{"id":10422,"date":"2026-05-21T15:09:00","date_gmt":"2026-05-21T15:09:00","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10422"},"modified":"2026-05-22T15:11:13","modified_gmt":"2026-05-22T15:11:13","slug":"dkt-mwigulu-ahimiza-ulinzi-katika-ziwa-victoria","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10422","title":{"rendered":"DKT. MWIGULU AHIMIZA ULINZI KATIKA ZIWA VICTORIA"},"content":{"rendered":"\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinapaswa kuendelea kushirikiana katika kulinda na kuhifadhi Ziwa Victoria kutokana na umuhimu wake kwa maisha ya wananchi, uchumi wa ukanda huo pamoja na mustakabali wa vizazi vijavyo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Dkt. Nchemba amesema Ziwa Victoria ni rasilimali inayounganisha mataifa ya Afrika Mashariki hivyo kuna haja ya kuwepo kwa ushirikiano wa pamoja katika kulinda mazingira, kuimarisha usalama na kukuza shughuli za kiuchumi zinazotegemea ziwa hilo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Amesema hayo leo Alhamisi Mei 21, 2026 wakati akizindua rasmi Siku ya Ziwa Victoria na kufunga kilele cha maadhimisho ya kwanza yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane Nyamhongolo jijini Mwanza.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Katika maadhimisho hayo yaliyobebwa na kauli mbiu ya \u201cMaji Yetu, Mustakabali Wetu: Tuungane kwa Uendelevu wa Bonde la Ziwa Victoria,\u201d Waziri Mkuu amesema maadhimisho hayo yanapaswa kuwa chachu ya kuhamasisha usimamizi endelevu wa rasilimali za maji, kuimarisha mshikamano wa kikanda na kuongeza uwajibikaji wa pamoja katika utunzaji wa mazingira ya Ziwa Victoria.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Aidha, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuimarisha mifumo ya usalama majini, kudhibiti uharibifu wa mazingira na kuendeleza matumizi ya teknolojia katika usimamizi wa rasilimali za ziwa hilo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">\u201cSote tunawajibika kutunza mazingira ya Ziwa Victoria kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo,\u201d amesema Dkt. Nchemba.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesisitiza umuhimu wa kuimarishwa kwa mifumo ya uokoaji majini pamoja na matumizi ya mifumo ya kidijitali katika kufuatilia shughuli za uvuvi, ubora wa maji na athari za mabadiliko ya tabianchi.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Pia ametoa wito kwa taasisi za utafiti kuendelea kufanya tafiti zitakazosaidia kupata suluhisho la changamoto mbalimbali zinazoathiri mazingira ya Ziwa Victoria ikiwemo ongezeko la magugu maji na uharibifu wa vyanzo vya maji.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Awali, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kulinda na kuhifadhi Ziwa Victoria kutokana na mchango wake mkubwa katika uchumi, usalama na maendeleo ya wananchi wa ukanda wa ziwa.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinapaswa kuendelea kushirikiana katika kulinda na kuhifadhi Ziwa Victoria kutokana na umuhimu wake kwa maisha ya wananchi, uchumi wa ukanda huo pamoja na mustakabali wa vizazi vijavyo. Dkt. Nchemba amesema Ziwa Victoria ni rasilimali inayounganisha mataifa ya Afrika Mashariki hivyo kuna haja [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":10423,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":true,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[201],"class_list":["post-10422","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","category-habari-kitaifa"],"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/05\/MWIGULU.jpeg?fit=480%2C270&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10422","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=10422"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10422\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":10424,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10422\/revisions\/10424"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/10423"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=10422"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=10422"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=10422"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=10422"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}