{"id":10542,"date":"2026-06-02T09:47:30","date_gmt":"2026-06-02T09:47:30","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10542"},"modified":"2026-06-02T09:47:36","modified_gmt":"2026-06-02T09:47:36","slug":"kwagilwa-ahimiza-uhifadhi-wa-mazingira-dodoma","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10542","title":{"rendered":"KWAGILWA AHIMIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA DODOMA"},"content":{"rendered":"\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Naibu Waziri wa Mazingira, Mhe. Reuben Kwagilwa, amewataka wananchi kuendelea kushiriki kikamilifu katika juhudi za uhifadhi wa mazingira, akisisitiza kuwa jukumu hilo ni la kila Mtanzania ili kuhakikisha Taifa linafikia malengo ya maendeleo endelevu na kujenga uchumi wa kijani.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Mhe. Kwagilwa ametoa kauli hiyo alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali ya taasisi na wadau wanaoshiriki Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani 2026 yanayofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre (JKCC) jijini Dodoma.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Katika ziara hiyo, amejionea shughuli, huduma na teknolojia mbalimbali zinazochangia uhifadhi wa mazingira, matumizi endelevu ya rasilimali za asili pamoja na juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Amezipongeza taasisi na wadau wanaoshiriki maonesho hayo kwa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira na kutumia teknolojia rafiki kwa mazingira katika shughuli za kila siku.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Aidha, amesema ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi na wananchi ni muhimu katika kufanikisha juhudi za uhifadhi wa mazingira na kufikia malengo ya maendeleo endelevu ya Taifa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Akiwa katika banda la Wizara ya Nishati na taasisi zake za TANESCO, REA na TPDC, Mhe. Kwagilwa amepokea maelezo kuhusu mchango wa sekta ya nishati katika kuhifadhi mazingira kupitia matumizi ya nishati safi ya kupikia pamoja na teknolojia ya Gesi Asilia Iliyoshindiliwa kwenye Magari (CNG).<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Ameelezwa kuwa matumizi ya CNG yanaendelea kuhamasishwa nchini kama sehemu ya jitihada za kupunguza uchafuzi wa mazingira, huku yakichochea matumizi ya nishati safi na endelevu. Pia amejionea teknolojia na huduma mbalimbali zinazotolewa na sekta ya nishati katika kuunga mkono agenda ya uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya kijani.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Mhe. Kwagilwa amewataka wananchi kuzingatia kaulimbiu ya mwaka huu ya \u201cDira 2050: Tuwajibike Kukijanisha Tanzania\u201d kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazolenga kulinda na kuhifadhi mazingira.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Maonesho ya Wiki ya Mazingira Duniani 2026 yameanza rasmi leo Juni 1 na yanatarajiwa kuhitimishwa Juni 5, sambamba na maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani. Katika kipindi hicho, wananchi wanaendelea kutembelea mabanda mbalimbali ikiwemo la Wizara ya Nishati ili kupata elimu kuhusu uhifadhi wa mazingira, matumizi ya nishati safi ya kupikia, teknolojia ya CNG na suluhisho nyingine rafiki kwa mazingira.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Naibu Waziri wa Mazingira, Mhe. Reuben Kwagilwa, amewataka wananchi kuendelea kushiriki kikamilifu katika juhudi za uhifadhi wa mazingira, akisisitiza kuwa jukumu hilo ni la kila Mtanzania ili kuhakikisha Taifa linafikia malengo ya maendeleo endelevu na kujenga uchumi wa kijani. Mhe. Kwagilwa ametoa kauli hiyo alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali ya taasisi na wadau wanaoshiriki Maadhimisho ya [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":10543,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[253],"class_list":["post-10542","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-habari-kitaifa"],"amp_enabled":true,"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/06\/MAZINGIRA.jpg","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10542","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=10542"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10542\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":10544,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10542\/revisions\/10544"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/10543"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=10542"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=10542"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=10542"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=10542"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}