Wednesday, March 12, 2025
spot_img

KAPINGA, MRAMBA WATOA NENO MKUTANO WA EAPCE’25 

TERESIA MHAGAMA

NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mhandisi Felchesmi Mramba wamewataka washiriki wa mkutano wa awali kuelekea kongamano la 11 la mafuta kwa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAPCE’25), kujadili mambo yatayoisaidia sekta ya mafuta ya gesi.

Naibu Waziri Kapinga ambaye alizungumza kwanza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam, alisema mkutano uweka msingi wa kongamano la 11 la mafuta kwa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki linaloanza leo jijini hapa.

“Siku ya leo kutakuwa na mada mbalimbali zitakazozungumzwa ambazo zitakuwa na majadiliano yatakayoweka msingi kwa ajili ya mkutano mkuu utakaoanza kesho (leo) na kufanyika kwa siku tatu.

“Mkutano huu ni muhimu uwaweka wadau pamoja na kujadiliana masuala ya msingi ambayo yatazisaidia Nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki katika Sekta ya Mafuta na Gesi,” alisema Kapinga.

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba alisema mkutano huo unaenda sambamba na maonesho ya bidhaa za mafuta na gesi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba

Alisema mkutano  unalenga kuangalia namna bora ya kuhama kutoka kwenye nishati zinazochafua mazingira kwenda kwenye nishati safi zisizochafua mazingira.

Mramba alisema dunia ipo kwenye kampeni ya matumizi ya nishati safi na malengo yaliyopo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2050 hadi 2060, dunia iwe imehamia kwenye nishati safi kwa kiasi kikubwa.

“Katika mkutano huu, nchi zitapata nafasi ya kuelezea maendeleo waliyofanya katika eneo la mafuta na gesi ambapo makatibu wakuu na mawaziri watazungumza kuhusu mafanikio, mipango na kazi zilizofanyika tangu kufanyika kwa mkutano uliopita wa EAPCE,” alisema.

Alisema katika mkutano huo wataalamu, watafiti na wabunifu watazungumzia ugunduzi wa mafuta na gesi, sehemu ambazo vitalu vinaandaliwa na kukaribisha uwekezaji kwa nchi za EAC.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya