{"id":10244,"date":"2026-05-05T11:41:07","date_gmt":"2026-05-05T11:41:07","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10244"},"modified":"2026-05-05T11:41:15","modified_gmt":"2026-05-05T11:41:15","slug":"mapitio-mapya-ya-sheria-ya-ununuzi-wa-umma-yafanyika-kuoanisha-na-dira-ya-maendeleo-ya-taifa-2050","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10244","title":{"rendered":"MAPITIO MAPYA YA SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA YAFANYIKA KUOANISHA NA DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050"},"content":{"rendered":"\n<p>Wizara ya Fedha imeanza mchakato wa kupitia upya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura ya 410, kwa lengo la kuiboresha na kuioanisha na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, hatua inayotarajiwa kuimarisha mfumo wa ugavi na kuchochea maendeleo ya uchumi wa nchi.<\/p>\n\n\n\n<p>Mchakato huo umeanza kwa kikao kazi kilichowakutanisha wadau kutoka sekta ya umma na binafsi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gasper jijini Dodoma, ambapo washiriki walipata nafasi ya kutoa maoni na mapendekezo yao.<\/p>\n\n\n\n<p>Akifungua kikao hicho, Kaimu Kamishna wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Bw. Alex J. Haraba, amesema mapitio hayo yanalenga kujenga mfumo wa kisasa na jumuishi unaogusa hatua zote za mnyororo wa ugavi.<\/p>\n\n\n\n<p>Aidha ameeleza kuwa mfumo huo utahusisha upangaji wa mahitaji, ununuzi, upokeaji na ugomboaji, uhifadhi na utunzaji, usambazaji hadi uondoshaji wa mali, ili kuongeza ufanisi na uwazi katika matumizi ya rasilimali za umma.<\/p>\n\n\n\n<p>\u201cMapitio haya ni hatua ya kimkakati ya kuhakikisha mnyororo mzima wa ugavi unazingatiwa kikamilifu katika sheria mpya, sambamba na kuchochea ukuaji wa uchumi, maendeleo ya viwanda na maendeleo jumuishi na endelevu kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo 2050,\u201d alisema Bw. Haraba.<\/p>\n\n\n\n<p>Ameongeza kuwa Wizara ya Fedha ina jukumu la kisheria la kupitia na kuhuisha sera, sheria, kanuni na miongozo inayohusu ununuzi wa umma, na kwamba maoni ya wadau yatatumika kubaini maeneo yenye uhitaji wa maboresho.<br>Bw. Haraba aliwahimiza wadau kushiriki kikamilifu katika mchakato huo, akisisitiza kuwa ushiriki wao utasaidia kupata sheria bora, jumuishi na yenye tija kwa maendeleo ya Taifa.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa mujibu wake, mapendekezo yote yatakayowasilishwa yatachambuliwa kwa kina na kufanyiwa kazi katika hatua zinazofuata za marekebisho ya sheria hiyo.<\/p>\n\n\n\n<p>Kikao hicho kiliwakutanisha taasisi mbalimbali za umma zikiwemo Tume ya Mipango, Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), miongoni mwa nyingine.<\/p>\n\n\n\n<p>Hatahivyo, wadau kutoka sekta binafsi wakiwemo wazabuni na makampuni mbalimbali wameshiriki kutoa maoni yao, wakilenga kuboresha mazingira ya biashara na kuongeza ushiriki wao katika shughuli za ununuzi wa umma na ugavi nchini.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Wizara ya Fedha imeanza mchakato wa kupitia upya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura ya 410, kwa lengo la kuiboresha na kuioanisha na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, hatua inayotarajiwa kuimarisha mfumo wa ugavi na kuchochea maendeleo ya uchumi wa nchi. Mchakato huo umeanza kwa kikao kazi kilichowakutanisha wadau kutoka sekta ya umma na [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":10,"featured_media":10245,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":true,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[253],"class_list":{"0":"post-10244","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-habari-kitaifa"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/05\/c717f04b-3898-444e-8f6b-25b35bce4714.jpeg?fit=480%2C320&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10244","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/10"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=10244"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10244\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":10246,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10244\/revisions\/10246"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/10245"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=10244"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=10244"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=10244"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=10244"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}