{"id":10172,"date":"2026-05-04T11:25:04","date_gmt":"2026-05-04T11:25:04","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10172"},"modified":"2026-05-04T11:25:10","modified_gmt":"2026-05-04T11:25:10","slug":"siasa-zilivyozigawa-palestina-israel-katika-soka","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10172","title":{"rendered":"SIASA ZILIVYOZIGAWA PALESTINA, ISRAEL KATIKA SOKA"},"content":{"rendered":"\n<p>VANCOUVER, Canada<\/p>\n\n\n\n<p>HIVI karibuni, ulifanyika Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) mjini Vancouver na tukio lililotikisa zaidi ni lile la viongozi wa mchezo huo katika mataifa ya Palestina na Israel kukataa kupiga picha ya pamoja.<\/p>\n\n\n\n<p>Ni Rais wa Chama cha Soka cha Palestina, Jibril Rajoub, na Makamu wa Rais wa Chama cha mchezo huo nchini Israel, Basim Sheikh Suliman.<\/p>\n\n\n\n<p>Baada ya kila mmoja kuzungumza, Rais wa FIFA, Gianni Infantino, aliwaomba kupeana mikono na kupiga picha ya pamoja, lakini Rajoub wa Palestina aligoma.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa wafuatiliaji wa siasa za Mashariki ya Kati, tukio hilo ni mwendelezo wa uhusiano mbaya wa kisiasa uliopo kati ya mataifa hayo, Israel na Palestina.<\/p>\n\n\n\n<p>Mwaka 2024, mamlaka za soka za Palestina ziliiandikia barua FIFA zikipendekeza Israel ifutiwe uanachama wake ndani ya Shirikisho hilo lenye makao makuu yake mjini Nyon, Uswis.<\/p>\n\n\n\n<p>Katika barua yake, Palestina iliutaja mzozo unaoendelea katika Ukanda wa Gaza, ikisema uharibifu unaofanywa na Israel unatosha kuzifanya klabu zake za soka kuondoshwa katika michuano ya FIFA.<\/p>\n\n\n\n<p>Aidha, walilalamikia pia kitendo cha Israel kusimamia klabu za soka zilizoko West Bank, eneo ambalo Palestina wanaamini liko katika mipaka yake.<\/p>\n\n\n\n<p>Hata katika hotuba yake katika Mkutano wa FIFA uliofanyika siku chache zilizopita, Rais wa Chama cha Soka cha Palestina, Rajoub, alijikita katika malalamiko hayo.<\/p>\n\n\n\n<p>Safari hii, alisema: &#8220;Hatuiambii FIFA ishughulikie mgogoro wa kisiasa, tunataka FIFA isimamie soka. Hatuiambii FIFA ikaamue mipaka, tunataka itumie sheria zake kuamua ni wapi wanachama wake wanapaswa kuishia katika kuratibu masuala ya soka.&#8221;<\/p>\n\n\n\n<p>Rajoub alisema West Bank, ikiwamo Mashariki mwa Jerusalem, si ardhi ya Israel kwa mujibu wa sheria zote za kimataifa. &#8220;Haikubaliki kuona chama kimoja cha soka kinaendesha shughuli zake katika ardhi ya mwenzake,&#8221; alisisitiza.<\/p>\n\n\n\n<p>Ikumbukwe, Rajoub ni miongoni mwa viongozi wenye misimamo mikali, ambapo mwaka 2018 alifungiwa na FIFA kwa kuhamasisha mashabiki kuchoma jezi ya Lionel Messi kuelekea mchezo wao dhidi ya Argentina.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>VANCOUVER, Canada HIVI karibuni, ulifanyika Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) mjini Vancouver na tukio lililotikisa zaidi ni lile la viongozi wa mchezo huo katika mataifa ya Palestina na Israel kukataa kupiga picha ya pamoja. Ni Rais wa Chama cha Soka cha Palestina, Jibril Rajoub, na Makamu wa Rais wa Chama cha [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":8,"featured_media":10113,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":true,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[81],"tags":[],"coauthors":[203],"class_list":{"0":"post-10172","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-makala-kimataifa"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/05\/fifa.jpeg?fit=1980%2C1320&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10172","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/8"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=10172"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10172\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":10173,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10172\/revisions\/10173"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/10113"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=10172"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=10172"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=10172"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=10172"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}