{"id":10295,"date":"2026-05-14T13:07:29","date_gmt":"2026-05-14T13:07:29","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10295"},"modified":"2026-05-14T13:09:03","modified_gmt":"2026-05-14T13:09:03","slug":"shughuli-za-uchimbaji-madini-za-sitishwa-katika-mito-ya-mtisi-na-ibanda-mkoani-katavi","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10295","title":{"rendered":"SHUGHULI ZA UCHIMBAJI MADINI ZA SITISHWA KATIKA MITO YA MTISI NA IBANDA MKOANI KATAVI"},"content":{"rendered":"\n<p>Serikali imechukua hatua kali dhidi ya ukiukwaji wa sheria katika sekta ya madini baada ya Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, kusitisha shughuli za uchimbaji katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Katavi kutokana na ukiukwaji wa taratibu za mazingira na matumizi mabaya ya mfumo wa msaada wa kiufundi.<\/p>\n\n\n\n<p>Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Mavunde amesema serikali imeamua kusimamisha shughuli za uchimbaji katika maeneo ya mito ya Mtisi na Ibindi baada ya kubainika kuwepo kwa uchafuzi wa mazingira, ikiwemo uchepushaji wa maji ya mito pamoja na kutowasilishwa kwa taarifa muhimu kwa mamlaka husika.<\/p>\n\n\n\n<p>Amesema hatua hiyo inalenga kulinda mazingira na kuhakikisha shughuli zote za uchimbaji zinafanyika kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa, huku akionya kuwa serikali haitamvumilia mtu au kampuni yoyote itakayokiuka masharti ya uwekezaji na uchimbaji nchini.<\/p>\n\n\n\n<p>Katika hatua nyingine, Waziri huyo ametoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya mfumo wa msaada wa kiufundi katika sekta ya madini, akisema baadhi ya wawekezaji wamekuwa wakitumia vibaya mfumo huo kwa kuwapa wageni nafasi ya kufanya uchimbaji kupitia leseni za wazawa jambo ambalo ni kinyume cha sheria.<\/p>\n\n\n\n<p>Mavunde amesema msaada wa kiufundi unapaswa kuhusisha utoaji wa teknolojia, vifaa au utaalamu wa uchimbaji na uchakataji wa madini, na si kuwapa wageni fursa ya kufanya shughuli za uchimbaji moja kwa moja kupitia leseni za wachimbaji wadogo wa Kitanzania.<\/p>\n\n\n\n<p>\u201cMitambo niliyoikuta katika machimbo ya Kabatini ndiyo ninayotaka kuiona Tanzania nzima. Lakini hairuhusiwi mgeni kuingia kwenye leseni ndogo ya uchimbaji halafu akaanza kufanya kazi kama Mtanzania. Huo sio msaada wa kiufundi,\u201d amesema Mavunde.<\/p>\n\n\n\n<p>Aidha, amewataka wachimbaji wazawa kuwa makini wanapoingia mikataba ya uwekezaji au ushirikiano kwa kuhakikisha wanashirikisha wataalamu na wanasheria ili kulinda maslahi yao na kuepuka mikataba yenye masharti yasiyoeleweka.<\/p>\n\n\n\n<p>Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na Wizara ya Mazingira pamoja na wataalamu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuhakikisha kunakuwa na usimamizi madhubuti wa shughuli za uchimbaji wa madini nchini kwa lengo la kulinda rasilimali za taifa na mazingira.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Serikali imechukua hatua kali dhidi ya ukiukwaji wa sheria katika sekta ya madini baada ya Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, kusitisha shughuli za uchimbaji katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Katavi kutokana na ukiukwaji wa taratibu za mazingira na matumizi mabaya ya mfumo wa msaada wa kiufundi. Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Mavunde amesema serikali [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":true,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[201,253],"class_list":{"0":"post-10295","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","6":"category-habari-kitaifa"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10295","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=10295"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10295\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":10297,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10295\/revisions\/10297"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=10295"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=10295"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=10295"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=10295"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}