Wednesday, March 12, 2025
spot_img

MAKUMBUSHO YA MKWAWA ‘YASUKWA’ UPYA

This image has an empty alt attribute; its file name is makala-LOGO-4-1024x197.jpg

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ‘limeisuka’ upya Makumbusho ya Chifu Mtwa Mkwawa, na sasa watalii kutoka nje ya nchi wanaweza kupata huduma zote muhimu wakiwa ndani ya makumbusho hiyo.

Serikali iliiweka makumbusho hiyo chini ya TANAPA mwaka 2019 baada ya kusuasua kwa muda mrefu katika utoaji huduma; na mwaka 2023 menejimenti mpya ya TANAPA ilianza kuisuka upya kwa kuimarisha miundombinu ya barabara na majengo, likiwemo jengo la Makumbusho ya Chifu Mkwawa.

Msaidizi wa Mkuu wa Makumbusho hiyo, Mhifadhi wa Malikale Daraja la Pili, Paulo Mduma anaeleza kuwa uwezekezaji mkubwa uliofanywa na TANAPA umekuwa na matokeo Chanya.

This image has an empty alt attribute; its file name is IMG_1463-683x1024.jpg

Paulo Mduma, Mhifadhi wa Malikale Daraja la Pili katika Makumbusho ya Chifu Mtwa Mkwawa iliyopo Kalenga, Iringa.

Anasema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 idadi ya watalii imeongezeka hadi kufikia 1695 kutoka watalii 1521 waliotembelea makumbusho hiyo, mwaka 2022/2023.

Mduma anasema hadhi ya makumbusho hiyo sasa ni ya kuridhisha baada ya TANAPA kuweka miundombinu ya umeme wa sola na huduma ya internet ambayo ni muhumu kwa watalii wa ndani na nje ya nchi.

Anasema ndani ya makumbusho kumefanyiwa ukarabati wa kabati za kuhifadhia vionyeshi ndani ya makumbusho na majengo yaliyojengwa na wakoloni wa Kiingereza nayo yamekarabatiwa.

This image has an empty alt attribute; its file name is waitara.webp

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Jenerali Mstaafu, George Waitara.

“Tunaishukuru hii menejimenti ya sasa na tunaishukuru sana Bodi ya TANAPA kwa kuituipia macho makumbusho hii. Umefanyika ukarabati mkubwa wa vitu vilivyokuwa vimechakaa, sasa kuna umeme wa uhakika, kuna internet. Huduma zote muhimu kwa watalii kwa sasa zipo bado maboresho kidogo kidogo tu, tunawaomba wazidi kuiimarisha kwani sehemu hii ikikaa vizuri ni kituo muhimu sana cha utalii,” anasema Mduma.

Makumbusho kumbukizi ya Chifu Mkwawa ni kituo kilichohifadhi historia ya wabantu wa Kabila la Wahehe ambao walikuwa shupavu katika kupigana vita na kushinda mwishoni mwa karne ya 18 na 19.

Chifu Mkwawa alikuwa kiongozi shupavu aliyepigana na majeshi ya Wajerumani na kuyashinda katika vita iliyopiganwa eneo la Lugalo, mwaka 1891.

Katika vita hivyo Chifu Mkwawa na jeshi lake waliwaangamiza zaidi ya wanajeshi 300 wa Kijerumani akiwamo kamanda wao, Emil Von Zelewisky.

Kituo cha Makumbusho Kumbukizi cha Chifu Mkwawa kina shughuli za utalii wa kitamaduni, maelezo ya historia na kutembelea makumbusho.

Zana za kivita zilizo Makumbusho ya Chifu Mkwawa

Vivutio vilivyo ndani ya makumbusho hiyo ni pamoja na fuvu la kichwa cha Chifu Mkwawa na vifaa alivyotumia wakati wa uhai wake, mabaki ya ngome ya Lipuli, mnara wa Lugalo ambako Chifu Mkwawa alipigana vita na Wajerumani na kaburi la Nyundo ambako wanajeshi zaidi ya 300 wa Kijerumani waliouwawa na Mkwawa walizikwa.

Daraja la Mungu.

Pia kuna kaburi la kiwiliwili cha Chifu Mkwawa na mnara wa kumbukumbu ya miaka 100 baada ya kifo chake na Daraja la Mungu; eneo ambalo mama yake Chifu Mkwawa alipotelea.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya