Thursday, May 15, 2025
spot_img

Yanga mdomoni kwa Watunisia

DROO ya hatua ya mchujo kuwania kutinga makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) imemalizika, ambapo Yanga itacheza na Club Africain ya nchini Tunisia.

Mchezo wa kwanza baina ya timu hizo utafanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Novemba 2, 2022 na kurudiana wiki mbili baadaye nchini Tunisia.

Katika hatua ya 32 Bora, Club Africain ilicheza na Kipanga ya Zanzibar, ambapo mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, timu hizo hazikufungana, lakini ziliporudiana nchini Tunisia mwishoni mwa wiki, Club Africain ilishinda mabao 7-0.

Yanga wameangukia michuano ya shirikisho baada ya kutolewa kwenye mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya