Sunday, August 24, 2025
spot_img

Je, Arsenal wanaelekea kufanya maajabu kama ya Leicester City msimu huu?

Bado ni mapema sana kwani ligi yenyewe ndio kwanza iko katika mzunguko wa 10, lakini kile kinachoendelea katika ligi hiyo hivi sasa, hususan kileleni mwa msimamo wa ligi yenyewe, kimewafanya watu wawe na mijadala kuhusu wanaoongoza ligi hiyo hivi sasa.

Manchester City wamefanya usajili wa mshambuliaji anayetisha duniani, Halaand, Liverpool walikuwa na msimu mzuri tu mwaka jana, Man United walifanya usajili wa kocha mwenye ujuzi mkubwa tu, huku Chelsea wakiwa chini ya umiliki mpya, wakiwa pia wamefanya sajili zilizoonekana kuwa zingeifanya iwe timu ya kuleta changamoto.

Katikati ya hayo, hakuna mtu aliyekuwa akiwaongelea sana Arsenal licha ya kusajili wachezaji wawili kutoka Man City, ambao walichukuliwa kuungana na damu changa ambazo msimu uliopita zilionyesha kandanda safi kabisa.

Hata hivyo, licha ya kuwa hawakuwa wakiongelewa sana, huku wengi wakitarajia wawe watu wa kuwania nafasi ya nne na ya mwisho ya kushiriki michuano ya Klabu bingwa Ulaya, Arsenal hivi sasa wako kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, wakiwa na alama 27, ikiwa ni alama nne mbele ya Manchester City na Tottenham, ambao wote walitajwa kuwa na vikosi imara zaidi kuliko msimu uliopita.

Licha ya ukweli huo kuhusu Spurs, Man City, Liverpool, Man United ba hata Chelsea, ligi ya Uingereza ni miongoni mwa ligi ambao kila baada ya miaka kadhaa huleta maajabu. Maajabu ya hivi karibuni kabisa yakiwa Arsenal kumaliza msimu bila kupoteza pambano na Leicester City kutwaa ubingwa bila kutarajiwa.

Ni historia hii ya maajabu ya ligi hiyo, ambayo inawavuta watu vijiweni hivi sasa, wakikaa na kujadili je, Arsenal yenye damu changa sana, inaweza kuonyesha maajabu na kwenda kutwaa ubingwa wa EPL kwa mara ya kwanza tangu walipofanya hivyo mara ya mwisho mwaka 2004.

Je, wewe kama mpenzi wa soka, una maoni na mtazamo gani kuhusu mwenendo wa EPL msimu huu?

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya