{"id":10076,"date":"2026-05-02T15:39:42","date_gmt":"2026-05-02T15:39:42","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10076"},"modified":"2026-05-02T15:39:47","modified_gmt":"2026-05-02T15:39:47","slug":"mabeki-wa-kati-wanaowindwa-real-madrid","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10076","title":{"rendered":"MABEKI WA KATI WANAOWINDWA REAL MADRID"},"content":{"rendered":"\n
MADRID, Hispania
KWA sasa, Real Madrid inahusishwa na usajili wa beki wa kati katika dirish kubwa la kiangazi, mwishoni mwa msimu huu.<\/p>\n\n\n\n
Uhitaji huo unatokana na mwenendo wa kikosi hicho, ambapo safu take ya ulinzi imekuwa ikiruhusu mabao.<\/p>\n\n\n\n
‘Pacha’ ya Eder Militao na Antonio R\u00fcdiger imekuwa ikiteswa na majeraha ya mara kwa mara ya nyota hao, huku Raul Asencio na David Alaba wakihusishwa na mpango wa kuondoka.<\/p>\n\n\n\n
Hivyo, licha ya uwepo wa makinda Joan Mart\u00ednez na Diego Aguado, ni wazi Madrid ya msimu ujao itahitaji usajili wa beki wa kati mwenye uzoefu.<\/p>\n\n\n\n
JOHN STONES
Madrid imeripotiwa kumtaka beki huyo ambaye ameshatangaza kuwa huu ni msimu wake wa mwisho kuitumikia Manchester City.<\/p>\n\n\n\n
Hata hivyo, licha ya uwezo, uzoefu na mafanikio yake, Stones ni mchezaji mwenye historia nzuri ya majeraha ya mara kwa mara.<\/p>\n\n\n\n
IBRAHIMA KONATE
Kwa misimu miwili mfululizo, Madrid imejaribu kumsajili beki huyo wa Liverpool. Walimkosa kidogo tu mwaka jana.<\/p>\n\n\n\n
Aprili, 2026, nyota huyo wa zamani wa RB Leipzig aliweka wazi, kwamba anataka kubaki Anfield kwa misimu mingi ijayo.<\/p>\n\n\n\n
ALESSANDRO BASTONI
Mbali ya ubora wa pasi, Bastoni anayekipiga Inter Milan ni mzuri pia katika kucheza mipira ya juu kutokana na urefu wake wa futi 6 na inchi 3.<\/p>\n\n\n\n
Madrid wanakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Barcelona, ambayo pia imeripotiwa kumtaka Muitalia huyo mwenye umri wa miaka 27.<\/p>\n\n\n\n
CRISTIAN ROMERO
Mkataba wake na Tottenham utakwisha mwaka 2029 lakini uwezekano wa kuondoka mwishoni mwa msimu huu ni mkubwa.<\/p>\n\n\n\n
Madrid wanampigia hesabu, ingawa Bayern Munich nayo inamtaka nyota huyo wa kimataifa wa Argentina.<\/p>\n\n\n\n
ANTONIO SILVA
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22, amebakiza miezi 12 tu katika mkataba wake na Benfica ya Ligi Kuu nchini Ureno.<\/p>\n\n\n\n
Kocha wa Benfica, Jose Mourinho, ambaye pia anahusishwa na mpango wa kurudi Madrid, amekuwa akimtaja Silva kuwa ni mmoja ya mabeki wa kati bora duniani.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"
MADRID, HispaniaKWA sasa, Real Madrid inahusishwa na usajili wa beki wa kati katika dirish kubwa la kiangazi, mwishoni mwa msimu huu. Uhitaji huo unatokana na mwenendo wa kikosi hicho, ambapo safu take ya ulinzi imekuwa ikiruhusu mabao. ‘Pacha’ ya Eder Militao na Antonio R\u00fcdiger imekuwa ikiteswa na majeraha ya mara kwa mara ya nyota hao, […]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":10077,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":true,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[215],"tags":[],"coauthors":[201,203],"class_list":{"0":"post-10076","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-michezo-kimataifa"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/05\/mabeki.jpeg?fit=399%2C501&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10076","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=10076"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10076\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":10078,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10076\/revisions\/10078"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/10077"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=10076"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=10076"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=10076"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=10076"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}