{"id":10464,"date":"2026-05-30T12:21:00","date_gmt":"2026-05-30T12:21:00","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10464"},"modified":"2026-05-30T12:21:07","modified_gmt":"2026-05-30T12:21:07","slug":"watatu-wafariki-dunia-katika-ajali-ya-basi-na-lori-mbeya","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10464","title":{"rendered":"WATATU WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BASI NA LORI MBEYA"},"content":{"rendered":"\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Watu watatu wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha basi la abiria na lori la mafuta iliyotokea leo Mei 30, 2026, majira ya saa 12 asubuhi katika Kijiji cha Mambi, Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Wilbert Siwa, amesema ajali hiyo ilihusisha lori lenye namba za usajili T115 DEH likiwa na tela T150 DFU aina ya Volvo Tank mali ya Kampuni ya Synergy ya Dar es Salaam, lililokuwa limebeba shehena ya mafuta ya dizeli kutoka Dar es Salaam kuelekea Tunduma mkoani Songwe.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Ameeleza kuwa lori hilo lilikuwa likiendeshwa na Mohamed Seif maarufu Maulid (60), mkazi wa Dar es Salaam, ambaye alilipotezea mwelekeo gari hilo wakati akijaribu kulipita gari lingine na kuvamia upande wa pili wa barabara.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kutokana na hali hiyo, lori hilo liligongana na basi la abiria lenye namba T200 ENQ aina ya Yutong mali ya Kampuni ya ABC Upper Class, lililokuwa likitoka Mbeya kuelekea Dar es Salaam likiendeshwa na Asead Asamu maarufu Tembo (40), mkazi wa Dar es Salaam.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Waliofariki dunia katika ajali hiyo ni dereva wa basi Asead Asamu (40), kondakta wa basi Letisia Bujabi (32), pamoja na dereva wa lori Mohamed Seif (60).<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Aidha, watu wanne walijeruhiwa katika ajali hiyo ambapo watatu walipatiwa matibabu na kuruhusiwa, huku majeruhi mmoja, Mariam Abdul (25), mkazi wa Dar es Salaam, akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Inyala.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kaimu Kamanda Siwa amesema uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori aliyekuwa akipishana na gari lingine bila kuchukua tahadhari stahiki.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limetoa wito kwa madereva wote kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuwa makini wanapokuwa safarini ili kuepusha ajali zinazoweza kusababisha vifo, majeruhi na hasara za mali.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Watu watatu wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha basi la abiria na lori la mafuta iliyotokea leo Mei 30, 2026, majira ya saa 12 asubuhi katika Kijiji cha Mambi, Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Wilbert Siwa, amesema ajali hiyo ilihusisha [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":10465,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[201,254],"class_list":["post-10464","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-habari-kitaifa"],"amp_enabled":true,"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/05\/AJALI.jpg","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10464","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=10464"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10464\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":10466,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10464\/revisions\/10466"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/10465"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=10464"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=10464"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=10464"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=10464"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}