{"id":10473,"date":"2026-05-30T12:56:36","date_gmt":"2026-05-30T12:56:36","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10473"},"modified":"2026-05-30T12:56:40","modified_gmt":"2026-05-30T12:56:40","slug":"mkufunzi-wa-unodc-apongeza-polisi-wanamaji-kwa-kuimarisha-mapambano-dhidi-ya-uhalifu-majini","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10473","title":{"rendered":"MKUFUNZI WA UNODC APONGEZA POLISI WANAMAJI KWA KUIMARISHA MAPAMBANO DHIDI YA UHALIFU MAJINI"},"content":{"rendered":"\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC), Andres Reyes kutoka Colombia, amepongeza ushirikiano uliopo kati ya UNODC na Polisi Wanamaji nchini Tanzania, akisema umeendelea kuzaa matokeo chanya katika mapambano dhidi ya uhalifu unaofanyika katika maeneo ya majini.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Reyes alitoa kauli hiyo jijini Mwanza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo maalumu ya wiki nne kwa askari Polisi Wanamaji kuhusu mbinu za kuzuilia, kukagua na kukamata vyombo vya majini (Maritime Boarding, Search and Seizure Operations).<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Alisema mafunzo hayo yamelenga kuongeza uwezo wa askari katika kukabiliana na vitendo vya magendo, uvuvi haramu, usafirishaji wa silaha haramu pamoja na aina nyingine za uhalifu wa kimataifa unaofanyika kupitia njia za majini.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kwa mujibu wa Reyes, washiriki wa mafunzo hayo wamepatiwa maarifa na ujuzi wa kisasa utakaowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi na kuimarisha usalama katika mipaka ya maji nchini.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Aidha, alieleza kufurahishwa na hali ya usalama nchini Tanzania, akibainisha kuwa licha ya changamoto za uhalifu wa kimataifa, nchi imeendelea kuwa tulivu na salama. Alisisitiza kuwa UNODC itaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kupitia mafunzo na programu mbalimbali za kujenga uwezo wa kukabiliana na uhalifu wa kimataifa katika maeneo ya majini.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Frolence Mwenda alisema askari 10 wamehitimu mafunzo hayo maalumu na kwamba yatawawezesha kukabiliana na mbinu mpya zinazotumiwa na wahalifu.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kwa upande wake, Mkuu wa Kikosi cha Polisi Wanamaji Mkoa wa Mwanza, Mrakibu wa Polisi (SP) Wenceslaus Muchunguzi, alisema mafunzo hayo yatakuwa chachu ya kuongeza ufanisi wa operesheni za usalama majini na kuimarisha mapambano dhidi ya uhalifu katika maeneo ya maji nchini.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC), Andres Reyes kutoka Colombia, amepongeza ushirikiano uliopo kati ya UNODC na Polisi Wanamaji nchini Tanzania, akisema umeendelea kuzaa matokeo chanya katika mapambano dhidi ya uhalifu unaofanyika katika maeneo ya majini. Reyes alitoa kauli hiyo jijini Mwanza wakati wa hafla [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":10474,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[74,69],"tags":[],"coauthors":[253],"class_list":["post-10473","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-habari-kimataifa","category-habari-kitaifa"],"amp_enabled":true,"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/05\/mambo.png","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10473","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=10473"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10473\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":10475,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10473\/revisions\/10475"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/10474"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=10473"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=10473"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=10473"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=10473"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}