kwenye matokeo yale ni ongezeko kubwa la watu ambalo chanzo chake ni watanzania wenyewe kupeana mimba bila mpangilio.<\/span><\/span><\/div>\n<p><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><span><span style=\"font-size:x-small;\">Na nilipojikita kuchunguza chanzo cha watanzania kujazana mimba kama hawana akili nzuri nilibaini kuwa ni mikito ya ukakasi wa maisha inayozidi kukita kila kukicha.<\/span><\/span><br \/><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><span><span style=\"font-size:x-small;\"><\/span><\/span><br \/><span><span style=\"font-size:x-small;\">Hebu twende pamoja ili kila ninapokita tukite pamoja. Tuzikite akili zetu kufikiri pamoja kwa kawaida tu kuwa ni kwanini watanzania wanapeana mimba kwa fujo kiasi cha takwimu za hesabu yao kuonyesha kuwa wameongezeka kwa kasi wakati kasi ya ukuaji wa uchumi wao na ustawi wao kisiasa ukididimia.<\/span><\/span><br \/><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><span><span style=\"font-size:x-small;\">Tuzifikirishe akili zetu kuwa ni kwanini watanzania wanazaliana sana licha ya kutokuwa na uhakika wa maisha yao ya kesho! Majibu ya haraka ingawa ni mepesi yanayopatikana ni haya.<\/span><\/span><br \/><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><\/p>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"margin:0 0 10pt;\"><span><span style=\"font-size:x-small;\">Mosi; ukosefu wa kazi. Kwamba watanzania wengi bila kujali kama wanapenda kufanya kazi au lah! Mara nyingi wanakuwa hawana kazi za kufanya kwa sababu ama hawataki kufanya kazi au wakati mwingine wanakuwa hawana kazi ya kufanya.<\/span><\/span><\/div>\n<p><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><span><span style=\"font-size:x-small;\">Watanzania hawataki kufanya kazi kwa sababu wamekulia katika mazingira ya kutofanya kazi. Siyo wote lakini wengi wamekulia katika mazingira ya aina hiyo. Kwao hawa maisha yanakwenda kiujanja ujanja. <\/span><\/span><br \/><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><\/p>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"margin:0 0 10pt;\"><span><span style=\"font-size:x-small;\">Wanaingiza fedha kwa kupiga porojo. Haijalisha kama porojo hizo zinaweza kutafasiliwa kuwa ni utaperi au lah! Muhimu ni kwamba hiyo ndiyo staili yao ya maisha.<\/span><\/span><\/div>\n<p><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><span><span style=\"font-size:x-small;\">Watanzania hawa wavivu wa kufanya kazi wana bidii ya kupeana mimba. Mazingira wanakopigia porojo yanahamasisha upeanaji mimba kwa sababu mara nyingi wanakuwa <span>\u00a0<\/span>baa au sehemu nyingine za starehe. Inaeleweka, starehe ni pamoja na kugawiana mimba.<\/span><\/span><br \/><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><\/p>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"margin:0 0 10pt;\"><span><span style=\"font-size:x-small;\">Pili; giza. Haina shaka hata kidogo kuwa mimba nyingi zinatungwa gizani, haijalishi kama ni mchana au usiku lakini ni kawaida kwa watu wengi wanapotaka kugawiana mimba kujifungia sehemu yenye giza. <\/span><\/span><\/div>\n<p><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><span><span style=\"font-size:x-small;\">Hata kama ni mchana kukiwa na mwangaza mkali wa jua shurti milango na madirisha ifungwe ili kuwe na giza. Kama ni mwanga basi utaruhusiwa kuwepo kidogo sana.<\/span><\/span><br \/><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><\/p>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"margin:0 0 10pt;\"><span><span style=\"font-size:x-small;\">Sasa Tanzania ni nchi ya giza. Nishati ya umeme imekuwa ikipatikana kwa kudra za mwenyezi mungu. Serikali imeridhika na hilo la Tanzania kuwa taifa la giza. <\/span><\/span><\/div>\n<p><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><span><span style=\"font-size:x-small;\">Kuna mamia ya watanzania wanaopenda kufanya kazi lakini wanashindwa kwa sababu ya kukosa mwanga unaozalishwa kwa nishati ya umeme ambayo serikali imeshindwa kuhakikisha upatikanaji wake wa uhakika.<\/span><\/span><br \/><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><\/p>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"margin:0 0 10pt;\"><span><span style=\"font-size:x-small;\">Serikali inapenda watanzania wagawiane mimba kwa wingi ingawa haitaki kusema hivyo wazi. Inachokifanya kuhakikisha nia yake hiyo inafanikiwa ni kusema uongo.<\/span><\/span><\/div>\n<p><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><span><span style=\"font-size:x-small;\">Mfano wa uongo huo ni ule wa profesa anayesimamia upatikanaji wa umeme ambaye alitangaza hivi karibuni kuwa kwa sababu yeye ni profesa na amechaguliwa kusimamia umeme ambao kwa miaka nenda rudi umekuwa adimu kupatikana, atauprofesa umeme ili upatikane kwa uhakika. Hautakosekana tena.<\/span><\/span><br \/><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><\/p>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"margin:0 0 10pt;\"><span><span style=\"font-size:x-small;\">Ajabu! Umeme umeuprofesa uprofesa wake, umeendelea kutopatikana. Kukatika kwa umeme bila mpangilio kunakoendelea sasa sehemu mbalimbali nchini kunadhihirisha hili. Kwamba profesa alisema uongo.<\/span><\/span><\/div>\n<p><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><span><span style=\"font-size:x-small;\">Hivyo kwa sababu ya giza, watu wakiwa majumbani hawawezi kuangalia televisheni au kusikiliza redio na badala yake hujifungia vyumbani mapema na kulala gizani. Matokeo yake ndiyo hayo, mimba. <\/span><\/span><br \/><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><\/p>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"margin:0 0 10pt;\"><span><span style=\"font-size:x-small;\">Sasa; kwa sababu watanzania wengi hawana kazi za kufanya kwa sababu ni wavuvi, na kwa sababu serikali imeshindwa kuwawezesha watanzania wengi kufanya kazi na badala yake wanashinda wakisogoa sehemu zao za kazi.<\/span><\/span><\/div>\n<p><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><span><span style=\"font-size:x-small;\">Na kwa sababu watu wengi wanapenda simulizi za kupeana mimba, nani kafumaniwa na nani na nani kachumbiwa na nani, kaolewa au yuko na nani. Matokeo ya maongezi haya huwasukuma watanzania ambao sehemu kubwa ya maisha yao ni giza kujikita katika kugawiana mimba.\u00a0<span>\u00a0<\/span><\/span><\/span><br \/><span style=\"font-size:x-small;\"> <\/span><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Na Simba Gembagu Ng\u2019wana Njamiti Kila nikikita ninakitwa. Popote ninapokita napokewa na mikito. Napokewa na mikito halisi ya kitanzania inayonikita. Ninakita ili nijikite lakini sijikiti badala yake ninakitwa. Ninatafuta pa kukita ili nipate pa kujikita na kuutangazia ulimwengu kuwa ingawa nimekuwa nikiweweseka kwa muda mrefu kutokana na kukosa mahali pa kukita, sasa nimepapata. Nimejikita. Baada [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":false,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[1],"tags":[35],"coauthors":[],"class_list":["post-1500","post","type-post","status-publish","format-standard","category-uncategorized","tag-mikito"],"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/1500","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=1500"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/1500\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=1500"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=1500"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=1500"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=1500"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}