Friday, July 4, 2025
spot_img

BEKI ALIYEWINDWA SIMBA KUTUA AZAM

KLABU ya Azam inatarajia kukamilisha usajili wa beki wa kati wa timu ya Coastal Union, Lameck Lawi, kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano mingine.

Beki huyo msimu uliopita alitajwa kuwindwa na vigogo wa soka nchini Simba, ambao walishindwa kumtwaa baada ya dili kukwama.

Hata hivyo, imeelezwa Azam imefanya kweli baada ya kufikia makubaliano mazuri na beki huyo ili aweze kuichezea timu yao msimu ujao.

Chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya Klabu ya Azam, kimesema tayari beki huyo amesaini mkataba wa miaka miwili.

Lawi anakuwa mchezaji mzawa ambaye anakwenda pambania kucheza katika kikosi cha kwanza wakiwamo mabeki wengine wa kigeni, Yeison Fuentus na Yoro Diaby.

Kikosi cha Azam kinajiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya Kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya