{"id":1070,"date":"2021-01-10T12:44:00","date_gmt":"2021-01-10T12:44:00","guid":{"rendered":"https:\/\/msangirstz8.wordpress.com\/2021\/01\/10\/jwtz-tiss-kuombwa-kumsaka-mwanafunzi-aliyepotea-st-marys\/"},"modified":"2021-01-10T12:44:00","modified_gmt":"2021-01-10T12:44:00","slug":"jwtz-tiss-kuombwa-kumsaka-mwanafunzi-aliyepotea-st-marys","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=1070","title":{"rendered":"JWTZ, TISS KUOMBWA KUMSAKA MWANAFUNZI ALIYEPOTEA ST MARY\u2019S"},"content":{"rendered":"<table align=\"center\" cellpadding=\"0\" cellspacing=\"0\" class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/babashadya6.files.wordpress.com\/2021\/01\/0f949-17.jpg\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"296\" src=\"https:\/\/babashadya6.files.wordpress.com\/2021\/01\/0f949-17.jpg?w=300&#038;resize=400%2C296\" width=\"400\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align:center;\">Mkuu wa Majeshi, Venance Mabeyo<\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<p>\u00a0<\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;font-size:large;\">NA MWANDISHI WETU<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) wataombwa kumsaka mwanafunzi aliyekuwa akisoma Shule ya Sekondari ya Bweni ya St. Mary\u2019s iliyoko Mbezi Makonde, Labna Said Salim ambaye ametoweka tangu Oktoba 4, 2020.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Taarifa iliyotolewa na Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Kinondoni, Joseph Kapere kwa Tanzania PANORAMA Blog leo, imeeleza kuwa taasisi hizo zitaombwa kusaidia kumsaka mwanafunzi huyo popote alipo baada ya jitihada za Jeshi la Polisi kumsaka kushindwa kuzaa matunda.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Kapere ambaye alikuwa akizungumzia mwenendo wa uchunguzi wa timu ya maafisa wanne wa serikali iliyoundwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo kuchunguza mazingira ya kutoweka kwa mwanafunzi huyo na kumsaka mahali alipo, ameeleza kuwa tume hiyo imekwishamkamata kijana anayedaiwa kuishi na mwanafunzi huyo baada ya kutoroka shuleni na sasa inasubiri wanafunzi wa kidato cha nne wamalize mitihani ya taifa ili iweze kuchukua hatua zaidi.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Timu hiyo inayomsaka mwanafunzi huyo inaundwa na Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Kinondoni, Afisa Usdalama wa Wilaya ya Kinondoni, Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Kinondoni na Mdhibiti Ubora wa Elimu Kanda.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cUchunguzi wetu unaendelea lakini hatufanikiwa kumpata huyo mtoto. Tiumekwishamkamata na kumuhoji kijana ambaye inadaiwa kuwa yule mtoto alitorokea kwake, anakiri kwamba ni kweli alikwenda chumbani kwake lakini huwa anakwenda mara kwa mara na marafiki zake na kwamba aliondoka akamuacha hapo chumbani akiwa na marafiki zake.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cLakini wale marafiki zake saba tuliowakuta nyumbani kwa baba yake mahali ambako anaishi huyo kijana wakiwa wanavuta bangi wameeleza kuwa ni kweli huyo mtoto alipotoroka shule ule usiku alikwenda kwa huyo kijana wakawa wote kabla ya kutoweka kusikojulikana,<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cNa wale waliomsindikiza kwenda kwenye hiyo nyumba ambao ni wanafunzi wenzake nao tuimewahoji na wanakiri kuwa mtoto Labna alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na huyo kijana na kwamba siku hiyo walimsindikiza akaenda kwake.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cSasa unajua wanafunzi wengi wa kidato cha nne wako kwenye mitahani, tunasubiri jumatano wamalize ili tuiwakutanishe pamoja wote tuliowahoji watueleze kwa pamoja ndipo tuchukua hatua zaidi,\u201d alisema Kapere.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Alipoulizwa hatua zitakazochikuliwa na timu hiyo baada ya kukamilisha uchunguzi wake alisema itaandika taarifa itakayoipeleka kwa Mkuu wa Wilaya kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi lakini itaomba Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) vialikwe kusaidia kumsaka mwanafunzi huyo kutokana na jeshi la polisi kutopata mafanikio.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cSisi tutaandika taarifa yetu na tumeishaanza kuandika, tutaeleza upungufu wote tulioubaini kwenye hiyo shule na tutatoa mapendekezo tutapeleka kwa mkuu wa wilaya ambaye ndiye aliyeunda timu hii. Lakini niseme tu moja kwa moja katika mapendekezo yetu tutashauri TISS na JWTZ waalikwe kumsaka huyu mtoto kwasababu nadhani polisi wanahitaji msaada maana mpaka sasa hawajafanikiwa,\u201d alisema Kapere.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><\/p>\n<table align=\"center\" cellpadding=\"0\" cellspacing=\"0\" class=\"tr-caption-container\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\">\n<tbody>\n<tr>\n<td style=\"text-align:center;\"><a href=\"https:\/\/babashadya6.files.wordpress.com\/2021\/01\/a2b55-11.jpg\" style=\"margin-left:auto;margin-right:auto;\" target=\"_blank\" rel=\"noopener\"><img data-recalc-dims=\"1\" loading=\"lazy\" decoding=\"async\" border=\"0\" height=\"400\" src=\"https:\/\/babashadya6.files.wordpress.com\/2021\/01\/a2b55-11.jpg?w=225&#038;resize=300%2C400\" width=\"300\" \/><\/a><\/td>\n<\/tr>\n<tr>\n<td class=\"tr-caption\" style=\"text-align:center;\">Labna<\/td>\n<\/tr>\n<\/tbody>\n<\/table>\n<p><span style=\"font-size:large;\"><br \/><\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Mwanafunzi Labna alitoweka shuleni Oktoba 4, 2020 na taarifa za awali zilieleza kuwa alitoroka akiwa na wafunzi wanzake kwenda kwenye maeneo ya starehe na kutokomea moja kwa moja.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">Zephania Maduhu ambaye ni mjomba wa mwanafunzi huyo aliyekuwa akimlipia ada ya shule aliieleza Tanzania PANORAMA Blog kuwa ana wasiwasi mtoto wake ameuawa kwani tangu Oktoba 4, 2020 alipopotea akiwa chini ya uangalizi wa shule, taarifa za kupotea kwake zilitolewa Oktoba 8, 2020 na matron wake, Sarah Murra aliyempigia simu mama mzazi wa mwanafunzi huyo akiulizia kama ameishafika nyumbani jambo ambalo limekuwa liibua hisia zinazotia shaka kuhusu usalama wa mtoto huyo.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u201cHuyo mtoto ninamlea mimi, ninamlipia ada ya shule mimi, ni mtoto wa dada yangu, anasoma St. Mary\u2019s, Mbezi Makonde. Oktoba 8, mwaka huu, matron wake anaitwa Sarah Murra, alimpigia simu mama yake, yaani dada yangu akimuuliza kama Labna kafika nyumbani.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u00a0\u201cDada yangu ambaye wakati huo alikuwa mkoani Shinyanga akashangaa akamuuliza amefikaje nyumbani wakati yupo shule au shule zimefungwa ghafla tena? Yule matron akamjibu ametoroka shuleni tangu Oktoba 4, 2020 hivyo alikuwa anataka kujua kama yupo nyumbani, dada akamwambia yeye yupo mkoani Shinyanga na anajua mtoto wake yupo shule.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u00a0\u201cAliporudi kutoka safari Shinyanga akakuta mtoto hajapatikana na shule haijatoa taarifa polisi yaani hata wasiwasi hawana. Ikabidi yeye aende kutoa ripoti Kituo cha Polisi cha Stakishari, waliponipa taarifa mimi nikafunga safari mpaka shuleni.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u00a0\u201cPale shuleni nikamkuta mkuu wa shule anaitwa Reca Ntipoo, akanijibu mtoto alitoroka shule usiku hajarudi na hawajui alipokwenda. Nikauliza kama wamefanya jitihada zozote za kumtafuta na kama wameisha ripoti polisi akasema hilo ni jukumu letu wazazi.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u00a0\u201cSasa hapo nikakasirika nikamuuliza mtoto tumemkabidhi shule na ada tumelipa kumbe katoroka zaidi ya mwezi hata taarifa polisi hawajatoa, hapo akajibu labda tukamtafute kwenye vijiwe vyao vya usiku wakitoroka huwa wanakwenda huko ambako wanafunzi wenzake wanavijua, akamuita mwanafunzi mmoja kweli akatuelekeza huko wanakokwenda usiku.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u00a0\u201cNilikuwa na rafiki yangu alinisindikiza tukaenda kumtafuta huko hatukumpata, hatukuwa na jinsi ikatubidi sisi tukatoe taarifa nyingine kituo cha Polisi Goba na polisi tulipowaelezea nao walishangaa\u00a0 kweli kweli.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span style=\"font-size:large;\"><span style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\">\u00a0\u201cSasa RB tunayo ni STK\/RB\/10714\/2020 na mpelelezi wa shauri hilo ni Afande Gwake Mwakapande. Sidhani kama yupo hai sisi tunaamini ameishakufa lakini uongozi wa shule hii ndiyo umetuulia mtoto wetu. <\/span><span lang=\"PT\" style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\">Polisi wanajua sasa sijui kama wameishawauliza au bado,\u201d alisema Maduhu.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span lang=\"PT\" style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u00a0Kapere amekwishaieleza Tanzania PANORAMA Blog kuwa Mkuu wa Shule ya St. Mary\u2019s, Ntipoo alikiri kufanya uzembe kutotoa taarifa polisi na kwa wazazi kuhusu kupotea kwa mwanafunzi Labna na kwamba kutoroka kwa wanafunzi usiku na kwenda kwenye maeneo ya starehe ni jambo alilolikuta shuleni hapo hivyo hata baada ya kutoonekana kwa Labna aliamini kuwa alitoroka usiku kwenda kwenye mambo yake lakini angerudi.<\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span lang=\"PT\" style=\"font-family:Garamond, serif;line-height:115%;\"><span style=\"font-size:large;\">\u00a0Aidha Kapere amwishaeleza kuwa timu imebaini kuwa Shule ya Sekondari ya St Mary\u2019s ni chafu, haina ulinzi wa kutosha na ukuta wake haufai.<\/span><span style=\"font-size:26pt;\"><\/span><\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span lang=\"PT\">\u00a0<\/span><\/p>\n<p class=\"MsoNormal\"><span lang=\"PT\">\u00a0<\/span><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Mkuu wa Majeshi, Venance Mabeyo \u00a0 NA MWANDISHI WETU JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) wataombwa kumsaka mwanafunzi aliyekuwa akisoma Shule ya Sekondari ya Bweni ya St. Mary\u2019s iliyoko Mbezi Makonde, Labna Said Salim ambaye ametoweka tangu Oktoba 4, 2020. Taarifa iliyotolewa na Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":false,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[1],"tags":[],"coauthors":[],"class_list":{"0":"post-1070","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","6":"category-uncategorized"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/1070","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=1070"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/1070\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=1070"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=1070"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=1070"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=1070"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}