{"id":1490,"date":"2017-08-26T16:18:00","date_gmt":"2017-08-26T16:18:00","guid":{"rendered":"https:\/\/msangirstz8.wordpress.com\/2017\/08\/26\/wanakita-kizulu-ninakita-kiswanglish\/"},"modified":"2022-11-09T11:17:05","modified_gmt":"2022-11-09T11:17:05","slug":"wanakita-kizulu-ninakita-kiswanglish","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=1490","title":{"rendered":"WANAKITA KIZULU, NINAKITA KISWANGLISH"},"content":{"rendered":"<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\"><em><strong>Simba Gembagu Ngw\u2019ana Njamiti<\/strong><\/em><\/div>\n<div><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">NIMEKUTANA wa Wazulu, nimekutana nao nchini kwao huku bondeni kwa mzee Madiba. Lakini mzee Madiba anaumwa sana, tumuombee.<\/div>\n<div><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">Wazulu, kama walivyo waafrika wengine wana mbwembwe za kibantu asilia, wanapenda sana kujivunia vya kwao, wanajivunia uafrika wao, wanawadharau sana wakuja bila kujali kama ni\u00a0 waafrika kama wao au lah.<\/div>\n<div><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">Eti! Walifikia hatua ya kunidharau hata mimi mzee Mikito. Kila nilipojikita kukitukuza Kiswahili wao walijikita kwenye lugha yao ya Kizulu, wakanilazimisha kuongea Kiswanglish. Watu wa ajabu sana.<\/div>\n<div><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">Hata hivyo, pamoja na katabia kao ka ujivuni ni watu wakarimu sana kwenye kinywaji. Wanaheshimu kinywaji nadhani kuliko kazi, hasa wanaoishi kwa kukitana.<\/div>\n<div><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">Wakiwa katika vikao vya wanamikito, humkaribisha yeyote kujiunga nao. Lakini karibu yao ina walakini, ukijongea sharti ujinunulie bia mwenyewe. Hukuna cha bure huku.<\/div>\n<div><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">Wiki iliyopita, nilikuwa nalanda landa katika vitongoji vya Soweto, nilikwenda kuweka kambi Zone Five ndani ya kilabu maarufu kinachoitwa \u2018gogo store.\u2019 kinapendelewa sana na waswihili wanaoishi eneo hilo.<\/div>\n<div><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">Ilipotimu saa moja kamili usiku kwa majira ya huku, huko nyumbani saa mbili kamili wateja waswahili wawili waliomba kuangalia taarifa ya habari ya nyumbani Tanzania.<\/div>\n<div><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">Dada muuzaji alikubali, akaweka ITV nikajiunga na wale waswahili wawili waliokuwa katikati ya kundi la vijana wa Kizulu kusikiliza taarifa ile.<\/div>\n<div><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">Wazulu, wake kwa waume walitaka kutafasiriwa kinachoripotiwa. Mzee Mikito haraka nikajipa kazi ya ukalimani na niliifanya kwa usafaha.<\/div>\n<div><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">Kizulu nilipata kijifunza enzi hizo katika masomo yangu ya elimu dunia.<\/div>\n<div><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">Ghafla wakati taarifa ya habari inaendelea alionekana afande mkubwa, anaitwa Suleiman Kova, akiwashukuru wananchi wa Dar es Salaam kwa ushirikiano waliouonyesha wakati wa mapokezi ya Rais wa Marekani, Barack Obama.<\/div>\n<table class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left: auto; margin-right: auto; text-align: center;\" cellspacing=\"0\" cellpadding=\"0\" align=\"center\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align: center;\"><a style=\"margin-left: auto; margin-right: auto;\" href=\"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/3be80-kova.jpg\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/3be80-kova.jpg?w=300\" width=\"320\" height=\"212\" border=\"0\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align: center;\">Afande Kova<\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">Ninamfahamu Kova ni mwanamikito wa Dar es Salaam, ni rafiki yangu sana huyu tangu tukiwa vijana kule mkoani Mwanza.<\/div>\n<div><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">Niliamua kumfagilia rafiki yangu Afande Kova kwa wazulu kwa sababu najua anapenda kusifiwa. Siyo dhambi kusifiwa kwa sababu hayupo asiyependa sifa.<\/div>\n<div><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">Nilianza kusifia mavazi yake ya rangi ya bluu aliyokuwa amevaa siku hiyo kama alivyoonekana kwenye televisheni.<\/div>\n<div><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">Halafu nikaeleza jinsi jamaa alivyo mchapakazi. Nilijikita kutoa sifa hadi za uongo, nilipoona nakaribia kuishiwa nilijikita kueleza jinsi alivyojikita kusimamia fukuza fukuza ya wamachinga ili Obama atakapokuwa anapita asiwaone wanavyohangaika juani kutafuta ngama.<\/div>\n<div><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">Dah! Nilidakwa mdomoni na Wazulu. Wa kwanza alipayuka, \u2018eeei wena, foseki, nkuruma ini,\u2019 akimaanisha ninazungumza nini. \u00a0Nikanyamaza. Yeye akasimama, akapayuka tena, \u2018wena ntombi, nginigeze ebia, Heineken.\u2019 Moyo ukatokota kwa hasira, nikajua jamaa kanitukana.<\/div>\n<div><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">Waswahili wenzangu wakaniambia hajatukana, bali alikuwa anaagiza bia, eti! Ntombi ni msichana. Lugha ya ajabu kweli kweli.<\/div>\n<div><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">Hakunijali, akajikita kutoa kauli za kumponda afande mkubwa Kova kwa kujikita kusimamia operesheni ondoa machinga,\u00a0 alimponda vilivyo baba wa watu, eti! Kwa cheo chake, kwa jinsi alivyoonekana na magwanda yake, kusimamia fukuza fukuza ya machinga kunaashiria kwamba hana kazi ya kufanya. Aliniudhi kweli.<\/div>\n<div><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">Kuepusha balaa, nikajikita kuzungumza Kiswanglish ambacho nilijua atakuwa anaelewa japo hivyo hivyo. Nikaanza kuelezea mipango ya mbeleni ya serikali ya kuhakikisha Dar es Salaam linakuwa jiji safi kuliko mengi barani Afrika na pilika pilika zinazoendelea sasa za ujenzi wa miundombinu na mambo mengine mengi.<\/div>\n<div><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">Akanikata kauli tena, akarudi kule kule alikokuwa amejikita mwanzoni, akahoji, Dar es Salaam itakayokuwa safi ni ipi? Ni hiyo inayoonekana kwenye televisheni jinsi ilivyopangiliwa hovyo hovyo kuliko maeneo ya ushenzini ya Soweto au?<\/div>\n<div><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">Hakunipa nafasi ya kuzungumza, akajikita kunieleza jinsi viongozi wa Tanzania wanavyofika Afrika Kusini mara nyingi na kuona miji ilivyojengwa, lakini wameshindwa kuiga walau robo ili kujenga huko nyumbani.<\/div>\n<div><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">Kwa dharau ambayo siwezi kuieleza hapa kwa sababu najua nitawaliza wakubwa serikalini, akasema, Dar es Salaam ilipaswa kujengwa mithili ya New York ndani ya miaka kumi kama kungekuwa na viongozi wenye utashi wa kulitumikia taifa, lakini kwa hawa waliopo, hadi mwisho wa dunia itaendelea kuwa jiji la hovyo lisilotazamika machoni hata na watoto wanaoishi uswahili katika vitongoji vya Soweto.<\/div>\n<table class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left: auto; margin-right: auto; text-align: center;\" cellspacing=\"0\" cellpadding=\"0\" align=\"center\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align: center;\"><a style=\"margin-left: auto; margin-right: auto;\" href=\"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/cbb06-uchafu2bdar.jpg\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/cbb06-uchafu2bdar.jpg?w=300\" width=\"320\" height=\"170\" border=\"0\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align: center;\">Taka zilizotupwa ovyo jijini Dar es Salaam<\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\"><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">Nilivuta picha Dar es Salaam na kuona jinsi ilivyo chafu nikaona jinsi waswahili wenzangu wanavyotupa maganda ya ndizi na machunga barabarani, nikaona msululu wa foleni barabarani, nikajiinamia kwa aibu.<\/div>\n<div><\/div>\n<div class=\"MsoNormal\" style=\"line-height: normal; margin: 0;\">Kama alivyofanya yeye na mimi kwa sauti ya kilevi nikapayuka, \u2018wena ntombi, nginigeze ebiere, Castel,\u2019 huku moyoni nikijiapiza kuufikisha ujumbe huu kwa afande mkubwa Kova na wenzake wanaohusika hata kama utawaudhi ili walau nao waone aibu kama hii iliyonikuta mimi.<\/div>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Simba Gembagu Ngw\u2019ana Njamiti NIMEKUTANA wa Wazulu, nimekutana nao nchini kwao huku bondeni kwa mzee Madiba. Lakini mzee Madiba anaumwa sana, tumuombee. Wazulu, kama walivyo waafrika wengine wana mbwembwe za kibantu asilia, wanapenda sana kujivunia vya kwao, wanajivunia uafrika wao, wanawadharau sana wakuja bila kujali kama ni\u00a0 waafrika kama wao au lah. Eti! Walifikia hatua [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":3412,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","footnotes":""},"categories":[72],"tags":[35],"coauthors":[],"class_list":{"0":"post-1490","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-mikito","8":"tag-mikito"},"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/1490","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=1490"}],"version-history":[{"count":2,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/1490\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":3413,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/1490\/revisions\/3413"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/3412"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=1490"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=1490"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=1490"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=1490"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}