MAKOCHA mbalimbali wa soka wametakiwa kujitokeza kushiriki kozi ya ukocha ngazi ya Diploma D, iliyopangwa kufanyika Julai 5 hadi 14, mwaka huu, wilayani Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na PANORAMA, mratibu wa mafunzo hayo, Issa Yahya, alisema milango ipo wazi kwa makocha waliosoma kozi ya ukocha ngazi ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF Grass root) .
Yahya alisema uthibitisho wa kushiriki mafunzo hayo utakwenda na washiriki kulipa ada Sh. 190,000.
” Maandalizi yanaendelea vizuri na tunaendelea kuhamasisha wadau kujitokeza kwa wingi kushiriki kozi kwa lengo la kupata elimu hii kwa manufaa ya Wilaya na Taifa kwa ujumla,” alisema Yahya.
Mratibu huyo alisema lengo la kozi hiyo ni kuzalisha makocha wengi na kuwaongezea ujuzi na maarifa ili waweze kwenda na wakati uliopo.