{"id":10650,"date":"2026-06-04T14:39:27","date_gmt":"2026-06-04T14:39:27","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10650"},"modified":"2026-06-04T14:39:36","modified_gmt":"2026-06-04T14:39:36","slug":"kampeni-za-chanjo-zaendelea-kuimarisha-afya-na-kinga-za-watoto-nchini","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10650","title":{"rendered":"KAMPENI ZA CHANJO ZAENDELEA KUIMARISHA AFYA NA KINGA ZA WATOTO NCHINI"},"content":{"rendered":"\n<figure class=\"wp-block-image size-full is-resized\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"483\" height=\"368\" src=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/06\/image-2.png\" alt=\"\" class=\"wp-image-10651\" style=\"width:1068px;height:auto\" srcset=\"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/06\/image-2.png 483w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/06\/image-2-300x229.png 300w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/06\/image-2-80x60.png 80w, https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/06\/image-2-150x114.png 150w\" sizes=\"auto, (max-width: 483px) 100vw, 483px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Serikali imeendelea kuimarisha huduma za chanjo nchini kupitia kampeni mbalimbali za chanjo, utoaji wa chanjo za kawaida katika vituo vya afya na kuwafikia watoto waliokosa chanjo ndani ya jamii, hatua inayolenga kuboresha afya na kinga ya watoto dhidi ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Hayo yameelezwa na Meneja wa Mpango wa Taifa wa Chanjo kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Georgina Joachim, leo Juni 4, 2026, wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Tathmini ya Utekelezaji wa Huduma za Chanjo nchini unaofanyika jijini Dar es Salaam.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Dkt. Joachim amesema kampeni za chanjo zimeendelea kuwa sehemu muhimu ya mkakati wa Taifa wa kuhakikisha watoto wote wanaostahili wanapatiwa chanjo kwa wakati, jambo linalochangia kupunguza magonjwa yanayoweza kuzuilika pamoja na vifo vya watoto huku akiongeza kuwa kampeni hizo zimekuwa nyenzo muhimu katika kuhakikisha hakuna mtoto anayebaki nyuma katika kupata huduma za chanjo, hivyo kuimarisha afya na ustawi wa watoto nchini.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cKampeni za chanjo zimekuwa nyenzo muhimu katika kuhakikisha hakuna mtoto anayebaki nyuma kwenye kupata huduma za chanjo. Hii ni hatua muhimu ya kulinda afya na maisha ya watoto wetu,\u201d amesema Dkt. Joachim.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Aidha, amefafanua kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu \u2013 TAMISEMI pamoja na wadau wa maendeleo, inaendelea kuimarisha mifumo ya ugavi na uhifadhi wa chanjo, ukusanyaji wa takwimu na ufuatiliaji wa utendaji ili kuhakikisha huduma za chanjo zinatolewa kwa ubora unaotakiwa na kuwafikia wananchi wote.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Dkt. Joachim amesisitiza kuwa mkutano huo wa tathmini ya mwaka ni fursa muhimu ya kutathmini mafanikio yaliyopatikana, kujadili changamoto zilizojitokeza na kuweka mikakati ya pamoja itakayosaidia kuboresha zaidi huduma za chanjo kwa manufaa ya watoto na jamii kwa ujumla.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Hatahivyo Amesema ushirikiano na wadau mbalimbali utaendelea kuwa nguzo muhimu katika kufanikisha malengo ya Taifa ya kuongeza kiwango cha chanjo na kuhakikisha watoto wote wanapata kinga dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Serikali imeendelea kuimarisha huduma za chanjo nchini kupitia kampeni mbalimbali za chanjo, utoaji wa chanjo za kawaida katika vituo vya afya na kuwafikia watoto waliokosa chanjo ndani ya jamii, hatua inayolenga kuboresha afya na kinga ya watoto dhidi ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo. Hayo yameelezwa na Meneja wa Mpango wa Taifa wa Chanjo kutoka Wizara [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":10651,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[253],"class_list":["post-10650","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-habari-kitaifa"],"amp_enabled":true,"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/06\/image-2.png","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10650","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=10650"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10650\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":10652,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10650\/revisions\/10652"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/10651"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=10650"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=10650"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=10650"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=10650"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}