NYOTA wa zamani wa Timu ya Soka ya Tanzania, Taifa Stars, Bakari Malima, Jembe Ulaya’, amesema klabu ya Yanga inatakiwa kumtafuta mbadala wa kiungo mkabaji, Khalid Aucho ili kukiboresha kikosi chao cha msimu ujao.
Jembe Ulaya ambaye pia beki kisiki wa zamani wa Yanga, alisema kutokana na Aucho ametumika kwa muda mrefu ni vizuri akatafutiwa msaidizi mwingine mwenye uwezo zaidi wa kupiga soka.
Alisema Aucho anaonekana anachezea uzoefu kutokana na umri kuwa mkubwa, hivyo kunahitajika mbadala wake.
Aucho ambaye ni raia wa Uganda ameichezea Yanga kwa mafanikio makubwa tangu alipotua Jangwani misimu mitatu iliyopita.