{"id":10394,"date":"2026-05-20T14:48:06","date_gmt":"2026-05-20T14:48:06","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10394"},"modified":"2026-05-20T14:48:10","modified_gmt":"2026-05-20T14:48:10","slug":"china-na-urusi-waimarisha-ushirikiano-zaidi","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10394","title":{"rendered":"CHINA NA URUSI WAIMARISHA USHIRIKIANO ZAIDI"},"content":{"rendered":"\n<p>Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Urusi Vladimir Putin wameahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kijeshi kati ya mataifa yao huku wakisisitiza umuhimu wa kusaidiana katika maendeleo na kufufua uchumi.<\/p>\n\n\n\n<p>Akizungumza katika mkutano huo, Xi amesema China na Urusi zinapaswa kuendeleza ushirikiano wa karibu ili kuimarisha maendeleo ya mataifa hayo mawili pamoja na kulinda maslahi yao ya pamoja duniani.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa upande wake, Putin amesema uhusiano kati ya Moscow na Beijing umefikia kiwango cha juu na unaendelea kuonyesha mwenendo mzuri wa ushirikiano. Pia aliisifia Urusi kuwa muuzaji wa nishati anayeaminika licha ya mvutano unaoendelea Mashariki ya Kati.<\/p>\n\n\n\n<p>Viongozi hao pia wamekubaliana kuongeza muda wa miaka mitano wa mkataba wa ushirikiano wa biashara na kijeshi uliopo kati ya China na Urusi, hatua inayotajwa kuimarisha zaidi mahusiano ya mataifa hayo mawili.<\/p>\n\n\n\n<p>Mbali na hayo, Xi na Putin walijadili hali ya vita Mashariki ya Kati, ambapo Xi alisisitiza kuwa umefika wakati wa kusitishwa kwa mashambulizi na kupatikana kwa amani katika eneo hilo.<\/p>\n\n\n\n<p>Katika mazungumzo hayo, Putin alimualika Xi kutembelea Urusi mwaka ujao akieleza kuwa ushirikiano kati ya Beijing na Moscow una mchango mkubwa katika kuleta utulivu duniani. Xi alifanya ziara yake ya mwisho nchini Urusi mwezi Mei mwaka jana.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Urusi Vladimir Putin wameahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kijeshi kati ya mataifa yao huku wakisisitiza umuhimu wa kusaidiana katika maendeleo na kufufua uchumi. Akizungumza katika mkutano huo, Xi amesema China na Urusi zinapaswa kuendeleza ushirikiano wa karibu ili kuimarisha maendeleo ya mataifa hayo mawili pamoja [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":10395,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":true,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[253],"class_list":{"0":"post-10394","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-habari-kitaifa"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/05\/PUTIN-NA-XI.jpg?fit=1024%2C576&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10394","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=10394"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10394\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":10396,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10394\/revisions\/10396"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/10395"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=10394"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=10394"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=10394"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=10394"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}