{"id":10097,"date":"2026-05-02T15:55:02","date_gmt":"2026-05-02T15:55:02","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10097"},"modified":"2026-05-02T15:55:09","modified_gmt":"2026-05-02T15:55:09","slug":"simba-v-yanga-dakika-90-za-kisasi-heshima-ligi-kuu-bara-wikiendi-hii","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10097","title":{"rendered":"SIMBA v YANGA: DAKIKA 90 ZA KISASI, HESHIMA LIGI KUU BARA WIKIENDI HII"},"content":{"rendered":"\n<p>EBWANA ee! Hebu sahau kidogo kile kilichotokea siku chache zilizopita katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, ambako Simba iiifunga Yanga bao 1-0 na kutwaa ubingwa wa Kombe la Muungano.<\/p>\n\n\n\n<p>Jumapili ya wiki hii, Mei 3, 2026, vigogo hao wa soka la Tanzania wataoneshana tena kazi katika dakika 90 za &#8216;derby&#8217; ya Ligi Kuu Bara itakayochezwa kwenye Uwanja wa Jenerali Isamuhyo.<\/p>\n\n\n\n<p>MECHI YA KISASI<br>Yanga wakiwa wageni wa mchezo, watashuka dimbani wikiendi hii wakiwa hawajasahau maumivu waliyoachiwa na Simba katika mchezo wa Jumatano ya wiki hii, Aprili 29, 2026.<\/p>\n\n\n\n<p>Ukiwa ni mtanange wa fainali ya Kombe la Muungano, timu hizo zikiwa zimebakiza sekunde chache kumaliza dakika 120 (90 + 30), Clatous Chama alisababisha penalti baada ya kuchezewa rafu ndani ya boksi la Yanga.<\/p>\n\n\n\n<p>Seleman Mwalim alipiga mkwaju huo wa penalti na kufunga bao pekee hilo lililozamisha jahazi la Yanga na kuipa Simba ubingwa wake wa saba wa michuano hiyo.<\/p>\n\n\n\n<p>Hivyo, wakati Yanga wakiiona mechi ya wikiendi hii ni nafasi ya kulipiza kisasi kwa kile walichofanyiwa Visiwani Zanzibar, Simba watatamani kutonesha kidonda cha wapinzani wao hao. Patamu hapo!<\/p>\n\n\n\n<p>VITA YA KILELENI MWA MSIMAMO<br>Achilia mbali ishu ya kisasi, timu hizo zinakutana katika wakati ambao zinapeana presha kubwa katika nafasi mbili za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu.<\/p>\n\n\n\n<p>Kila moja imeshacheza mechi 19 na Yanga &#8216;Timu ya Wananchi&#8217; wako kileleni wakiwa na pointi 47, wakiizidi tano tu Simba inayoshika nafasi ya pili.<\/p>\n\n\n\n<p>Hivyo, endapo &#8216;Wekundu wa Msimbazi&#8217; watashinda wikiendi hii, watabakiza pointi mbili pekee kuifikia Yanga. Kinyume chake, Yanga wakishinda wataongeza pengo la pointi na kufikia nane.<\/p>\n\n\n\n<p>MWENDO WA MABAO TU<br>Katika mechi 19 walizoshuka dimbani msimu huu, mabingwa watetezi msimu huu wa Ligi Kuu Bara, Yanga, wameshinda 14 na kutoa sare tano.<\/p>\n\n\n\n<p>Mechi hizo zimeishuhudia Yanga ikiongoza kwa upachikaji mabao (44), pia ikiwa ndiyo timu iliyoruhusu nyavu zake kutikiswa mara chache zaidi (3).<\/p>\n\n\n\n<p>Kwa upande wa Simba, katika michezo 19 waliyocheza kufikia hatua hii ya msimu wa Ligi, wameshinda 12, sare sita na kufungwa mmoja.<\/p>\n\n\n\n<p>Simba, kwa upande wao, wameshafunga mabao 32, huku safu ya ulinzi ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara saba pekee.<\/p>\n\n\n\n<p>SOMA HAPA<br>Vigogo hao wa Ligi Kuu Bara, Yanga na Simba, watakutana kwa mara ya pili msimu huu wa Ligi Kuu Bara baada ya matokeo ya suluhu (0-0) katika mchezo wa kwanza.<\/p>\n\n\n\n<p>Kwamba timu itakayoshinda wikiendi hii, itajivunia kumaliza msimu huu ikiwa imezoa pointi nne za mpinzani wake. Je, ni Simba au ni Yanga? Tusubiri.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>EBWANA ee! Hebu sahau kidogo kile kilichotokea siku chache zilizopita katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, ambako Simba iiifunga Yanga bao 1-0 na kutwaa ubingwa wa Kombe la Muungano. Jumapili ya wiki hii, Mei 3, 2026, vigogo hao wa soka la Tanzania wataoneshana tena kazi katika dakika 90 za &#8216;derby&#8217; ya Ligi Kuu Bara [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":8,"featured_media":10098,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":true,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[79],"tags":[],"coauthors":[203],"class_list":{"0":"post-10097","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-michezo"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/05\/256bdba7-3c6a-4064-8a71-0d5a3957bfb1.jpeg?fit=554%2C554&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10097","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/8"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=10097"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10097\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":10099,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10097\/revisions\/10099"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/10098"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=10097"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=10097"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=10097"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=10097"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}