{"id":10291,"date":"2026-05-09T11:06:38","date_gmt":"2026-05-09T11:06:38","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10291"},"modified":"2026-05-09T11:06:46","modified_gmt":"2026-05-09T11:06:46","slug":"mlango-bahari-wa-hormuz-unavyoitesa-dunia","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10291","title":{"rendered":"MLANGO-BAHARI WA HORMUZ UNAVYOITESA DUNIA"},"content":{"rendered":"\n<p>TEHRAN, Iran<\/p>\n\n\n\n<p>MGOGORO unaoendelea kati ya Iran na Marekani katika Mlango-Bahari wa Hormuz umetikisa uchumi wa dunia. Kila nchi, zikiwamo za Afrika, inapitia maumivu ya kupanda kwa bei ya nishati ya mafuta.<\/p>\n\n\n\n<p>Maumivu yanatokana na ukweli kwamba kupanda kwa bei ya nishati hiyo kumeathiri sekta nyingi, mathalan ile ya usafiri, ambapo nauli zimekuwa juu.<\/p>\n\n\n\n<p>Hali ilianza kuwa mbaya baada ya Iran kufunga njia hiyo, ikiwa ni katika kulipiza kisasi kwa kitendo cha kushambuliwa na Marekani na Israel.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa sasa, Iran imeshikilia msimamo wake wa kudhibiti Hormuz na meli zinazokatiza hapo zimekuwa zikishambuliwa kwa mabomu.<\/p>\n\n\n\n<p>Taarifa rasmi za Umoja wa Mataifa (UN) zinaeleza kuwa meli 32 zimeshashambuliwa tangu vita vianze na kusababisha vifo vya mabaharia 10.<\/p>\n\n\n\n<p>Hormuz ni Mlango-Bahari wenye upana wa maili 21, sawa na kilometa 34. Kabla ya vita, asilimia 20 ya mafuta duniani yalipita hapo kila siku.<\/p>\n\n\n\n<p>Ukiweka kando mafuta, Mlango-Bahari huo ulitumika kusafirisha gesi asilia, mbolea na bidhaa zingine za petroli.<\/p>\n\n\n\n<p>Meli takribani 130 za mafuta na mizigo zilikatiza hapo kila siku, kwa mujibu wa Taasisi ya Tafiti ya Marekani, Lloyd\u2019s List Intelligence.<\/p>\n\n\n\n<p>Tangu vita vilipoanza Februari 28 hadi Mei 4, 2026, meli 534 zimekatiza, nyingi zikiwa ni zile zilizobeba mafuta ya Iran. Idadi hiyo ni ndogo, ukilinganisha na kipindi cha kabla ya vita.<\/p>\n\n\n\n<p>Mvutano katika Mlango-Bahari huo umesababisha kupanda kwa asilimia 50 ya bei ya gesi nchini Marekani na kufikia Dola 4.56 kwa kidumu kimoja.<\/p>\n\n\n\n<p>Bei ya mafuta ya ndege nchini humo nayo imeongezeka mara mbili, huku kiwango cha bima za meli nacho kikipanda kwa asilimia 10.<\/p>\n\n\n\n<p>Kukabiliana na majanga hayo, Rais Donald Trump alianzisha kile anachokiita &#8216;Project Freedom&#8217;. Ni mkakati wake wa kuhakisha Mlango-Bahari wa Hormuz unapitika, licha ya Iran kuweka ngumu.<\/p>\n\n\n\n<p>Wanajeshi wa Marekani wapatao 15,000 wako hapo, sambamba na ndege za kivita 100, lengo likiwa ni kuzipa ulinzi meli zote zinazokatiza Hormuz.<\/p>\n\n\n\n<p>Aidha, Shirika la Mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa (WFP) limetahadharisha kuwa watu milioni 45 duniani watakumbwa na balaa la njaa endapo Mlango-Bahari wa Hormuz hautofunguliwa.<\/p>\n\n\n\n<p>Katika ripoti yao, WFP wanaeleza kuwa uhaba wa nishati ya mafuta na mbolea unaweza kupandisha bei ya vyakula.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>TEHRAN, Iran MGOGORO unaoendelea kati ya Iran na Marekani katika Mlango-Bahari wa Hormuz umetikisa uchumi wa dunia. Kila nchi, zikiwamo za Afrika, inapitia maumivu ya kupanda kwa bei ya nishati ya mafuta. Maumivu yanatokana na ukweli kwamba kupanda kwa bei ya nishati hiyo kumeathiri sekta nyingi, mathalan ile ya usafiri, ambapo nauli zimekuwa juu. Hali [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":10292,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":true,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[81],"tags":[],"coauthors":[201,203],"class_list":{"0":"post-10291","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-makala-kimataifa"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/05\/trump.jpeg?fit=1280%2C960&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10291","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=10291"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10291\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":10293,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10291\/revisions\/10293"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/10292"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=10291"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=10291"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=10291"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=10291"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}