Saturday, April 19, 2025
spot_img

CHALAMILA ATAKA KASI UPANUZI BARABARA YA UBUNGO – KIMARA

ZERUBABEL CHUMA,

Dar es Salaam

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amemtaka mkandarasi anayefanya upanuzi wa barabara ya Morogoro, eneo la Ubungo Mataa hadi Kimara kuongeza kasi ya ujenzi.

Chalamila alitoa agizo hilo jana akiwa katika siku ya pili ya ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na serikali wilayani Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Alisema mradi huo ni kiungo muhimu kwenye ukuaji wa uchumi hivyo ni budi ukamilike kwa wakati. Hivi sasa umefikia asilimia 45.

Akizungumza na wananchi wa eneo hilo, Chalamila alisema serikali imekwishaandaa mpango wa kupata magari ya kutosha ya mwendo kasi na kuwepo watoa huduma wengi badala ya mmoja, UDART.

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Lazaro Twange aliyeandamana na Chalamila kwenye ziara hiyo alisema, serikali inapanua barabara hiyo ili kupunguza msongamano wa magari.

Katika ziara hiyo, pia Chalamila alitembelea mradi wa Shule ya Msingi Msewe na Kituo cha Afya Makurumla.

MATUKIO KATIKA PICHA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, ALBERT CHALAMILA AKIKAGUA UPANUZI WA BARABARA YA UBUNGO ENEO LA UBUNGO – MATAA HADI KIMARA NA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya