{"id":11346,"date":"2026-10-30T12:37:07","date_gmt":"2026-10-30T12:37:07","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=11346"},"modified":"2026-10-30T12:53:27","modified_gmt":"2026-10-30T12:53:27","slug":"ndoto-za-wafanyabiashara-wavuvi-na-wasafiri-zinapokutana-bandari-ya-bukoba","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=11346","title":{"rendered":"NDOTO ZA WAFANYABIASHARA, WAVUVI NA WASAFIRI ZINAPOKUTANA BANDARI YA BUKOBA"},"content":{"rendered":"\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><em>NASMA MAYUNGA<\/em><\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">BANDARI ya Bukoba,&nbsp;ndipo mahali ambapo ndoto za wafanyabiashara, wavuvi na wasafiri hukutana na uhalisia wa maendeleo ya kasi.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Unapozungumzia historia ya usafiri na biashara katika ukanda wa Ziwa Victoria, jina Bukoba linaishi kwenye mioyo ya wengi. Lakini leo simulizi ya Bandari ya Bukoba imebadilika na kuwa ya kusisimua zaidi.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kutoka kwenye miundombinu ya kale, ya zama za ukoloni hadi sasa kwenye fukwe za kisasa zinazovutia machoni,&nbsp;mandhari ya kuvutia ya bandari, vifaa vya kisasa vya kupakia na kupakua shehena, majengo ya kisasa ya ofisi, wasafiri na kuhifadhi mizigo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Ni mabadiliko makubwa kila eneo katika Bandari ya Bukoba; mabadiliko ambayo yameleta mapinduzi ya kiuchumi na kijamii kwa wanajamii &nbsp;mkoani Kagera.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Ni haki ya kila Mtanzania kujua kiini cha mabadiliko haya makubwa, kuzionea fahari meli mpya, kubwa na za kisasa zinazotia nanga katika Bandari ya Bukoba na maana ya uwepo wa meli hizo kwa uchumi wa Mkoa wa Kagera.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Lakini kubwa zaidi ni kwa nini Bandari ya Bukoba sasa inatajwa kama lango kuu la biashara katika eneo la ukanda wa maziwa makuu?<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"768\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/de876269-eeb4-40c3-855f-d4cbcbfcbbc1-1024x768.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-11348\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/de876269-eeb4-40c3-855f-d4cbcbfcbbc1-1024x768.jpg 1024w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/de876269-eeb4-40c3-855f-d4cbcbfcbbc1-768x576.jpg 768w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/de876269-eeb4-40c3-855f-d4cbcbfcbbc1-300x225.jpg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/de876269-eeb4-40c3-855f-d4cbcbfcbbc1.jpg 1280w\" sizes=\"auto, (max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><em>Mhandisi Mnanka Maginga<\/em><\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">&nbsp;Katika Makala haya, Mhandisi wa Bandari ya Bukoba,&nbsp;Mnanka Maginga ambaye amefanya mahojiano na Tanzania PANORAMA Blog kuhusu maboresho makubwa yaliyofanywa na Mamlaka ya Usimamzi wa Bandari (TPA) katika Bandari ya Bukoba anaeleza;<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cBandari ya Bukoba ilianzishwa miaka ya 1930 na historia inaonyesha kwamba ilikamilika kujengwa mwaka 1945.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cUjenzi uliofanyika kipindi hicho; kwanza kabisa kilijengwa kizuizi cha upepo (wind breaker) ambayo inakinga bandari dhidi ya mawimbi na upepo ili meli zinapoingia bandarini ziweze kushusha na kupakia mizigo kwa usalama.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cPia yalijengwa magati mawili, gati namba moja lilikuwa na urefu wa mita 60 na gati namba mbili likiwa na urefu wa mita 82. Lilijengwa pia jengo la abiria lililokuwa na uwezo wa kuchukua abiria wachache tu.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cPamoja na jengo la abiria pia yalijengwa maghala ya mizigo. Kwa hiyo huo ndio ujenzi uliofanyika kipindi hicho katika Bandari ya Bukoba.\u201d<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Anapomaliza kuzungumza kuhusu hali ilivyokuwa awali katika Bandari ya Bukoba, anazungumzia hali ya sasa; anasema:<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cBaada ya Bandari ya Bukoba kufanya kazi kwa muda mrefu, ilionekana kuwepo uhitaji wa kuiboresha. Maboresho ya kwanza yalianza kutekelezwa mwaka 2023.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cMradi huo wa uboreshaji wa Bandari ya Bukoba ulikuwa na thamani ya Shilingi bilioni 19.5. Utekelezaji wake ulianza mwezi Januari, 2023 na ulikamilika mwezi Aprili, 2025.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"640\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/152A1965.jpg-1024x640.jpeg\" alt=\"\" class=\"wp-image-11349\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/152A1965.jpg-1024x640.jpeg 1024w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/152A1965.jpg-768x480.jpeg 768w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/152A1965.jpg-300x188.jpeg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/152A1965.jpg.jpeg 1280w\" sizes=\"auto, (max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><em>Gati jipya la kupakia na kushusha mizigo lililojengwa katika Bandari ya Bukoba. <\/em><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"640\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/152A1967.jpg-1024x640.jpeg\" alt=\"\" class=\"wp-image-11350\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/152A1967.jpg-1024x640.jpeg 1024w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/152A1967.jpg-300x188.jpeg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/152A1967.jpg-768x480.jpeg 768w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/152A1967.jpg.jpeg 1280w\" sizes=\"auto, (max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><em>Boya la kuongozea meli.<\/em><\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cKazi hiyo ilipokamilika, &nbsp;Bandari ya Bukoba iliingia kwenye kipindi cha uangalizi cha mwaka mmoja ambacho kimekamilika Julai, 2026 na sasa tunatarajia bandari itaendelea na utoaji huduma kama kawaida kuanzia Oktoba, 2026.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Mhandisi Maginga anasema maboresho ya miundombinu yaliyofanyika kwenye &nbsp;bandari hiyo yamebadilisha mandhari, ubora wa utoaji huduma na kwamba kiujumla, kila kitu katika bandari hiyo kimebadilika.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cKabla ya maboresho, abiria walikuwa wakiteseka wakati wanasubiri kusafiri. Mazingira ya jengo la abiria kusubiri safiri hayakuwa rafiki na naweza kusema yalikuwa mazingira magumu sana, jengo lilikuwa dogo sana.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cHivi sasa limejengwa jengo kubwa na la kisasa, lina viti vya kutosha, vyoo safi na mazingira yake yote ni rafiki yenye hadhi ya kimataifa. Jengo lina uwezo wa kuchukua abiria wengi kwa wakati mmoja na lina urahisi wa huduma za ukaguzi.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cTPA imejenga jengo jipya la abiria lenye uwezo wa kuchukua abiria 313, lakini pia imejenga maegesho mawili ya magari yenye uwezo wa kuegesha magari kati ya 40 mpaka 60 kwa wakati mmoja.\u201d<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"640\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/152A1978.jpg-1024x640.jpeg\" alt=\"\" class=\"wp-image-11351\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/152A1978.jpg-1024x640.jpeg 1024w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/152A1978.jpg-768x480.jpeg 768w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/152A1978.jpg-300x188.jpeg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/152A1978.jpg.jpeg 1280w\" sizes=\"auto, (max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><em>Eneo jipya la kushusha mizigo katika Bandari ya Bukoba.<\/em><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"640\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/152A1979.jpg-1024x640.jpeg\" alt=\"\" class=\"wp-image-11352\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/152A1979.jpg-1024x640.jpeg 1024w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/152A1979.jpg-300x188.jpeg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/152A1979.jpg-768x480.jpeg 768w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/152A1979.jpg.jpeg 1280w\" sizes=\"auto, (max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><em>Eneo jipya linatumika kwa ajili ya kupakia mizigo<\/em>. <\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Mhandisi Maginga anazungumzia pia maboresho yaliyofanywa kwenye magati kwa kueleza kuwa;<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cZamani gati zilizokuwepo zilikuwa ndogo na za kizamani, zilijengwa miaka 1900 huko hivyo meli kubwa za kisasa zilikuwa haziwezi kutia nanga kwa urahisi.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cHivi sasa baada ya maboresho meli kubwa na za kisasa zinatia &nbsp;nanga kwa usalama na ufanisi mkubwa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u00a0\u201cTPA imeyaboresha magati mawili yalikuwepo; gati namba moja kabla ya kuboreshwa, wakati wa masika ambapo mvua huwa nyingi na kina cha maji katika Ziwa Victoria huongezeka, gati hilo lilikuwa linafunikwa na maji.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cLimejengwa upya, limeinuliwa juu zaidi, hivi sasa linafanya kazi kipindi chote cha mwaka ikiwemo wakati wa mvua nyingi. Gati namba mbili lilikuwa na urefu wa mita 82, limeboreshwa na kuwa na urefu wa mita 100.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cKuna hili jambo la &nbsp;mabadiliko ya tabia nchi. Lilikuwa likisababisha changamoto kubwa sana kwenye baadhi ya magati hasa gati namba moja na kwenye magati yanayohudumia boti zinazokwenda visiwani nayo wakati wa mvua nyingi yalikuwa yanafunikwa na maji kabisa.<\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"576\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/WhatsApp-Image-2026-10-27-at-17.11.42-2-1024x576.jpeg\" alt=\"\" class=\"wp-image-11353\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/WhatsApp-Image-2026-10-27-at-17.11.42-2-1024x576.jpeg 1024w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/WhatsApp-Image-2026-10-27-at-17.11.42-2-300x169.jpeg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/WhatsApp-Image-2026-10-27-at-17.11.42-2-768x432.jpeg 768w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/WhatsApp-Image-2026-10-27-at-17.11.42-2-1536x864.jpeg 1536w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/WhatsApp-Image-2026-10-27-at-17.11.42-2.jpeg 1600w\" sizes=\"auto, (max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Mwonekano wa gati la<em> Bandari ya Bukoba baada ya kufanyiwa maboresho.<\/em><\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cChangamoto hizo sasa zimebaki historia, gati namba moja lina uwezo wa kutoa huduma kipindi chote cha mwaka hata kipindi cha mvua nyingi. Magati madogo yanayohudumia boti zinazokwenda visiwani nayo yamepandishwa juu ili kuweza kutoa huduma. Kazi iliyofanyika ni kubwa sana.\u201d<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Pembeni ya Mhandisi Maginga yupo Afisa wa Bandari ya Bukoba, &nbsp;Agabi Abraham Kasebere ambaye anapogeukiwa na Tanzania PANORAMA na kuulizwa kuhusu hatua zilizochukuliwa na TPA kuimarisha miundombinu ya bandari hiyo, haraka haraka anasema;<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"768\" height=\"1024\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/58834d2f-3320-4b37-845d-a511b5ad7ef7-768x1024-1.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-11354\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/58834d2f-3320-4b37-845d-a511b5ad7ef7-768x1024-1.jpg 768w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/58834d2f-3320-4b37-845d-a511b5ad7ef7-225x300.jpg 225w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/58834d2f-3320-4b37-845d-a511b5ad7ef7.jpg 960w\" sizes=\"auto, (max-width: 768px) 100vw, 768px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><em>Afisa wa Bandari ya Bukoba, Agabi Kasebele.<\/em><\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cHali inajieleza. Zamani &nbsp;upakiaji na ushushaji wa mizigo ulitegemea misuli ya binadamu na mifumo ya kizamani iliyochelewesha shughuli.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cBaada ya maboresho, bandari imewekewa miundombinu bora ya kupakia na kushusha mizigo, maeneo maalumu ya wazi yaliyosakafiwa na mifumo ya usalama kwa ajili ya kulinda mali za wafanyabiashara na abiria wanaosafiri ndani na nje ya nchi imeimarishwa. Hivi sasa bandari yote hii imefungwa kamera.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cUnajua ndugu mwandishi, mahali popote mazingira ya kazi yakiwa mazuri ufanisi pia unakuwepo. Hapa bandarini hivi sasa meli kubwa kama MV. Mwanza zinatia nanga bila shida.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cZipo pia meli za watu binafsi nyingi tu ambazo zinakuja kupakia mizigo hapa. Katika mkoa huu wa Kagera tuna kiwanda kikubwa cha sukari, Kiwanda cha Kagera Sugar, ndio kiwanda pekee kinachozalisha sukari kwa wingi katika ukanda huu, meli nyingi zinakuja kupakia shehena ya sukari katika bandari hii.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cHapa kwa sasa zinatia nanga meli zenye uwezo wa kubeba mzigo wa tani 600, tani 500 na zaidi. &nbsp;<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cLakini pia hivi sasa tunapokea mizigo mingi kutoka Uganda na Kenya. Bandari ya Bukoba kwa sasa ni sehemu ambayo wafanyabiashara, wavuvi na wasafiri wanakutana na uhalisia wa shughuli zao zinazowafungulia fursa za maendeleo kwa kasi sana.\u201d <\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"640\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/BC2A2045.jpg-1024x640.jpeg\" alt=\"\" class=\"wp-image-11355\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/BC2A2045.jpg-1024x640.jpeg 1024w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/BC2A2045.jpg-300x188.jpeg 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/BC2A2045.jpg-768x480.jpeg 768w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/BC2A2045.jpg.jpeg 1280w\" sizes=\"auto, (max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><em>Kutoka kushoto ni mpiga picha wa Tanzania PANORAMA, Japhet Massawe, Mhandisi wa Bandari ya Bukoba, Mnanka Maginga, Mtangazaji wa Tanzania PANORAMA, Mariam Milondomo, Afisa wa Bandari ya Bukoba, Agabi Kasebele, Msanifu wa Tanzania PANORAMA, Collin Mullinda na mwisho ni Mtangazaji Mwandamizi wa Tanzania PANORAMA, Nasma Mayunga.<\/em><\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kasebele anaeleza zaidi kuwa mbali ya maboresho yaliyoibadili Bandari ya Bukoba, miundombinu mingine &nbsp;inayozunguka bandari hiyo, mfano barabara ni rafiki kwa watumiaji.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Anasema maboresho yaliyofanyika kwenye Bandari ya Bukoba yamebadilisha sura ya mji wa Bukoba na kuwa kitovu cha biashara na usafiri katika ukanda wa Ziwa Victoria.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>NASMA MAYUNGA BANDARI ya Bukoba,&nbsp;ndipo mahali ambapo ndoto za wafanyabiashara, wavuvi na wasafiri hukutana na uhalisia wa maendeleo ya kasi. Unapozungumzia historia ya usafiri na biashara katika ukanda wa Ziwa Victoria, jina Bukoba linaishi kwenye mioyo ya wengi. Lakini leo simulizi ya Bandari ya Bukoba imebadilika na kuwa ya kusisimua zaidi. Kutoka kwenye miundombinu ya [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":11347,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[70],"tags":[],"coauthors":[201],"class_list":["post-11346","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-makala-za-kitaifa"],"amp_enabled":true,"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/10\/WhatsApp-Image-2026-10-27-at-17.11.43-1.jpeg","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/11346","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=11346"}],"version-history":[{"count":3,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/11346\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":11359,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/11346\/revisions\/11359"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/11347"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=11346"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=11346"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=11346"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=11346"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}