{"id":10001,"date":"2026-04-27T10:58:00","date_gmt":"2026-04-27T10:58:00","guid":{"rendered":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10001"},"modified":"2026-04-27T10:58:08","modified_gmt":"2026-04-27T10:58:08","slug":"serikali-yaweka-wazi-mkakati-wa-kuifanya-sekta-ya-madini-kuwa-mhimili-wa-uchumi","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/?p=10001","title":{"rendered":"SERIKALI YAWEKA WAZI MKAKATI WA KUIFANYA SEKTA YA MADINI KUWA MHIMILI WA UCHUMI"},"content":{"rendered":"\n<p>Akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2026\/2027 bungeni jijini Dodoma leo Aprili 27, 2026, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, ameeleza kuwa mkazo utawekwa katika kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli ili kuongeza mapato ya Serikali na kuhakikisha rasilimali za madini zinawanufaisha Watanzania.<\/p>\n\n\n\n<p>Miongoni mwa vipaumbele vilivyotajwa ni pamoja na kuongeza mchango wa sekta ya madini kwenye pato la taifa, kuendeleza mnyororo wa thamani wa madini muhimu na ya kimkakati, pamoja na kuhamasisha uwekezaji katika shughuli za uongezaji thamani ya madini ndani ya nchi.<\/p>\n\n\n\n<p>Aidha, Serikali inalenga kuimarisha uendeshaji wa minada na maonesho ya madini ya vito ili kuongeza uwazi na tija katika biashara ya madini, huku ikiwekeza zaidi katika tafiti za kina zitakazosaidia kugundua na kuendeleza rasilimali mpya za madini.<\/p>\n\n\n\n<p>Katika kuhakikisha ushirikishwaji mpana wa wananchi, Wizara pia imejipanga kuwarasimisha na kuwaendeleza wachimbaji wadogo, ambao ni sehemu muhimu ya sekta hiyo, pamoja na kuzijengea uwezo taasisi zilizo chini ya wizara ili ziweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2026\/2027 bungeni jijini Dodoma leo Aprili 27, 2026, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, ameeleza kuwa mkazo utawekwa katika kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli ili kuongeza mapato ya Serikali na kuhakikisha rasilimali za madini zinawanufaisha Watanzania. Miongoni mwa vipaumbele vilivyotajwa ni pamoja na kuongeza mchango wa sekta [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":10002,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"tdm_status":"","tdm_grid_status":"","_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":true,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2}},"categories":[69],"tags":[],"coauthors":[201,253],"class_list":{"0":"post-10001","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","5":"has-post-thumbnail","7":"category-habari-kitaifa"},"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_featured_media_url":"https:\/\/i0.wp.com\/tanzaniapanorama.com\/wp-content\/uploads\/2026\/04\/93c1c85b-3eb8-44be-8434-57fd78c51475.jpeg?fit=480%2C320&ssl=1","jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10001","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=10001"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10001\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":10003,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/10001\/revisions\/10003"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/10002"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=10001"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=10001"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=10001"},{"taxonomy":"author","embeddable":true,"href":"https:\/\/tanzaniapanorama.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcoauthors&post=10001"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}