Friday, July 4, 2025
spot_img

JULIO ATOA SOMO KWA SIMBA

KOCHA wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Jamhuri Kihwelo, ‘Julio’, ametoa wito kwa wanachama na viongozi wa klabu hiyo, kuendelea kushikamana pamoja, wakati wakijiandaa na msimu mpya wa michuano ijayo.

Simba wamemaliza nafasi ya pili msimu wa 2024/2025 wa Ligi Tanzania Bara, huku wakishindwa kutwaa ubingwa kwa miaka minne mfululizo, mara zote ukienda kwa watani wao wa jadi Yanga.

Kutokana na Wekundu wa Msimbazi hao kushindwa kutwaa kombe hilo, Julio alisema mashabiki wa timu hiyo wanatakiwa kutulia na kuwa kitu kimoja huku benchi la ufundi likiendelea kujenga kikosi bora.

Julio ambaye ni beki wa zamani wa Simba na Taifa Stars alisema mashabiki wa timu hiyo hawatakiwi kuwa wanyonge kwa kushindwa kutwaa ubingwa wa ndani kwa muda mrefu.

Kocha huyo alisema katika kipindi hiki cha kuelekea usajili wa wachezaji wapya wanasimba wanatakiwa kujenga umoja na mshikamano huku wakiwaacha maskauti ya wachezaji kufanya kazi yao.

“Simba wasilalamike timu yao pamoja na inajengwa msimu uliopita walifika fainali michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, sio haba,” alisema Julio.

Pia alisema pamoja na mashabiki hao kulalamikia timu yao kutofanya vizuri Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini wanashindwa kutambua wapi wamejikwaa.

Katika msimu uliopita, Simba walishindwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufungwa na AS Berkane ya Morocco kwa jumla ya mabao 3_1. Kwa sasa klabu ya Simba inajipanga na msimu mpya wa michuano ya ndani na LIgi ya Mabingwa Afrika.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya