Friday, March 14, 2025
spot_img

MABILIONI YACHOTWA TANESCO

RIPOTA PANORAMA

GENGE la mafisadi papa linachota taratibu mabilioni ya fedha kwenye Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco).

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Tanesco na nyaraka zilizoonwa na Tanzania PANORAMA Blog vimeonyesha kuwa genge hilo linachota mabilioni hayo kwa kushirikiana na watumishi wasio waaminifu wa Tanesco.

Kwa mujibu wa taarifa, genge hilo lina kampuni ambayo imepewa zabuni na Tanesco ya kuendesha moja ya vituo vya utoaji huduma kwa wateja na kwa kutumia kampuni hiyo limekuwa likitengeneza nyaraka za malipo bandia na kulipwa mabilioni ya shilingi na Tanesco.

Taarifa na nyaraka zilizopo zinaonyesha kuwepo kwa mkataba kati ya Tanesco na kampuni hiyo ambao umefanyiwa maboresho na mmoja wa viongozi wa Tanesco anayetajwa kuwa mshirika wa genge hilo ambaye wadhfa wake hamruhusu kufanya hivyo.

Hata hivyo, taarifa za hivi karibuni zinaonyesha kuwa kiongozi huyo amehamishwa kutoka Tanesco na kupelekwa taasisi nyingine ya umma baada ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko kuanza kufuatilia mwenendo wa utendaji kazi wa viongozi wa shirika hilo.

Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa genge hilo kwa kutumia kampuni iliyopewa zabuni na Tanesco imekuwa ikidai na kulipwa malipo ambayo hayazingatia mkataba na bila kuwa na vielelezo.

Vyanzo vya habari vya ndani ya Tanesco vimeeleza kuwa iliundwa timu ya kuchunguza madai hayo pamoja na mambo mengine ambayo iligundua udanganyifu huo na kuwasilisha ripoti yake kwa uongozi wa juu wa shirika.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko.

Inaelezwa kuwa baadhi ya watumishi wa Tanesco wanaoshirikiana na kampuni hiyo waliandaa taarifa ya uongo ya kuisafisha kampuni hiyo ambayo ilikuwa ikieleza kuwa huduma iliyolipiwa ni ya kukodi magari aina ya Coaster kwa ajili ya kuhudumia mawakala au watumishi wa kituo hicho.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Biteko kabla ya kufanya ziara kwenye kituo kinachoendeshwa na kampuni hiyo hivi karibuni alipewa taarifa zisizo sahihi kuhusu mwenendo wa uendeshaji wa kituo hicho, jambo lililosababisha atoe maelekezo yenye athari hasi kuhusu hatua za kuchukuliwa.

SOMA TANZANIA PANORAMA KESHO UJUE KWA UNDANI SKANDALI HII.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya