{"id":10204,"date":"2026-05-04T14:52:17","date_gmt":"2026-05-04T14:52:17","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10204"},"modified":"2026-05-04T14:52:22","modified_gmt":"2026-05-04T14:52:22","slug":"kamisheni-ya-tume-ya-madini-ya-ridhishwa-na-kasi-ya-ukusanyaji-wa-maduhuli-sekta-ya-madini-nchini","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10204","title":{"rendered":"KAMISHENI YA TUME YA MADINI YA RIDHISHWA NA KASI YA UKUSANYAJI WA MADUHULI, SEKTA YA MADINI NCHINI"},"content":{"rendered":"\n<p>Kamisheni ya Tume ya Madini imeridhishwa na kasi ya ukusanyaji wa maduhuli katika Sekta ya Madini kupitia Tume ya Madini, hatua inayotoa matarajio ya Serikali kuvuka lengo la kukusanya shilingi trilioni 1.2 kwa mwaka wa fedha 2025\/2026.<\/p>\n\n\n\n<p>Hayo yamebainishwa leo Mei 4, 2026 jijini Dodoma wakati Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Dkt. Janet R. Lekashingo, alipoongoza kikao cha Kamisheni kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume kwa kipindi cha miezi mitatu pamoja na kuweka mikakati ya kuendelea kuimarisha mchango wa Sekta ya Madini katika uchumi wa Taifa.<\/p>\n\n\n\n<p>Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Lekashingo amewapongeza watendaji wa Tume ya Madini kwa mafanikio yaliyopatikana hususan katika ukusanyaji wa maduhuli, usimamizi wa masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa madini, kuimarika kwa usalama migodini pamoja na kuongezeka kwa ushiriki wa Watanzania katika Sekta ya Madini.<\/p>\n\n\n\n<p>\u201cNina imani kwa kasi iliyopo tutavuka lengo la Serikali la ukusanyaji wa maduhuli kwa mwaka huu wa fedha. Kazi inayofanywa na watendaji wa Tume inaonesha dhamira ya dhati ya kukuza Sekta ya Madini,\u201d amesema Dkt. Lekashingo.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo, katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita Tume imeendelea kusimamia utoaji na ufuatiliaji wa leseni za madini, ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali, usimamizi wa uzalishaji na mauzo ya madini pamoja na utekelezaji wa majukumu ya kisheria katika sekta hiyo.<\/p>\n\n\n\n<p>Pia ameongezaTume imefanya kaguzi katika migodi mikubwa, ya kati na midogo, mitambo ya uchakataji na uchenjuaji wa madini, mabwawa ya kuhifadhi tope sumu, maeneo ya miambataka na maghala ya kuhifadhi baruti katika mikoa yote ya kimadini nchini kwa lengo la kuhakikisha shughuli za uchimbaji zinafanyika kwa kuzingatia usalama, afya na utunzaji wa mazingira.<\/p>\n\n\n\n<p>Aidha, ameeleza kuwa usimamizi wa biashara ya madini umeendelea kuimarika kupitia masoko ya madini 44 na vituo 120 vya ununuzi wa madini vilivyoanzishwa nchini, hatua iliyosaidia kuongeza uwazi wa biashara na kuongeza ufanisi katika mfumo wa uuzaji na usafirishaji wa madini nchini.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Kamisheni ya Tume ya Madini imeridhishwa na kasi ya ukusanyaji wa maduhuli katika Sekta ya Madini kupitia Tume ya Madini, hatua inayotoa matarajio ya Serikali kuvuka lengo la kukusanya shilingi trilioni 1.2 kwa mwaka wa fedha 2025\/2026. Hayo yamebainishwa leo Mei 4, 2026 jijini Dodoma wakati Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Dkt. Janet R. Lekashingo, [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":10,"featured_media":10206,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":true,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[253],"class_list":{"0":"post-10204","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-habari-kitaifa"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/05\/TUME.jpeg?fit=480%2C339&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10204","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/10"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=10204"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10204\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":10207,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10204\/revisions\/10207"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/10206"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=10204"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=10204"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=10204"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=10204"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}