{"id":1087,"date":"2021-01-10T12:03:00","date_gmt":"2021-01-10T12:03:00","guid":{"rendered":"https:\/\/msangirstz8.wordpress.com\/2021\/01\/10\/ccm-ilala-yatoa-msimamo-madai-ya-diwani-wake-kudanganya-uraia\/"},"modified":"2021-01-10T12:03:00","modified_gmt":"2021-01-10T12:03:00","slug":"ccm-ilala-yatoa-msimamo-madai-ya-diwani-wake-kudanganya-uraia","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=1087","title":{"rendered":"CCM ILALA YATOA MSIMAMO MADAI YA DIWANI WAKE KUDANGANYA URAIA"},"content":{"rendered":"<p>\u00a0<\/p>\n<div class=\"separator\" style=\"clear:both;text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/bfefb-9.jpg?ssl=1\" style=\"margin-left:1em;margin-right:1em;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"400\" src=\"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.co.tz\/wp-content\/uploads\/2022\/11\/bfefb-9.jpg?resize=400%2C400&#038;ssl=1\" width=\"400\" \/><\/a><\/div>\n<p><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">NA MWANDISHI WETU<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ilala, kimesema hakina shaka na maelezo yaliyotolewa na Diwani wa Kata Kivukoni, Sharik Choughule kuhusu uraia wake.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Kimesema kabla ya wagombea wa chama hicho kupitishwa kuiwa wagombea katika uchaguzi, kilijiridhisha kuwa wote wana sifa stahiki.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">CCM kimesema watu wanaoibuka sasa kudai uraia wa Choughule una utata wanapaswa kupuuzwa kwa sababu CCM huteua wagombea wake kwa umakini na baada ya kujiridhisha hivyo wenye shaka na uteuzi huo wafuate taratibu za kimahakama kuthibitisha madai yao.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Hayo yameelezwa jana na Katibu wa CCM wa Wilaya ya Ilala Iddi Mkowa katika mahojiano yake na Tanzania PANORAMA kuhusu madai ya utata wa uraia wa Choughule na kwamba alitoa taarifa zisizokuwa sahihi kwa chama zilizomuwezesha kuteuliwa.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Mkowa alisema CCM hakina muda wa kuanza kuchunguza tuhuma za udanganyifu au utata wa uraia wa kada wake huyo kwa sababu kina uhakika na taarifa alizotoa hivyo wenye wasiwasi wana wajibu wa kuthibitisha madai yao kisheria ndipo chama kiweze kuchukua hatua.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Kauli hii ya Mkowa inafuatia taarifa iliyoripotiwa juzi na Tanzania PANORAMA kuwa Choughule anadaiwa kutoa taarifa zisizokuwa sahihi kuhusu uraia wake ili kufanikisha azma yake ya kuwa kiongozi katika chama hicho.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Madai hayo yalianza kusambaa mapema mwezi uliopita lakini jitahada za Tanzania PANORAMA kumfikia kuyazungumzia hazikuweza kufanikiwa kutokana na kile kilichoelezwa kuwa kutingwa na shughuli nyingi za kisiasa.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Hata hivyo, mmoja wa viongozi wa kata hiyo aliyefikiwa na Tanzania PANORAMA na kukubali kuzungumza kwa sharti la jina lake kuhifadhiwa kwa vile hataki aonekane ana nia mbaya dhidi ya mbio za kusaka uongozi wa kisiasa za Choughule, alisema awali kulikuwa na utata huo lakini ulitatuliwa.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Taarifa zilizokusanywa Tanzania PANORAMA zimeonyesha kuwa Choughule aliingia nchini kwa kutumia hati ya kusafiria ya India akiwa ameambata na ndugu yake wa kiume, ambao walikuja kumtembelea mjomba wao anayefanya biashara jijini Dar es Salaam.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Uchunguzi umeonyesha kuwa Choughule na ndugu yake walikuja nchini kuonana na mjomba wao aliyekuwa ametwaa mali za baba yao baada ya kufariki dunia.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Washirika wa karibu wa Choughule wamekaririwa kuwa vijana hao wawili walishindwa kuafikiana na mjomba wao ndipo walipogoma kuondoka nchini kurejea India walikokuwa wakiishi na mama yao.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Kwamba ili kuzika mzozo baina yao, mjomba wao aliwaingiza katika moja ya kampuni zake kufanya kazi huku akiwataka wawe na subira ya kutatua utata wa umiliki wa mali hizo.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u00a0Imeelezwa kuwa mjomba (jina limehifadhiwa kwa sababu hajapatikana kuzungumza) alitoa taarifa ofisi za uhamiaji kuhusu uwepo wa vijana hao waliokuwa wakiishi nchini na kufanya kazi kinyume cha sheria na walikamatwa na taratibu za kuwarudisha India zilianza kufanyika.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Taarifa zaidi zimeeleza kuwa vijana hao walilia na kupiga magoti mbele ya mjomba wao wakimuomba azungumze na maofisa wa Uhamiaji ili wasirejeshwe India kwa sababu walikuwa wakiishi maisha ya shida na mama yao baada ya baba yao kufariki na kwamba mjomba wao alikuwa hawatumii fedha kama alivyokuwa akifanya baba yao licha ya kujimilikisha mali zote.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Inadaiwa mjomba wao aliwapa sharti la kutomuuliza tena kuhusu mali alizotwaa kwa marehemu kama wanataka kiendelea kuwepo Tanzania, amri ambayo waliiafiki na yalifanyika mazungumzo wakaachiwa.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u00a0Afisa mmoja wa CCM wa Kata ya Kivukoni ambaye jina lake limehifadhiwa ameeleza kuwa ni kweli vijana hao waliingia nchini wakitokea India na kufikia kwa mjomba wao kabla ya kukamatwa na maofisa uhamiaji ambao waliwapakia kwenye ndege na kuwarudisha India ambako walikataliwa kuingia na kurudishwa hapa nchini.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">&#8220;Ni kweli Choughule alikuja nchini akiwa na mwenzake. Walikuja kwa mjomba wao lakini baadaye kulitoka mtafaruku wakakamatwa na uhamiaji wakapandishwa ndege wakarejeshwa India ambako hawakupokelewa walirudishiwa uwanja wa ndege, wakarejea Tanzania.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">&#8220;Hakukuwa na namna ikabidi wapokelewe hapa nchini wakarudi tena kuishi na mjomba wao ndipo zikaanza kufanyika taratibu za uraia na uhamiaji iliwasafisha kwa kuwapa uraia wakawa huru kujihusisha na shughuli za kisiasa na mpaka sasa Choughule anaendelea na siasa,&#8221; alisema.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Choughule amekuwa akikwepa kulizungumzia suala hilo kwa zaidi ya wiki tatu sasa kwani licha ya Tanzania PANORAMA kufika ofisi za CCM Kata ya Kivukoni ambako hakupatikani na kisha kutafutwa kwa simu yake ya kiganjani na kuomba apewe muda kabla ya kuzungumza, hajatekeleza ahadi yake hiyo wala kujibu maswali aliyotumiwa.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphery Polepole ambaye alitafutwa kwa simu yake ya kiganjani kuzungumzia suala hilo, simu yake imekuwa ikiita bila majibu na hata alipotumiwa ujumbe wa maandishi kwenye simu yake hakuujibu.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Kwa mujibu wa taratibu za Idara ya Uhamiaji, raia wa kigeni anaweza kupewa uraia kabla ya kuwa na sifa za kugombea nafasi za uongozi wa kisiasa isipokuwa urais wa Tanzania akiishi nchini kuanzia miaka nane na kufuata taratibu za kuomba uraia ikiwemo muda wote wa kuishi nchini kuwa na kibali.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Tanzania PANORAMA limeperuzi sifa zinazotakiwa kwa wanachama wa CCM kugombea uongozi wa kisiasa ambapo ya kwanza inasomeka awe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.<\/span><span style=\"font-size:26pt;\"><\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span>\u00a0<\/span><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>\u00a0 NA MWANDISHI WETU CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ilala, kimesema hakina shaka na maelezo yaliyotolewa na Diwani wa Kata Kivukoni, Sharik Choughule kuhusu uraia wake. Kimesema kabla ya wagombea wa chama hicho kupitishwa kuiwa wagombea katika uchaguzi, kilijiridhisha kuwa wote wana sifa stahiki. CCM kimesema watu wanaoibuka sasa kudai uraia wa Choughule una [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":false,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[1],"tags":[],"coauthors":[],"class_list":{"0":"post-1087","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","6":"category-uncategorized"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/1087","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=1087"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/1087\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=1087"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=1087"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=1087"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=1087"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}