{"id":10425,"date":"2026-05-22T15:13:53","date_gmt":"2026-05-22T15:13:53","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10425"},"modified":"2026-05-22T15:13:58","modified_gmt":"2026-05-22T15:13:58","slug":"mwanafunzi-kidato-cha-tatu-adaiwa-kujifungua-na-kumtupa-mtoto-chooni","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10425","title":{"rendered":"MWANAFUNZI KIDATO CHA TATU ADAIWA KUJIFUNGUA NA KUMTUPA MTOTO CHOONI"},"content":{"rendered":"\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Mwanafunzi wa kidato cha tatu wa Shule ya Sekondari Kibindu wilayani Chalinze mkoani Pwani anadaiwa kujifungua mtoto wa kike na kumtupa katika shimo la choo cha mabweni ya wanafunzi wa kike, tukio lililosababisha taharuki miongoni mwa wanafunzi na walimu wa shule hiyo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salum Morcase amesema tukio hilo lilitokea Mei 19, 2026 majira ya saa 4:00 asubuhi katika shule hiyo huku akibainisha kuwa mwanafunzi huyo alikuwa na ujauzito ambao haukubainika kwa kipindi chote cha miezi tisa kutokana na kuvaa majuba, hadi alipopatwa na maumivu makali ya tumbo na kwenda chooni ambapo alijifungua mtoto huyo kabla ya kumtupa kwenye shimo la choo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kwa mujibu wa Kamanda Morcase, mwanafunzi mwingine alipokwenda chooni aliona matone ya damu karibu na tundu la choo, na baada ya kumwaga maji alisikia sauti ya mtoto ndipo alipotoa taarifa kwa uongozi wa shule.<br>Kupitia ushirikiano wa viongozi wa kijiji, Polisi Kata pamoja na uongozi wa shule, mtoto huyo aliokolewa na kukimbizwa katika Kituo cha Afya Kibindu kwa ajili ya matibabu.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cMama na mtoto wanaendelea na matibabu katika Kituo cha Afya Kibindu na baada ya matibabu kukamilika hatua nyingine za kisheria zitafuata,\u201d amesema Kamanda Morcase.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Katika tukio jingine, Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia Kesi Juma Ibrahim (22), mkulima na mkazi wa Kifuleta wilayani Chalinze, kwa tuhuma za kumfanyia ukatili wa kingono mtoto wa miaka sita ambaye jina lake limehifadhiwa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kamanda Morcase amesema tukio hilo lilitokea Mei 17, 2026 majira ya saa 7:00 mchana baada ya mtuhumiwa huyo kumshawishi mtoto ambaye ni jirani yake na kumuingiza ndani kabla ya kutekeleza kitendo hicho.<br>Amesema wazazi wa mtoto walipobaini tukio hilo walitoa taarifa katika Kituo cha Polisi Mbwewe ambapo mtuhumiwa alikamatwa huku uchunguzi ukiendelea kabla ya kufikishwa mahakamani.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limekemea vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu kwa wakati ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Mwanafunzi wa kidato cha tatu wa Shule ya Sekondari Kibindu wilayani Chalinze mkoani Pwani anadaiwa kujifungua mtoto wa kike na kumtupa katika shimo la choo cha mabweni ya wanafunzi wa kike, tukio lililosababisha taharuki miongoni mwa wanafunzi na walimu wa shule hiyo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salum Morcase amesema tukio hilo lilitokea Mei [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":10426,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":true,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[70],"tags":[],"coauthors":[201],"class_list":["post-10425","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","category-makala-za-kitaifa"],"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/05\/d8208d70-1bc0-40a6-aaf5-8fcd4e56977c.jpeg?fit=275%2C183&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10425","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=10425"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10425\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":10427,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10425\/revisions\/10427"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/10426"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=10425"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=10425"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=10425"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=10425"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}