{"id":10132,"date":"2026-05-02T16:25:14","date_gmt":"2026-05-02T16:25:14","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10132"},"modified":"2026-05-02T16:25:20","modified_gmt":"2026-05-02T16:25:20","slug":"namibia-ya-maliza-deni-la-imf","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10132","title":{"rendered":"NAMIBIA YA MALIZA DENI LA IMF"},"content":{"rendered":"\n<p>Rais wa Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah, ameiongoza nchi yake kufikia hatua muhimu ya kiuchumi baada ya kukamilisha malipo yote ya deni la Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). <\/p>\n\n\n\n<p>Namibia imelipa jumla ya dola milioni 23.9, hatua inayotajwa kupunguza mzigo wa madeni ya nje na kuongeza uthabiti wa uchumi wa taifa hilo. Mafanikio hayo yamepokelewa kama ishara ya usimamizi mzuri wa fedha za umma chini ya uongozi wa sasa.<\/p>\n\n\n\n<p>Kukamilika kwa deni hilo kunatajwa kuipa Namibia uhuru mkubwa zaidi wa kifedha, huku serikali ikitarajiwa kuwa na nafasi pana ya kuelekeza rasilimali katika miradi ya maendeleo ya ndani. <\/p>\n\n\n\n<p>Kwa mujibu wa takwimu hadi Machi mwaka huu, malipo hayo yalifikia dola milioni 23.8875. Namibia sasa imejiunga na baadhi ya mataifa ya Afrika yaliyofanikiwa kufuta madeni yao kwa IMF, ikiwemo Msumbiji.<\/p>\n\n\n\n<p>Netumbo Nandi-Ndaitwah, mwenye umri wa miaka 72, ndiye rais wa kwanza mwanamke wa Namibia. Aliingia madarakani mwezi Disemba 2024 baada ya kushinda uchaguzi kwa asilimia 57 ya kura, huku mpinzani wake wa karibu Panduleni Itula akipata asilimia 26. <\/p>\n\n\n\n<p>Tangu akiwa na umri wa miaka 14, amekuwa mwanachama wa chama tawala cha SWAPO, hatua iliyomjengea historia ndefu ya kisiasa nchini humo.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Rais wa Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah, ameiongoza nchi yake kufikia hatua muhimu ya kiuchumi baada ya kukamilisha malipo yote ya deni la Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Namibia imelipa jumla ya dola milioni 23.9, hatua inayotajwa kupunguza mzigo wa madeni ya nje na kuongeza uthabiti wa uchumi wa taifa hilo. Mafanikio hayo yamepokelewa kama ishara [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":10,"featured_media":10133,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":true,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[74],"tags":[],"coauthors":[253],"class_list":{"0":"post-10132","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-habari-kimataifa"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/05\/NAMIBIA.jpeg?fit=735%2C912&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10132","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/10"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=10132"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10132\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":10134,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10132\/revisions\/10134"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/10133"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=10132"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=10132"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=10132"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=10132"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}