{"id":10268,"date":"2026-05-06T15:17:49","date_gmt":"2026-05-06T15:17:49","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10268"},"modified":"2026-05-06T15:17:58","modified_gmt":"2026-05-06T15:17:58","slug":"athari-za-vita-mashariki-ya-kati-bei-ya-mafuta-yazidi-kupaa-nchini","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10268","title":{"rendered":"ATHARI ZA VITA MASHARIKI YA KATI: BEI YA MAFUTA YAZIDI KUPAA NCHINI"},"content":{"rendered":"\n<p>Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za kikomo za mafuta ya petroli nchini, huku bei ya petroli katika Mkoa wa Dar es Salaam ikipanda kwa Sh295 kwa lita na kufikia Sh4,115 mwezi Mei 2026 kutoka Sh3,820 ya mwezi uliopita.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa mujibu wa taarifa hiyo, bei hizo mpya zimeanza kutumika rasmi kuanzia Mei 6, 2026 saa 6:01 usiku, ambapo dizeli inauzwa kwa Sh4,248 kwa lita na mafuta ya taa kufikia Sh4,677 kwa lita katika jiji la Dar es Salaam.<\/p>\n\n\n\n<p>EWURA imeeleza kuwa ongezeko hilo limetokana na kupanda kwa bei za mafuta katika soko la dunia, kunakosababishwa na mvutano wa kisiasa na vita vinavyoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati, hususan kati ya Marekani, Israel na Iran.<\/p>\n\n\n\n<p>Aidha, imebainisha kuwa kufungwa kwa Mlango Bahari wa Hormuz, unaopitisha takriban asilimia 20 ya mafuta yanayosafirishwa duniani, kumeongeza gharama za usafirishaji pamoja na bima za meli za mafuta, hali iliyochochea kupanda kwa bei hizo kimataifa.<\/p>\n\n\n\n<p>Mamlaka hiyo imeongeza kuwa Tanzania inaagiza sehemu kubwa ya mafuta kutoka Mashariki ya Kati, hivyo mabadiliko ya bei katika eneo hilo yana athari ya moja kwa moja kwa soko la ndani.<\/p>\n\n\n\n<p>Hata hivyo, Serikali imeendelea kutoa ruzuku ya Sh259 kwa kila lita ya dizeli ili kupunguza makali ya bei kwa wananchi, hasa katika sekta za usafirishaji na uzalishaji.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa mujibu wa viwango vipya, Mkoa wa Tanga petroli itauzwa kwa Sh4,176 kwa lita na dizeli Sh4,309, wakati Mtwara petroli itauzwa kwa Sh4,207 na dizeli Sh4,341 kwa lita.<\/p>\n\n\n\n<p>EWURA imewataka wafanyabiashara kuuza mafuta kwa bei zisizozidi viwango vilivyotangazwa, huku ikiwahimiza wananchi kutoa taarifa dhidi ya vituo vitakavyokiuka maelekezo hayo.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za kikomo za mafuta ya petroli nchini, huku bei ya petroli katika Mkoa wa Dar es Salaam ikipanda kwa Sh295 kwa lita na kufikia Sh4,115 mwezi Mei 2026 kutoka Sh3,820 ya mwezi uliopita. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, bei hizo mpya zimeanza [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":10269,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":true,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[201,253],"class_list":{"0":"post-10268","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-habari-kitaifa"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/05\/MAFUTA.jpeg?fit=724%2C900&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10268","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=10268"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10268\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":10270,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10268\/revisions\/10270"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/10269"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=10268"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=10268"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=10268"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=10268"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}