{"id":10736,"date":"2026-06-23T10:56:36","date_gmt":"2026-06-23T10:56:36","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10736"},"modified":"2026-06-23T10:56:41","modified_gmt":"2026-06-23T10:56:41","slug":"dirisha-la-tuzo-kwa-watafiti-awamu-ya-nne-lafunguliwa","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10736","title":{"rendered":"DIRISHA LA TUZO KWA WATAFITI AWAMU YA NNE LAFUNGULIWA"},"content":{"rendered":"\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefungua Dirisha la Maombi ya Awamu ya Nne ya Tuzo kwa Watafiti wanaochapisha matokeo ya tafiti zao katika majarida yenye hadhi ya juu kimataifa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Dirisha hilo limekuwa wazi tangu Juni 19 hadi Oktoba 31, 2026, likilenga kuhamasisha utafiti, ubunifu na matumizi ya sayansi katika kuchochea maendeleo ya taifa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Akizindua dirisha hilo jijini Dodoma, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema tuzo hizo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuimarisha tafiti zinazotoa suluhisho kwa changamoto za kijamii na kiuchumi, pamoja na kuongeza uzalishaji wa teknolojia na ubunifu wa ndani unaochangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Prof. Mkenda amesema tangu kuanzishwa kwa mpango huo mwaka 2023, jumla ya machapisho 336 yaliwasilishwa katika awamu tatu zilizopita, huku machapisho 86 yakikidhi vigezo vya kutunukiwa tuzo. Watafiti 200 wa Kitanzania wamefaidika na mpango huo, ambapo Serikali imetoa zaidi ya Sh. bilioni 1.9 kama motisha ya kuendeleza tafiti zenye ubora wa kimataifa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kwa mwaka wa fedha 2026\/27, Serikali imetenga Sh bilioni 1.5 kwa ajili ya utekelezaji wa tuzo hizo ambazo zitahusisha nyanja za Sayansi Asilia na Hisabati, Afya na Sayansi Shirikishi, Sayansi za Wanyama na Kilimo pamoja na Uhandisi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), maeneo yanayotajwa kuwa muhimu katika kuharakisha maendeleo ya uchumi unaotegemea maarifa, sayansi na ubunifu.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefungua Dirisha la Maombi ya Awamu ya Nne ya Tuzo kwa Watafiti wanaochapisha matokeo ya tafiti zao katika majarida yenye hadhi ya juu kimataifa. Dirisha hilo limekuwa wazi tangu Juni 19 hadi Oktoba 31, 2026, likilenga kuhamasisha utafiti, ubunifu na matumizi ya sayansi katika kuchochea maendeleo ya taifa. Akizindua [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":10737,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":true,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[254],"class_list":["post-10736","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","category-habari-kitaifa"],"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/06\/9499f4df-24a1-4a84-91a1-2005810acbb9.jpg?fit=1080%2C720&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10736","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=10736"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10736\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":10738,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10736\/revisions\/10738"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/10737"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=10736"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=10736"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=10736"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=10736"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}