{"id":10041,"date":"2026-04-29T14:14:05","date_gmt":"2026-04-29T14:14:05","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10041"},"modified":"2026-04-29T14:14:11","modified_gmt":"2026-04-29T14:14:11","slug":"serikali-yaimarisha-usambazaji-wa-chanjo-ikizindua-boti-7-za-bilion1-1","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10041","title":{"rendered":"SERIKALI YAIMARISHA USAMBAZAJI WA CHANJO IKIZINDUA BOTI 7 ZA BILION1.1"},"content":{"rendered":"\n<p>Serikali imeendelea kuimarisha huduma za chanjo nchini kupitia uzinduzi wa boti saba zenye thamani ya shilingi Bilioni 1.1 zitakazosaidia kusambaza chanjo na huduma nyingine za afya ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya kwa wakati.<\/p>\n\n\n\n<p>Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema hayo leo Aprili 29, 2026 katika hafla ya makabidhiano ya boti kwa ajili ya huduma za chanjo, ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya afya Kitaifa iliyofanyika katika bandari ya Nyamisati iliyopo Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani.<\/p>\n\n\n\n<p>&#8220;Hatua hii imezingatia viwango vyote vya usalama wa majini, ambapo kila moja imewekewa vifaa vya kujiokoa pamoja na kuzingatia uwezo maalum wa kubeba abiria na watumishi wa afya kulingana na taratibu zilizowekwa,&#8221; amesema Mhe. Mchengerwa<\/p>\n\n\n\n<p>Aidha, Mhe. Mchengerwa, amezitaka Halmashauri zilizonufaika kuzitunza boti hizo ili ziweze kudumu na kuendelea kutoa huduma kwa wananchi kwa muda mrefu, kwa kuwa ni mali za umma na ni amana ya wananchi ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa ya kuwafikia wananchi waliopo katika maeneo ambayo hayawezi kufikika Kwa urahisi.<\/p>\n\n\n\n<p>\u201cHalmashauri ziweke utaratibu mzuri wa matengenezo, ratiba za matumizi, usimamizi wa mafuta pamoja na ufuatiliaji wa matokeo ya huduma zinazotolewa, boti hizi zisibaki kuwa alama ya sherehe ya leo, bali ziwe sehemu ya kazi za kila siku katika kuwafikia wananchi wanaohitaji huduma za chanjo,&#8221; amesema Mhe. Mchengerwa<\/p>\n\n\n\n<p>Aidha Mchengerwa ameongeza kuwa uwekezaji huo utaongeza uwezo wa utoaji wa huduma za mkoba na tembezi, kusimamia utoaji wa chanjo kwa ufanisi pamoja na kuwafikia watoto ambao hapo awali walikuwa wakikosa huduma kutokana na changamoto za usafiri.<\/p>\n\n\n\n<p>Katika hatua nyingine, Mhe. Mchengerwa amewapongeza watumishi wa sekta ya afya kwa kujitolea kwao katika kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi, akisisitiza kuwa mafanikio ya huduma za afya hayategemei vifaa pekee, bali pia weledi, nidhamu na moyo wa kujituma wa watumishi.<\/p>\n\n\n\n<p>Sambamba na hayo Mhe. mchengerwa amewashukuru wadau wakiwemo GAVI, Shirika la Afya Duniani (WHO), pamoja na UNICEF kwa kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuimarisha huduma za afya nchini ambapo ushirikiano huo umeendelea kuleta matokeo chanya kwa wananchi kupitia huduma bora za chanjo na kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Serikali imeendelea kuimarisha huduma za chanjo nchini kupitia uzinduzi wa boti saba zenye thamani ya shilingi Bilioni 1.1 zitakazosaidia kusambaza chanjo na huduma nyingine za afya ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya kwa wakati. Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema hayo leo Aprili 29, 2026 katika hafla ya [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":10,"featured_media":10042,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":true,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[253],"class_list":{"0":"post-10041","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-habari-kitaifa"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/04\/1c291b9b-91ef-4f67-8918-d44f4e9e13f0.jpeg?fit=480%2C320&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10041","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/10"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=10041"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10041\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":10043,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10041\/revisions\/10043"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/10042"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=10041"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=10041"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=10041"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=10041"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}