{"id":10224,"date":"2026-05-05T11:25:07","date_gmt":"2026-05-05T11:25:07","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10224"},"modified":"2026-05-05T11:25:12","modified_gmt":"2026-05-05T11:25:12","slug":"carrick-alivyofaulu-mtihani-mgumu-old-trafford","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10224","title":{"rendered":"CARRICK ALIVYOFAULU MTIHANI MGUMU OLD TRAFFORD"},"content":{"rendered":"\n<p>MANCHESTER, Uingereza<br>KUKINOA kikosi cha Manchester United kimekuwa ni kibarua kigumu kwa makocha wengi katika miaka 13 ya hivi karibuni.<\/p>\n\n\n\n<p>Ruben Amorim alikiri hilo wiki chache tu baada ya kuanza kazi, akisema Man United yake Ni mbovu kuliko zote alizowahi kuziona.<\/p>\n\n\n\n<p>Hata hivyo, mambo yamebadilika &#8216;fasta&#8217; tangu Michael Carrick alipochukua nafasi ya kukiongoza kikosi hicho hadi mwishoni mwa msimu huu (2025-26).<\/p>\n\n\n\n<p>Baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Liverpool, Carrick ameiwezesha timu hiyo kurejea katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.<\/p>\n\n\n\n<p>Carrick aliikuta Man United ikiwa nafasi ya saba katika msimamo lakini sasa wako ndani ya &#8216;Top 4&#8217;, hivyo kujipatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.<\/p>\n\n\n\n<p>\u201cTulikuwa mbali na Ligi ya Mabingwa na tulitaka kurudi kwenye michuano hiyo. Kuwa hapa tulipo, tukiwa na mechi tatu mkononi, ni mafanikio makubwa,&#8221; amesema Carrick.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa upande mwingine, bado kuna sintofahamu juu ya hatima ya Carrick. Je, ataajiriwa moja kwa moja au atakabidhi mikoba kwa kocha mwingine mwishoni mwa msimu ujao?<\/p>\n\n\n\n<p>Wakati huo huo, Man United wameendelea kuhusishwa na makocha kadhaa wa kumpokea kijiti kiungo wao huyo wa zamani. Luis Enrique na Thomas Tuchel ni miongoni mwao.<\/p>\n\n\n\n<p>Baada ya kuifunga Liverpool wikiendi iliyopita, Muingereza huyo alisema angetamani kuwa kwenye benchi la ufundi msimu ujao. \u201cNapenda ninachokifanya. Ni nafasi nzuri kuendelea kuwa nayo,&#8221; alisema.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa sasa, nguvu kubwa aliyonayo Carrick, mbali ya kuimarika kwa kiwango cha timu, ni &#8216;sapoti&#8217; anayopewa na wachezaji wake pale Old Trafford, wengi wakitamani abaki.<\/p>\n\n\n\n<p>Nyota aliyesaini mkataba mpya hivi karibuni, Kobie Mainoo, ameeleza matumaini yake ya kuona kocha wake huyo akiajiriwa moja kwa moja kwa ajili ya msimu ujao.<\/p>\n\n\n\n<p>Lakini, mabosi wa Man United hawatokuwa wamesahau kile kilichotokea kwa Ole Gunnar Solskjaer, ambaye alifanya vizuri akiwa kocha wa muda lakini alichemsha baada ya kupewa mkataba wa kudumu.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>MANCHESTER, UingerezaKUKINOA kikosi cha Manchester United kimekuwa ni kibarua kigumu kwa makocha wengi katika miaka 13 ya hivi karibuni. Ruben Amorim alikiri hilo wiki chache tu baada ya kuanza kazi, akisema Man United yake Ni mbovu kuliko zote alizowahi kuziona. Hata hivyo, mambo yamebadilika &#8216;fasta&#8217; tangu Michael Carrick alipochukua nafasi ya kukiongoza kikosi hicho hadi [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":8,"featured_media":10225,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":true,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[80,79],"tags":[],"coauthors":[203],"class_list":{"0":"post-10224","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-makala","8":"category-michezo"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/05\/carrick.webp?fit=1140%2C641&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10224","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/8"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=10224"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10224\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":10226,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10224\/revisions\/10226"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/10225"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=10224"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=10224"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=10224"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=10224"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}